Identity theft unavyotesa watumiaji wa tigo pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Identity theft unavyotesa watumiaji wa tigo pesa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mirindimo, Apr 26, 2012.

 1. mirindimo

  mirindimo JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  Niliingia katika hiki kibanda ili nitoe pesa yangu katika account ya tigo pesa ndipo dada anaehudumia akaniambia hawezi nihudumia sababu anawaza kufungwa kwa wizi uliotokea kwani hana namna anaweza kulipa hizo laki 9...ilikua hivi ; huyu dada alitumiwa msg na namba ya boss wake kua atume laki 7 kutoka laini ya tigo pesa na laki 2 kutoka m pesa,alifanya kama message ilivyosema baadae kidogo akatakiwa kutuma tena laki nane kutoka tigo pesa ndipo akashtuka kumpigia boss wake na kumuuliza kama kweli anataka pesa hiyo itumwe boss wake akabaki anamshangaa unatuma pesa zipi na wapi ndipo akashtuka kua ameibiwa kiasi cha jumla ya Tsh 900,000 hapa kimara mwisho jioni hii.Hili ni tatizo kubwa sana na linawakuta ma agent wengi na kuishia kuumiza wafanya kazi wanaowalipa elfu 70 mpaka laki....naomba mitandao husika washughulikie tatizo hili na watoe ufumbuzi kwani haiwezekani mtu kuiba identity (namba ya simu) ya mtu mwingine bila kushirikisha watu walioko kwenye system , hili mimi haliniingii akilini kama laweza fanywa na mtu asiejua a b c za system ya tigo! Na hili linafanya ma agent wengi wakatae kutoa huduma hii na si kwa ma agent tu hata watumiaji wa kawaida tumekua tukiibiwa pesa kiajabu ajabu tu mimi pia niliibiwa na nikafuatilia namba hii 0713251725 niliyopewa cust care kua ndio imetumiwa pesa bila mafanikio, tafadhalini sana tigo,chonde chonde tunatafuta hii pesa kwa taabu mno! Nawasilisha jamani aliesoma alifikishe kwa wahusika
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi sijui hii kampuni ya TIGO inaendeshwa kwa kutumia sheria za nchi gani kwani kwani hata namba zao zinauzwa kama njugu mtaani na watu hawazisajili na zipo hewani zinafanya uhalifu kama kawaida.
   
 3. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145

  Halafu wakiambiwa kazi zimewashinda wajiuzulu wanalialia....
   
Loading...