Nimeangalia sana documentary ya Idi Amin, kimsingi inaonekana kuwa hakuwa na sera yoyote ya kuendeleza nchi zaidi ya kuiangamiza. Utawala wake uliiyumbisha Uganda kwa kiasi kikubwa, na wanawake aliokuwa akiwapa madaraka wengi walikuwa ni vimada wake na sio kama alikuwa akifanya hivyo kwa sababu ya kuona umuhimu wao. Mpaka sasa sijaona kama kuna lolote ambalo mganda anaweza kujivunia kutokana na utawala wa Idi Amin, labda utupe mifano zaidi. Sijui kama kukifanya kiswahili kiwe lugha ya Black Americans ilikuwa idea nzuri na sijui maana yake ilikuwa nini. Yeye mwenyewe alikuwa anajifunza kiingereza kwa nguvu lakini hakufundisha kiswahili nchini mwake.