Idi Amin Dada: Mazuri na Mabaya ya utawala wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idi Amin Dada: Mazuri na Mabaya ya utawala wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Nov 30, 2008.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Idi Amin Dada Rais wa Uganda aliyechukua madaraka toka kwa Milton Obote kwa mapinduzi. Amin alikuwa mkuu wa majeshi ya uganda, pamoja na mabaya yote mtu huyu alikuwa na mitazamo mingi chanya.

  1. Alikuwa na ndoto ya kukifanya kiswahili kiwe lugha ya black Americans

  2. Ni mtu aliyekuwa na mtazamo wa kuwawezesha wanawake katika madaraka. Alikuwa na nadharia ya kwamba kama mwanamke alikuwa na uwezo wa kuhudumia familia, basi hata katika mahoteli ya kimataifa wanawake wapewe nafasi ya kuongoza(ma-manager)

  3. Amini alikuwa na dhana halisi ya uwajibikaji kwa wananchi na kuwa karibu zaidi na wananchi bila kutumuia middlemen.
  Haya ni baadhi ya mazuri yake.

  Jambo baya zaidi kwa Amin lilikuwa ni kutokuwa na uongozi wa sheria, yaani akikuhisi kuwa upo against nae basi hukumu yako ni risasi. Hali hii ilifanya wasaidizi wake kuishi kwa mashaka makubwa na kujipendekeza zaidi.

  Je sera hizi za Amin ukiacha ya kuchukua sheria mkononi ingeweza kuifikisha Uganda mbali kimaendeleo kama siyo kung'olewa mwaka 1979 na majeshi ya Tanzania? katika vita ya Kagera?

  Msikilize Idi Amin Dada Halisi kwenye link hii na uamue mwenyewe

  Documentary – “People must love their Leader!” – Portrait of Gen. Idi Amin Dada
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nimeangalia sana documentary ya Idi Amin, kimsingi inaonekana kuwa hakuwa na sera yoyote ya kuendeleza nchi zaidi ya kuiangamiza. Utawala wake uliiyumbisha Uganda kwa kiasi kikubwa, na wanawake aliokuwa akiwapa madaraka wengi walikuwa ni vimada wake na sio kama alikuwa akifanya hivyo kwa sababu ya kuona umuhimu wao. Mpaka sasa sijaona kama kuna lolote ambalo mganda anaweza kujivunia kutokana na utawala wa Idi Amin, labda utupe mifano zaidi. Sijui kama kukifanya kiswahili kiwe lugha ya Black Americans ilikuwa idea nzuri na sijui maana yake ilikuwa nini. Yeye mwenyewe alikuwa anajifunza kiingereza kwa nguvu lakini hakufundisha kiswahili nchini mwake.
   
 3. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Alijenga Uganda house (inatumiwa kama ubalozi na maofisi) on +ve side hii.
   
 4. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  a very sad chapter in the annals of african history.he must have gone straight to hell
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nilichosema si kumtetea au kumpa credit Idi Amin, nilitaka uangalie film yake huenda unaweza kugundua kuwa huyu jamaa pamoja na mabaya yake pia alikuwa na mtazamo wa kizalendo, japo elimu duni aliyokuwa nayo na kukosa utawala wa sheria vilikuwa na impact kubwa katika kuiendeleza Uganda.
   
 6. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkulu Hofstede,

  Heshima mbele.

  Nataka kukuaambia kwamba hapa,ukizungumzia maswala ya methods/ways zinazoletea out comes watu hawata kuelewa hapa rather zungumzia OUT COMES.
  Mim i ni mmoja wa wale wanadhani Amin alikua na mipango mizuri zaidi ila elimu ndio kitu kikubwa kilicho mwangusha(hakujua jinsi ya ku-tackle matatizo ili kufikia kwenye malengo ambayo alijiwekea,na hii inatokana na watu walio chini yake hawakua willing )

  Sikuzote maendeleo au imput inatokana na IDEA,ukiweza kuendeleza idea basi ni lazima upate output,hapo ndipo utajua hiyo output ni nzuri au mabya.Amin kama ulivyo outline kwenye post yako ya kwanza alikua na malengo(ingawa itasemeka ni Mipango hewa) na ilihitaji wasaidizi wazuri ambao wangekua wakifanya kazi vizuri out of fear of Amin ,i am lead to believe jamaa (Uganda) wangeendelea kutuzidi
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nadhani la uzalendo siwezi kupingana na wewe, hata waganda niliowahi kuzungumza nao wanasema kama jamaa angekuwa amesoma na angekuwa na akili basi Uganda ingepiga hatua kubwa sana. He was a really nationalist, na kati ya wenyekiti wa OAU waliofanya vizuri, Amin alikuwa one of the best.
   
 8. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Shukrani sana kwa clip hii haya huyu jamaa. Aisee inadhihirisha kabisa jamaa alikuwa kichwa maji mno. Alikuwa na baadhi ya idea ambazo on a positive spectrum zingeweza kuleta mantiki lakini duh kweli alikuwa na bahati ya mtende kuotea jangwani. Ilikuwajekuwaje hadi akafikia alipofikia????
  Nimecheka sana telegram ya kwenda Nyerere.......Kumbe mzee kifimbo alitaka kuposwa sio......Kali.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanzange.
  ebu iweke hiyo telegram ya Idd Amin tucheke vizuri
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Huu ni mfano mzuri.It is a landmark...to remember him by!
  Uganda kwa hili wanapata sifa sana maana licha ya kuwa na uhakika wa ofisi ya ubalozi pia wanapata kipato cha uhakika kwa kupangisha ofisi kwa wengine...tena kwenye eneo la maana ...karibu na makao makuu ya UN New York. Je serikali yetu ingekuwa na viongozi wenye kujali maslahi ya nchi tungeshindwa nini kuwa na majengo kama haya? Tulipotaka kununua jengo huko Roma Italia...pesa iliishia kwenye ufisadi na kuneemesha wale tuliowaamini!Shame on our leaders!
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unasema Rais wa Uganda alikuwa na ndoto ya kuwafanya raia wa nchi nyingine, African Americans, wabadili lugha wanayotumia! Ha ha aaaa! Siwezi kujizuia, Hofstede, hicho kitu yani kinachekesha.

  Katika hiyo clip Iddi Amini mwenyewe anaongea Kiingereza kwenye cabinet meeting na public speeches!
  Kwenye hii documentary kwenye kikao cha baraza la mawaziri Amin anasema “tuwahimize wanawake waamke saa kumi na moja alfajiri wakachume mboga na kuuza magenge”!!!

  Hofstede, kwa taarifa tu, mwanamke sehemu yake sio kuhudumia familia! Hiyo ni dhana ya zama za mawe, na za giza (dark ages ) na karne iliyopita ya ma bigot kwa kijinsia.

  Iddi Amini amefungua kikao cha baraza la mawaziri (wanaume watupu ) kwa maneno haya:

  "All of you are in very high ranking governmental positions. Your duty is not to be very weak. You must not be like a woman who is just very weak and can not speak even talk..."

  “...You must not make the womens of Uganda very weak, they must get up quickly in the morning at about 5 o'clock, they are prepared and ready to sell vegetables and everything in the shop...

  You must tell our women that I said that the duty of the woman is house woman. She knows how to keep house very well the duty of the woman is housewoman. If she can do that let me make first examination: appoint women to be managers of hotels, which is done. Because this is part of the women's job. If they can keep house very well it is exactly like their duty as housewife. If she is well educated, she’s got that brain, she is determined, she can look after the hotel very well…

  I think we are the first now country in Africa today who have got many women managers than other countries. We’ve got how many ? Manager woman ?
  (Mawaziri wakamjibu “wanne”!) Akaendelea: We’ve got four managers and we’ve 2 assistant managers…

  Iddi Amini anasema alikuwa mstari wa mbele kuteua mameneja hoteli wa kike, aliongoza Africa nzima, alikuwa nao wanne! Haha haaa aaa...Such a comic!

