Idd ninga=SIMBA ATAMLA SIMBA (shairi)

Idd ninga=SIMBA ATAMLA SIMBA (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
IFUATAYO NI SEHEMU NYINGINE YA SHAIRI LILOANDIKWA NA IDD NINGA.
INGAWA MAUDHUI YA SHAIRI HILI YAMEJIFICHA LAKINI NI MARAHISI KUYAELEWA

1>ni majanga na balaa,nyoka anajibabua.
Kwa ndugu na majamaa,ngozi yeye ajivua.
Alozika ujamaa,dhambi anaijutia.
Simba atamla simba,nyumbu aliwa na mbugo.
2>machoni wamezubaa,mende atawazibua.
Itatumika sanaa,uongo kuufumua.
Msuko wa kitambaa,wenye ladha ya halua.
Simba atamla simba,nyumbu aliwa na mbugo.
3>panzi wanawahadaa,kwa kasi wanapumua.
Machoni wamezubaa,wamepakwa ndimu mua.
Wamemezeshwa miraa,bila kusoma barua.
Simba atamla simba,nyumbu aliwa na mbugo.
Shairi=SIMBA ATAMLA SIMBA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 au 0655519736
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom