hili ndilo tatizo kuu, kwamba vyombo hivi vinatazama mafanikio ya wahandisi kwa kutazama usajili, kumiliki muhuri na barcode.Mkuu Uko Registered kwanza?
Una Muhuri?
Una Barcode?
[emoji3516][emoji2957][emoji851]
Hayo Mengine unayohitaji yatafuata Baadae
Umekuwa registered kama GE,PE au CE? zungukia kampuni za wachina unaweza kupata nafasi..daaah haya maisha bhana nimwendo wa roho mbaya na kukomoana. Nipo registered na ERB toka 2019, ila hadi Leo sijapata hata sehemu ya kujitolea.hata ukienda ruwasa au tarura unaonekana kama mwanga.ninamengi ila ngoja niishie hapa.SIJUI TUTOKE VIPI
Mkuu ERB mbona kwa nafasi yao wanajitahidi sana kusaidia wahandisi wachanga?Wahandisi tutoke vipi? taasisi ambazo zingekuwa zinatusaidia tupige hatua zimesinzia kabisa.
Kazi yao ni kuandaa safari za kutalihi tu kwenye miradi.
Mimi nilitegemea labda tusikie taasisi hizi zikipendekeza namna gani jamii inaweza kuwatumia wataalamu
Mimi nilitegemea kusikia labda wakipendekeza kwa serikali itunge sheria za kuwa na vizazi tofauti makazini kwamba ni lazima kuwe na wazoefu na wanaotafuta ujuzi.
Vijana wanamaliza na kukaa mitaani na hakuna anayeweza kushauri cha kufanya kwa serikali.
Je, waache kufundisha vijana wapya au ubunifu wa namna ya kuwaingiza vizazi vipya?
Wenye dhamana ya kusimamia taaluma hizi wamesinzia FOFOFO
Umekuwa registered kama GE,PE au CE? zungukia kampuni za wachina unaweza kupata nafasi..
Hakuna wanachowasaidiaMkuu ERB mbona kwa nafasi yao wanajitahidi sana kusaidia wahandisi wachanga?
Mbona graduates wanaajiriwa tu ...kumbuka mkuu huwa taasisi inaajiri mtu kwa uwepo wa uhitaji na si kanuniHakuna wanachowasaidia
SEAP programe is a disaster
Wapo waajiri wengi hawaajiri tena wanachukua Trainee na ama hawawalipi na kuwafanyisha kazi wakitegemea walipwe na ERB kupitia SEAP programme au wanawalipa kidogo.
Kilichotakiwa ni taasisi hizi kushauri serikali kutunga kanuni zinazowezesha graduates kuajiriwa.
mfano kwa hapa tulipofika tunahitaji kuona vizazi tofauti vya kihandisi makazini, tunahitaji kuona shughuli za mtaani kwenye jamii zikiingizwa wataalamu.
serikali ikiwatengenezea fursa kupitia kanuni wataajirika na kuingia makazini na sio utaratibu wa sasa wa kuwapa uzoefu bila kutazama saturation ya fursa zilizokuwepo
Bora uwe dalali wa bodaboda inalipaGE, nisha zunguka kampuni kadhaaa ila hakuna tumaini
Pole sana itakubid urud ERB uwaombe wakusaidie upate ufadhili wa SEAP ambayo itaweza kukusaidia kupata uzoefu wa kazi na baadae kusajiliwa kama PE ambapo hautapata msoto wa kazi kama kuwa GE.GE, nisha zunguka kampuni kadhaaa ila hakuna tumaini
Jambo usilolielewa ni kwamba kila mwaka vyuo vinazalisha wataalamu wengi tu.Mbona graduates wanaajiriwa tu ...kumbuka mkuu huwa taasisi inaajiri mtu kwa uwepo wa uhitaji na si kanuni
HATUNA SHIDA KWENYE TRAINING TUNA SHIDA KWENYE LIFE AFTER TRAININGSerikali ihakikishe kila kampuni ya level fulani Tanzania inakuwa na apprentice programes + trainee programs for engineers na wawalipe... hii itasaidia junior engineers kupata uzoefu.
Serikali ihakikishe mtaala wa science na masomo mengine unaendana na uhalisia wa dunia, dunia iko mbali sana kwenye teknolojia, Ni vyema wahitimu wakaandaliwa kulinga na dunia ilipo..Katika hili pia mashuleni elimu iwe ya vitendo sana kuliko nadharia...study tours ziwe za kutosha maviwandani, maofisini, migodini nk..
Serikali ifute kabisa elimu ya kidato cha sita na muda wa elimu ya msingi upunguzwe sambamba na elimu ya chekechea kutolewa mkazo kwa wazazi kupeleka watoto wakiwa na miaka mitatu, na lakwanza iwe miaka 6 huku elimu ya msingi ikiwa miaka mitano...mbadala wa kidato cha sita iwe diploma level kuanzia law, engineering, uhasibu nk huku vyuo hivi vikiwekeza sana kwenye elimu kwa vitendo na wanaotoka na matokeo mazuri wanakwenda vyuo vikuu..
Kuanzia elimu ya msingi na sekondari wanafunzi wawe wanapewa projects na kufanya presentation wao kwa wao mbele ya wazazi, hata kwenda kwenye taasisi tofauti tofauti na mashule mengine tofauti tofauti...
Kwasasa Inasikitisha sana kiwango cha wahitimu wetu kutoka mashuleni na vyuoni ni hatari sana kwa hiki kizazi na uelekeo wa dunia...Serikali ijaribu kuwa sikivu na kuweka nguvu haraka na mapema katika hili vinginevyo Taifa hili litabaki kuwa la watu walalamishi, watu watumwa nk..
Kama hujui kitu bora kua kimya tu, dhihaka haita kusaidiaBora uwe dalali wa bodaboda inalipa
Dhihaka kuwa dalali?Kama hujui kitu bora kua kimya tu, dhihaka haita kusaidia