Iddi Amini Dada

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
c5148a3709840b76dbd6e6ce42e50835.jpg


HUYU NDIE “FIELD MARSHAL ALHAJI DR, IDI AMIN NDUL DADA” RAIS WA TATU WA UGANDA AMBAYE UTAWALA WAKE UMEGUBIKWA NA UTATA.

Na, Comred Mbwana Allyamtu.
Sunday -29/10/2017.

Idi Amini alichukua madalaka kutoka kwa Obote, huyu Militon Obote ndiye alie anzisha vuguvugu la ukombozi nchini Uganda, Milton Obote alikuwa mtu wa Kabila la Walang'o kutoka kaskazini mwa Uganda, na alikuwa akipinga madai ya Baganda kuwa na haki za kuchukuwa madaraka na pia urithi wa zama za ukoloni. Kupitia muungano wa chama chake cha Uganda People's Congress (UPC) uliokuwa na wanachama kutoka nchini kote, alifanikiwa kushinda wingi wa kura bungeni na kufanikiwa kuunda serikali ya kwanza kabisa mwaka 1962 na kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Uganda na Kabaka Mutesa kuwa Rais wa kwanza wa Uganda asie na mamlaka makubwa.

Obote na Amini walikuwa watu wa kalibu sana katika urafiki wao na ni Obote aliyemuingiza Amini kwenye ngazi za juu za jeshi yamkini Obote ndie aliyempandisha Amini kwenye duru za kitaifa ni kipindi Obote alipokuwa na mkakati wake wa kumuondosha Rais Kabaka madalakani alimtumia Amini kumpindua Kabaka na baadae kumzawadia cheo cha ukuu wa majeshi kwa mantiki ya kudhibiti watu wa upande wa Mutesa na wafuasi wa kabila la Baganda.

Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada mbabe wa Afrika mashaliki wa miaka ya 1970 Amini ni mtu kutoka kabila la Wakakwa japo zipo duru zingine udai alikuwa mtu wa kabila la Lango, jambo linalopingwa na mwanae Hussen Amin Lumumba, katika historia yake kuanzia kuzaliwa mpaka utawala wake uligubikwa na utata sana.

Alhaji Dr. Idi Amin Dada alikuwa rais wa tatu wa Uganda alianza utawala wa taifa hilo kuanzia tarehe 25 Januari 1971 mpaka tarehe 11 Aprili 1979. Miaka tisa baadae katika utawala wa Amini kume kuwepo na utata mwingi juu hali ya mambo ndani ya utawala wake, wako wanaedai kuwa utawala wake ulikuwa ni wa kinyama na ulikithili katika mauaji ya watu waliotajwa kuto kumuunga mkono.

Lakini pia upande mwingine utazama utawala wake kama zama mpya za Uganda ambapo nchi ilipata mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mtazamo huu ndio watu umtazama Amini kama mwanamageuzi na mwafika aliyetaka kuijenga nchi yake kujitegemea ambapo alilijenga jeshi imara na kuhodhi mali zilizokuwa zikimilikiwa na mabepali na kuziludisha mikononi mwa waganda. Je kama dhana hii ni kweli je dhana ya mwazo ya kuwa amini hutazamwa kama mnyama asiyekuwa na huruma na mla nyama za watu inatoka wapi?

FIELD MARSHAL ALHAJI DR IDI AMIN NDUL DADA NI NANI?

Idi Amin Dada (alizaliwa 1923–28 – na kufaliki 16 Agosti 2003) alikuwa mwanasiasa na afisa wa jeshi ambaye alikuwa Rais wa wa tatu wa Uganda kuanzia 1971 hadi 1979. Baadhi ya wachumbuzi wanadai kuwa Alitawala kidikteta huku uchumi wa nchi uliporomoka na makosa mengi ya jinai dhidi ya haki za kibinadamu yalitendwa.

Wachambuzi hao husema kuwa Idadi ya watu waliouawa Uganda kutokana na utawala wake imekadiriwa kuwa kati ya 100,000 na 500,000. Katika miaka yake ya kushika serikali lakini kuna wachumbuzi hupingana na hilo huku wakiitupia lawama tawala za magharibi kwa kupika maneno juu ya Amini.

Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi na hasa Israeli kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki. Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake kipindi ambacho Amini alikuwa akiimalisha Jeshi lake.

Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza kisha akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE ("Conqueror of the British Empire"). Kuanzia wakati ule cheo chake rasmi kilikuwa ni "His Excellency President for Life, Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE". Jaribio la Amin la kutwaa sehemu za Mkoa wa Kagera wa Tanzania kwenye mwaka 1978 lilisababisha Vita ya Kagera baina ya Tanzania na Uganda na mwisho wa utawala wake. Vita hii baadhi ya wachambuzi huitazama kama mkakati wa mataifa ya Marekani na Uingereza wa kumuondosha madalakani Amini ndipo walipoamua kumtumia Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania wakati huu kwa kuita “Vita ya uchochezi” baada ya vita ile Amin alikimbia kukaa ugenini Libya na baadaye Saudia alipoishi hadi kifo chake mwaka 2003.
a791a2e3711fbc4a3578fc99b1602e6b.jpg


HISTORIA YA MAISHA YAKE

Hakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1925 Koboko au Kampala. Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928, lakini hii imepingwa. Mwanawe Amin Hussein alisema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928.

Kufuatana na Fred Guweddeko wa Chuo Kikuu cha Makerere Idi Amin alikuwa mwana wa Andreas Nyabire (1889–1976) wa kabila la Wakakwa, ambaye alikuwa Mkatoliki aliyehamia Uislamu mnamo 1910 akibadilisha jina lake kuwa Amin Dada na kumpa mwana wa kwanza jina hilo pia.

Iddi Amin alilelewa na mama yake bila baba kijijini katika Uganda ya Kaskazini-magharibi. Kufuatana na mtafiti Gudewekko mamake Amin Assa Aatte (1904–1970) alikuwa Mlugbara aliyetibu watu kwa mitishamba (mganga wa kienyeji). Hata hivyo Amin alisoma miaka kadhaa kwenye shule ya Kiislamu huko Bombo kuanzia mwaka 1941 mpaka mwaka 1946 alipoamua kujiunga na jeshi nah ii ilitokana hali ngumu ya maisha ya familia yake hasa mama yake aliyemlea.

KUJIUNGA NA JESHI 1946

Baada ya miaka michache ya shule na kazi ndogondogo aliajiriwa mwaka 1946 na afisa Mwingereza wa jeshi la kikoloni King's African Rifles (KAR). Aliingia jeshini huko katika mji wa Jinja akifanya kazi ya msaidizi jikoni akiendelea kupokea mafunzo ya kijeshi. Baadaye Amin alidai ya kwamba alilazimishwa kuhudumia huko Burma katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwaka 1947 alihamishiwa Gilgil, Kenya. Mwaka 1949 alitumwa kaskazini kwa kupigania waasi Wasomalia huko. Tangu mwaka 1952 kikosi chake kilihudhuria katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa Maumau karibu na Mlima Kenya.

Aliendela kupanda vyeo vilivyopatikana kwa Waafrika katika jeshi la KAR na muda mfupi baada ya uhuru alipewa cheo cha luteni yaani afisa kamili kama mmoja wa Wauganda wawili. Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 alikuwa kapteni halafu mwaka 1963 meja. Kisha Mwaka 1964 alikuwa makamu wa mkuu wa jeshi la Uganda na mwaka 1965 mkuu wa jeshi kamili, mwaka 1970 mkuu wa kijeshi NA KAMANDA MKUU. In 1970, he was promoted to commander of all the armed forces.

IDD AMINI JINSI ALIVYOPANDA VYEO JESHINI

Alijiunga na jeshi la kikoloni la King's African Rifles Mwaka 1946 baada ya kujiunga na jeshi hilo la King's African Rifles mwaka huo ndipo mwaka 1947 akawa Askari wa kawaida Mpaka mwaka 1952 alipanda na kuwa Koplo kisha mwaka 1953 akapanda na kuwa Sajenti Lakini mwaka 1958 alipanda tena na kuwa Sajenti mtumishi Kutokana na utumishi wake wa ukakamavu na kujituma alipanda tena mwaka 1959 na kuteuliwa kuwa asikali mwenye cheo cha “Effendi” (afisa mteule).

Ilipo fika mwaka 1961 alipanda cheo cha Luteni (mmoja kati ya Wauganda wawili waliofikia cheo hiki katika KAR) ndani ya Jeshi la Uganda Ilipofika mwaka 1962 alipanda mpaka kufikia cheo cha Kapteni Utendaji wake ulimfanya afike mbali ndipo alipanda na kufikia ngazi ya juu ilipofika mwaka 1963 alifikia ngazi ya Meja.

Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 aliendelea kupanda ngazi na kufikia ngazi ya juu kabisa na hii ilikuwa bahati kwake ndipo mwaka 1964 aliteuliwa na Obote kuwa Makamu wa Mkuu wa Jeshi la Uganda
Mpaka mwaka 1965 alipopanda na kuwa Kanali, Mkuu wa Jeshi na ilipofika mwaka 1968 ilipanda ngazimpaka kufikia cheo cha Meja Jenerali mpaka mwaka 1971 alipokuwa Mkuu wa dola baada ya kufanya mapinduzi yaliyomuondoa madalakani Ndugu Milton Obote.

Baada ya mapinduzi alijiteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wa Dola na Amiri Jeshi Mkuu wa Uganda na hivyo mwaka 1975 ilijipa cheo cha Field Marshal ambacho alidumu nacho mpaka alipopinduliwa mwaka 1978.

IDD AMIN MKUU WA JESHI NA KUONGOZA MAPINDUZI MWAKA 1970

Amin alipandishwa cheo na waziri mkuu Milton Obote baada ya uasi wa wanajeshi katika Afrika ya Mashariki wa 1964 uliokomeshwa na askari Waingereza katika Tanganyika, Kenya na Uganda akawa makamu wa mkuu wa Jeshi huku mkuu wa jeshi alikuwa bado Mwingereza. Kutoka hapa alishirikiana na Obote katika hatua za kuimarisha utawala wa waziri mkuu. Wakati bunge la Uganda lilitaka utafiti kuhusu mashtaka ya Obote kushiriki katika biashara ya siri ya pembe za ndovu kutoka Kongo Obote iliamua kubadilisha katiba na jeshi la Amini lilimfukuza Mkuu wa Dola Kabaka Mutesa kwa nguvu, halafu Obote alijitangaza kuwa rais. Sasa Amin alikuwa kanali na Mkuu wa Jeshi.

Amin alianza kuajiri hasa askari kutoka kaskazini ya Uganda mpakani mwa Sudani bila Obote kujua kumbe masikini hii ilikuwa ni njia ya kujiimalisha kwa Amini katika jeshi. Mwaka 1970 Obote aliendelea kumpa Amin cheo cha mkuu wa jeshi na ulinzi. Lakini Amin alisikia pia ya kwamba kulikuwa na mashtaka dhidi yake kutokana na matumizi mabaya ya makisio ya jeshi na mipango ya Obote kumfanyia uchunguzi. Hapo Amin ndipo alitumia nafasi ya safari ya Obote kwenda nje kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, kufanya mapinduzi na akatwaa mamlaka ya serikali tarehe 25 Januari 1971.

AMINI NA UTAWALA WAKE UGANDA

Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka. Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake(taalifa hizi hupingwa na baadhi ya wachambuzi wengine)

Wale wachambuzi wanaoulaumu utawala wa Amini hudai kuwa Amin Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani na Kanada.

Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979. Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia na siasa tena. Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003. Na hii ndio ikawa mwisho wa Idi Amin Dada.

Wako Mjoli wa Historia ya dunia na mambo ya dipromasia ya dunia......

ae9c1d00168e8cccb3ce2e699c510608.jpg
.
 
shukrani sana comrade ukipata nafasi utupatie na ya yule bwana COLONEL ISSAAC MALIYAMUNGU historia yake na alipo sasa kama bado yupo mana sisi wengine vijana sana hatuyajui hayo ...nawasilisha
 
Yatapita hizo shida za kunywa maji ya kandolo mbadala wa kilimanjaro ipo siku yatapitaaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom