Shairi; Tushaanza kutishana.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
TUSHAANZA KUTISHANA.

1)Ile ni siku ya kwanza,tulidhani yamepita.
Kumbe mwanzo yalianza,bunduki kwenye utata.
Kwa lipi tunajifunza,ama mapito twapita.
Tushaanza kutishana,katika kisiwa hiki.

2)mitupu yake mikono,vipi umtishe panga.
Ubabe na malumbano,bora ungetia nanga.
Ufe wetu muungano,ama mmeshalipanga.
Tushaanza kutishana,katika kisiwa hiki.

3)Wazi wazi hadharani,dharau waikataa.
Kwa kuipiga hewani,katikati ya mtaa.
Mchana barabarani,umma ukikushangaa.
Tushaanza kutishana,katika kisiwa hiki.

4)Hao nao maarufu,vipi wale masikini.
Tena waso na wasifu,na majina mitaani.
Siyo zama za awafu,tujenge yetu imani.
Tushaanza kutishana,katika kisiwa hiki.

5)Heshima ikitoweka,nguvu zote hupotea.
Likizuka patashika,hakuna wakukimbia.
Ni bora kuheshimika,nidhamu kujijengea.
Tumeanza kutishana,katika kisiwa hiki.

Shairi-TUSHAANZA KUTISHANA
Mtunzi-Idd Ninga wa Tengeru arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
[HASHTAG]#mimimalenga[/HASHTAG]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom