Ieleweke: Tanzania haijapiga kura kuiunga mkono Palestina; imeunga mkono azimio kusitisha mapigano(humanitarian truce)

Ndimbo M

Member
Aug 30, 2023
13
62
Watu wengi wamepotosha kwa kutokujua kuhusu kitendo cha Tanzania kupiga kura katika baraza la Umoja wa mataifa ijumaa iliyopita kuhusu mzozo baina ya Israel na Hamas/ Palestina. Nasema kupotisha bila kujua kwa vile kuna mmoja kwa mfano,jioni ya leo kafikia hatua ya kusema Tanzania imepiga kura ya veto kuiunga mkono Palestina.

Kwanza anaonesha wazi kabisa haelewi maana kura ya veto, na pia haelewi ukweli kwamba ni nchi tano tu(America, Russia, China, France na UK) ndizo zenye kupiga kura ya veto. Na kura ya veto maana yake ni kupinga,..siyo kura ya kuunga mkono hoja au azimio.

Kwanza ieleweke, Tanzania ilishatoa msimamo wake ambao unataka pande zote zinazohusika katika mapigano katika huo mzozo zisitishe mara moja ili hatua za mazungumzo ya amani zichukue nafasi yake.
Pili, wiki hii kulikuwa na azimio katika baraza la umoja wa mataifa lililotaka wanaohusika kusitisha mapigano ili kuruhusu amani ya kudumu kutamalaki,na ili watu waweze kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahanga.

Sasa azimio ili lipite ni lazima lipigiwe kura...,na kwa vile azimio lenyewe limeendana na msimamo wa Tanzania kwamba pande zote mbili zisitishe mapigano ili kupisha mazungumzo, ndo maana ikapigia kura. Tanzania haijapiga kura kuiunga mkono Palestina kama watu walivyopotosha, imepiga kura kusitisha mapigano ili kupisha huduma za kibinadamu (humanitarian truce)
 
Mtazamo wangu: Wote mnazungumzia kitu kimoja ila kwa lugha tofauti. Ukitaka kujua kama mnazungumzia kitu kimoja. weka hivi:
1) Wapalestina walikuwa na msimamo gani kuhusu kupisha huduma za kibinadamu.
2)Na serikali ya Israel ilikuwa na msimamo gani kuhusu kupisha huduma za kibinadamu?
 
Yule balozi wa Israel UN amesema kura haikuwapendeza,watalivunja jengo la UNO.
Kwa sababu wamesahau UNO ilijengwa kwa sababu gani.
Ilijengwa itetee haki sasa imefanya nini?

It is what he did not say that is important. UNO ilijengwa na Wayahudi. (kwa sababu za kuwasaidia Wayahudi,mambo kama holcaust yalikuwa yanatajwa yasijirudie)
Yule Secretary of State aliyeianzisha UNO alikuwa Myahudi. Alikuwa Nani sijui,Alger Hiss,nadhani.
Kwa hiyo ukimsikia Myahudi anatishia usalama wa jengo la UNO it means just that.
Niko safarini naenda Arusha.
 
Mtazamo wangu: Wote mnazungumzia kitu kimoja ila kwa lugha tofauti. Ukitaka kujua kama mnazungumzia kitu kimoja. weka hivi:
1) Wapalestina walikuwa na msimamo gani kuhusu kupisha huduma za kibinadamu.
2)Na serikali ya Israel ilikuwa na msimamo gani kuhusu kupisha huduma za kibinadamu?
Nilichokisema kinamaanisha kwamba Tanzania imeunga mkono azimio la umoja wa mataifa linalotaka nchi husika wasitishe mapigano kuwezesha misaada ya kibinadamu kwa wahanga.
Sasa ukisema Tanzania imeumga mkono Palestina,tafsiri yake ni kwamba unaunga mkono madai na hoja zote za Palestina katika mzozo wao na Israel. Na hata mtoa mada aliiweka hoja yake katika namna hiyo kiasi cha kuwafanya wachangiaji waandike kwa mtindo wa mabishano kwa kudhani kwamba Tanzania sasa siyo 'neutral' katika mzozo.
Na kitu kingine,alipotosha aliposema Tanzania imepiga kura ya veto kuunga mkono Palestina. Tanzania toka lini ina kura ya veto UN? Kwa hiyo kapotosha mambo mawili kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom