Ielewe fasihi

Ric gifted

New Member
Dec 21, 2015
4
0
Fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa jamii.Kuna fasihi andishi na fasihi simulizi.Nyimbo ni sehemu ya fasihi simulizi.Fasihi ni zao la jamii,kwa sababu hujadili mambo mbalimbali yaliyo katika jamii husika!!Mara nyingi sana wasanii hujadili matatizo mbalimbali kwa aina tofauti kwa kuzingatia,matumizi ya lugha,wahusika,mtindo na muundo wa kazi husika.Ukisoma riwaya ya A MAN OF THE PEOPLE cha Hayati Chinua Achebe,na riwaya ya THE BEAUTYFUL ONES ARE NOT YET BORN cha Ayi,utagundua kuwa vyote vimejikita kujadili uongozi mbaya ila kwa njia tofauti!!Ukiusikiliza wimbo wa Mike tee mnyalu na Wimbo mpya wa Diamondplatnmuz utagundua kuwa dhamira yao kuu ni HOFU ya maisha yao ya baadae endapo watafulia,lakini ukija kuchambua vipengele vya fani katika nyimbo hizo(matumizi ya lugha,wahusika,mtindo na muundo)hapo ndipo utaweza kuelewa kuwa fasihi hujadili suala ama tatizo moja kwa njia tofauti katika kufikisha ujumbe kwa hadhira.Tusipende kujadili vitu kwa hisia za kishabiki na kuusahau ukweli!!
 
Back
Top Bottom