  Hofstede, mtu anaeiambia cabinet yake “msiwe dhaifu kama wanawake,” aneamini mwamke kazi yake ni kukaa mkao wa kuchuma mboga na kuuza genge ni bigot wa kijinsia!

  Sikiliza tena kile kikao cha baraza la mawaziri, mkutano mzima alikuwa anatoa maagizo kwa mawaziri nini cha kwenda kuwaambia ma bureaucrats wao. Kawa karibu na wananchi kwa vipi, kwa sababu yeye mwenyewe ndio kasema hivyo ? Kuwa karibu na wananchi kwa ku show up kwenye vi shamrashamra vya kupiga zeze ? Na kutoa speeches kuhusiana na boxing career yake ? Let’s not praise this buffoonery ya “kuwa karibu zaidi na wananchi.”

  Sera zipi hizo, za wanawake waamke mapema kuchuma mboga na kuuza magenge ?
   
 12. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeiona humohumo kwenye clip.......somehwere katikati...
   
 13. F

  Foti Mwarobaini Member

  #13
  Dec 6, 2008
  Joined: Jan 1, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la uongozi mbovu kwa ujumla unatufanya kuona kuwa Amin alikuwa kiongozi mzuri. Angekuwa ametupa jamaa zetu mtoni kuliwa na mamba sijui kama hoja hii ingejitokeza.
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kukutana na Mganda akamponda Iddi Amin wote wanamsifia as a hero.
   
 15. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama sie tunavyomsifu Marehemu Nyerere!!!!!!
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  you are now becoming old....! guy ugandans blame and throw stones at him....!
  kumbuka waakati wa mazishi yake how many walishiriki halafu ndo umfananishe na MZEE WA MSASANI...?
  amin kama alipendwa na waganda why alienda ishi EXILE...?
   
 17. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wadhani, kina McGhee wangefanikiwa kumpindua JKN, asingelala mbele????

  Any way hata mimi natia shaka kama waganda wengi walimpenda Amini. Yawezekana ni idadi kubwa ya waganda ila si wengi kwa kulinganisha na waliomchukia!!!!!!
   
 18. N

  Nsunza Member

  #18
  Dec 7, 2008
  Joined: Jan 21, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unayo sema ni kweli. Swali ni hili, tunamiliki jengo la ubalozi wetu Marekani "DC"? Kama hatumiliki, kwa nini tusi nunue maana bei imeshuka karibu kwa asilimia hamsini? Ooooh! Nmesahau viongozi wetu hawajui kinachoendelea duniani.
   
 19. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2008
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Instead wanamponda Milton Obote...(that's another topic hapa JF)

  Hero? wow!!! the rest of the world does not think so, though...who all watched the "Last King of Scotland" if it's anything to go by, "Raid on Entebbe" Or even "The Rise and fall of Iddi Amin"...i know these are just movies but? that is how the world has been "told or compelled"(sp) to remember him!!

  Every time one says Africa, the ones(Western world) who think they are enlightened think Idi Amin and they procede to start talking in their myopic ways and display all their ignorant ideas about Africa.

  They always wanna talk about is Iddi Amin.
  I'm sure he must have had some good qualities like every one else, the only question is what were they?

  I know the West has never potrayed anything from Africa as good or reasonable OR positive(apart from HIV, pun intended)
  I can't say i know much about Iddi Amin but was there any good that he did?
  Can someone enlighten me? as I do not have any well argued time tested facts.
  Please wana JF?!! I know there are members who know alot abot EA politics and history.
   
 20. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Alijenga ukumbi mkubwa was mikutano ambao unatumika hivi sasa huko Uganda.
  Ila huyu jamaa aliponifurahisha ni alipompa Maliyamungu Lake Victoria kama birthday present yake!
   
Loading...