Idd ninga=MLIMA UNALIPUKA[shairi.

Idd ninga=MLIMA UNALIPUKA[shairi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
sote twendeni sanjari,kwa nguvu pia na hari.
Tuvisahau viburi,tuifanye kwa hiyari.
Tena tukiwa tayari,kama vile tu mandari.
Kwa nguvu ka majabari,tuupande kihodari.
Kwa miguu ama gari,tuukwee na tairi
MLIMA UNALIPUKA,TWENDE SOTE TUKAZIME.
mtunzi=idd ninga wa tengeru arusha.
0655519736
 
Mlima kusema kweli, ni mama yetu wa asili
Hututunza kwa mengi,maji mvua na hewa
Kama mama anaungua, hima tuondoe hii balaa
Tutateketea bila kujua, haraka tuzuie ukiwa
Mlima sote twajua, ni mama yetu wa asili.

Aisee Idd Ninga, hii mistari koko mitano imenitoa jasho lita mbili!
Ni zoezi zuri kwangu hivyo endelea kunipa changamoto
 
Last edited by a moderator:
hakika wajitahidi,kukusifu sina budi.
yakuwa yako juhudi,sana yanipa midadi.

shairi weza andika,kalamu utaposhika.
beti nyingi kwa hakika,utakuja ziandika
SHIEKA
 
Last edited by a moderator:
Mlima kusema kweli, ni mama yetu wa asili
Hututunza kwa mengi,maji mvua na hewa
Kama mama anaungua, hima tuondoe hii balaa
Tutateketea bila kujua, haraka tuzuie ukiwa
Mlima sote twajua, ni mama yetu wa asili.

Aisee Idd Ninga, hii mistari koko mitano imenitoa jasho lita mbili!
Ni zoezi zuri kwangu hivyo endelea kunipa changamoto

wasema ule mlima, tena ni wenye kuwaka
mlima leta neema, asili iso mashaka
alikuja mkulima, mjuvi alo miaka
mlima akauchoma, viumbe nakakadhalika

Eti maslahi ya umma, mlima kuteketea
ni IPI ilo hekima, busara Inge ngojea
kwanini awe halima, wengine hawajatokea?
mhimili uwe vema, vizuri kujitegemea

hupigwa ulio mwema, lakini Si jitakia
tukumbuke zile zama, hivi ndo katuhusia?
nani asiye na mama? na manju kampatia
nimefika kaditama, tutaona na jalia
 
Last edited by a moderator:
hausikii kishindo,kikubwa kunalipuka.
kikali kuliko nyundo,nalo jivu linaruka.
na moto upo marundo,sauti inasikika.
miale ipo mafundo,itachoma ikiwaka.
nani wakulinda lindo,na mlima una waka ?
Ilongailunga
 
Kikali kuliko nyundo, chachongwa tena maumbo
kwanini yawe mafundo, kumiza yetu matumbo
basi tulitie pindo, tubomoe chetu chombo
hadidhi ya bwana tindo, Leo nakupa matambo

hakufwata zake nyendo, mkongwe mwenye kifimbo
kusuka pekee kindo, ukiri USO mayombo
hata yule mweka kando, hajui hana hujambo?
risala iso na mwendo, mechoka tena kitambo
 
Wee mrangi najua Madrsa inakubeba sana.
 
Last edited by a moderator:
Kikali kuliko nyundo, chachongwa tena maumbo
kwanini yawe mafundo, kumiza yetu matumbo
basi tulitie pindo, tubomoe chetu chombo
hadidhi ya bwana tindo, Leo nakupa matambo

hakufwata zake nyendo, mkongwe mwenye kifimbo
kusuka pekee kindo, ukiri USO mayombo
hata yule mweka kando, hajui hana hujambo?
risala iso na mwendo, mechoka tena kitambo

Mkuu. Nawapenda sana washairi. Sijui kutunga lakini ninaposoma huwa najisikia raha sana..
Ila ninachokiona ili uwe mshairi basi meneno mengi ya kiswahili uyajue.
Hongereni sana pamoja na mleta uzi.
 
yeye aliwasha moto,mlimani kwenye pango.
akayapata mazito,kwa yeye kupinga hongo.
vyote hivi ni vitoto,alievilisha pongo.
hawajui ni mazito,wai wafanya maringo
mlima kweli wawaka,alowasha twamjua.
Ilongailunga
 
Last edited by a moderator:
SaaMbovu kweli misemo ya kiswahili inaweza fanya wakati mwingine kupata shida wakati wa uandishi.
karibu sana tutunge,mashairi tuandike.
kiswahili tukilonge,mpaka mbali kisifike.
nyingi tungo tuzitunge,misemo ikusanyike.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu. Nawapenda sana washairi. Sijui kutunga lakini ninaposoma huwa najisikia raha sana..
Ila ninachokiona ili uwe mshairi basi meneno mengi ya kiswahili uyajue.
Hongereni sana pamoja na mleta uzi.

Ushairi huu fani, muhimu ni maudhui
shairi pia mizani, vina nakama hujui
misemo ni mathalani, utunzi nia sifai
tungo zenyewe matini, jaribu kwa kujidai
 
alaaaaaa,balaaaa
tungo zenyewe kwa fungo,alonaswa na urimbo.
tuvifungue vifungo,tulofungwa tangu tambo .
tena tuiteme nyongo,kwa sifa pia matambo.
na kilima kizimike,alowasha tumshike.
Ilongailunga
 
Last edited by a moderator:
alaaaaaa,balaaaa
tungo zenyewe kwa fungo,alonaswa na urimbo.
tuvifungue vifungo,tulofungwa tangu tambo .
tena tuiteme nyongo,kwa sifa pia matambo.
na kilima kizimike,alowasha tumshike.
Ilongailunga

Kayi hai aye...tengeru tuku hahaaa
 
Last edited by a moderator:
alaaaaaa,balaaaa
tungo zenyewe kwa fungo,alonaswa na urimbo.
tuvifungue vifungo,tulofungwa tangu tambo .
tena tuiteme nyongo,kwa sifa pia matambo.
na kilima kizimike,alowasha tumshike.
Ilongailunga

mweledi mshinda uga, sikia hii habari
uwache nao uoga, kilele ukitayari
usipande na maboga, usije tiwa shubiri
saambovu alo kiga, jamani hana hiari.
 
Last edited by a moderator:
mweledi mshinda uga, sikia hii habari
uwache nao uoga, kilele ukitayari
usipande na maboga, usije tiwa shubiri
saambovu alo kiga, jamani hana hiari.

naona wingu latanda,laufunika mlima.
buibui ametanda,basi tusimame hima.
sote tuache vitanda,twende kukwe kilima.
kilima ni kichuguu,kumbikumbi wanaruka.
haooooooooooooooooo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom