Maisha ni mzunguko ndugu, usifurahie matatizo ya mwenzako. Hujui kesho nini kitakutokea na nani atakusaidia, weka akiba ya maneno.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jikite kwenye sheria na katiba ambayo watu wameapa kuilinda kama hukumu hutolewa na mtu mmoja mahakama za nini?Kamshika paka sharubu , makucha yanamhusu
sishabikii yanayomtokea Idrissa, ila anatakiwa ajifunze pahala pa kufanyia masihara!
Kwa ufupi Idris si mchekeshaji! Hicho kipaji hana! Mr. Khan ameliweka wazi hili aangalie wapi pa kufanya mzaha.Pengine utakuwa umekengeuka kama nwanadamu usitafute kuwaadhibu wale wanaokukosea Mungu pekee mkamilifu hata ww huwa unamlaumu na kumkosea bado kakusimamia unavuta pumz yake vipi kama angekuwa anatoa adhabu kwa kila afanyalo mwanadamu?
SanaaaKwa ufupi Idris si mchekeshaji! Hicho kipaji hana! Mr. Khan ameliweka wazi hili aangalie wapi pa kufanya mzaha.
Unapoishi ndani ya jamii inakubidi utambue silika za watu wanaokuzunguka. Kuna baadhi ya watu hawapendi mizaha kabisa. Ni watu hao katika jamii, inabidi uheshimu msimamo wao na uutambue. Kuna wengine wanapenda mizaha! Ni sehemu nao katika jamii! Inabidi uheshimu msimamo wao na uutambue.
Siafiki anachofanyiwa ila awe na utambuzi huo! Na hiyo fursa ya kulielewa hili walimpatia mara ya kwanza! Karudia tena kwa Bw. Yule asiyependa mizaha. Kajitakia!
sitaki kusema kuhusu hilo, your life your rensponsibility, sasa hivi anasuffer mwenyewe, The same kwa Mdude!Inaonyesha jinsi dikteta alivyofanikiwa kuogopesha watu Tanzania. Hata wachekashaji na wachora katuni hawatakiwi kusema lolote.
Ukiwa Roma ishi kama wanavyoishi waRoma, ukiwa Tanzania ishi kama wanavyoishi waTanzania!Wachekeshaji kina Ticha Mparire na kina Otoyo wa Churchill ingekuwa ni hapa kwetu wangepigwa risasi kabisa !!. Hapa kutabasamu na picha ni kukosa nidhamu ?! Du Tanganyika umepoteza njia [emoji40][emoji87]
Odhis *
Mkuu hauoni jinsi wanavyoteseka hao? mwisho wa siku mahangaiko yatakuja kwako wewe na familia yako!Jpm ni mwanadamu kama wewe kwa nini umwogope mwanadamu mwenzio kiasi hicho? Mungu wa Tanzania? Mbaya sana aisee
Mkuu hata ww leo unatulia kuna watu walihangaika kututoa kwenye huu ukandamizwaji kama mtu kakosea peleka mahakamani wamfunge sasa polisi anafanya nini?Mkuu hauoni jinsi wanavyoteseka hao? mwisho wa siku mahangaiko yatakuja kwako wewe na familia yako!
Hii habari inaharibu uhuru wa watu wote Tanzania.Mwache aendelee kukaa rumande mpaka akili itakapomkaa sawa. Mtu kipaji hana ana kazi ya kujifanya Mockingbird tu. Yeye kila tukio analigeuza mzaha ili afurahishe vi slay queen vinavyo mfollow huko insta.
kipanya aliishaambiwa aongeze kipumi(paji).anachoweka ni kidogo sana.Hii habari inaharibu uhuru wa watu wote Tanzania.
Imajenga precedent mbaya hata kwa Kipanya kuchora cartoon.
Inakuwekea hata wewe mazingira mabaya uweze kukamatwa kwa makosa ya kuungaunga ya kijinga.
Inaweka mazingira ya woga nchi nzima.
Si habari ya kufurahia kwa mtu yeyote mwenye werevu.
Sent from my typewriter using Tapatalk
Idris ametusaidia sana kuonesha jinsi nchi inavyoongozwa kwa maguvu na bila kufuata misingi ya katiba inayoruhusu mtu kucheka anachoona kinamchekesha na kuwasiliana na wengine.sishabikii yanayomtokea Idrissa, ila anatakiwa ajifunze pahala pa kufanyia masihara!
Hao uliowataja wana-vipaji vyao huwezi kuwalinganisha na huyu jamaa anaelazimisha fani!Wachekeshaji kina Ticha Mparire na kina Otoyo wa Churchill ingekuwa ni hapa kwetu wangepigwa risasi kabisa !!. Hapa kutabasamu na picha ni kukosa nidhamu ?! Du Tanganyika umepoteza njia [emoji40][emoji87]
Odhis *
Huenda, lakini tatizo linakuja pale suffering inakuwa kwake yeye na familia yake tu kwa kiasi kikubwa.. je haikuwa bora kwa yeye kukaa kimya? angepungukiwa nini?Idris ametusaidia sana kuonesha jinsi nchi inavyoongozwa kwa maguvu na bila kufuata misingi ya katiba inayoruhusu mtu kicheka anachoona kinamchekesha na kiwasiliana na wengine.
Tatizo si kwamba Idris anatakiwa ajifunze pahala pa kufanya masihara.
Tatizo no kwamba Watanzania wameaninishwa na kukubali kwamba pahala fulani hutakiwi kupafanyia masihara.
Mtu kafanywa Mungu.
Ujinga gani huu.
Sent from my typewriter using Tapatalk
Ni kweli mkuu sikupingi lakini kwanini uteseke na kitu unachoweza kukikwepa? huyu jamaa hateswi na wenye nchi anateswa na wanaotaka waonekane kwa mwenye nchi!Mkuu hata ww leo unatulia kuna watu walihangaika kututoa kwenye huu ukandamizwaji kama mtu kakosea peleka mahakamani wamfunge sasa polisi anafanya nini?
Watu hawaelewi umuhimu wa utawala wa sheria, hadi iwakute.Idadi ya watu wanaosapoti mtu kua rumande kisa picha kuchekwa is very alarming it's like kuna kikao ambacho sikuhudhuria na tulikubaliana kua hakuna kuchekana.
Sasa nashindwa kuelewa. Ni ile wivu wetu wa wabongo kua jamaa ana hao slay queen kukuzidi au ni hicho kikao ndiyo kinamhukumu huyu jamaa.
Idris si Mandela, kwa hiyo, simfananishi na Mandela. Natoa mfano wa Mandela kuonesha point yangu.Huenda, lakini tatizo linakuja pale suffering inakuwa kwake yeye na familia yake tu kwa kiasi kikubwa.. je haikuwa bora kwa yeye kukaa kimya? angepungukiwa nini?
Naielewa sana hoja yako Kiranga, tatizo linakuja anafanya mzaha kwenye taifa la aina gani? wananchi wa nchi gani? ingekuwa mbele idrisa angepiganiwa hata na jamii.. wananchi wengi wa baadhi ya nchi zenye demokrasia ya kweli hawana uoga.. lakini si wa nchi yetu.. Idrisaa anatakiwa agundue hicho kitu!Idris si Mandela, kwa hiyo, simfananishi na Mandela. Natoa mfano wa Mandela kuonesha point yangu.
Mandela alivyofungwa, yeye na familia yake walipata hiyo suffering kwa kiasi kikubwa.
Haikuwa bora kwa Mandela kukaa kimya? Angepungukiwa nini?
Utawala wa sheria unaheshimu katiba.