Idara ya ujenzi zaondolewa toka halmashauri

Idara ya ujenzi zaondolewa toka halmashauri

TARURA = TAnzania Rural and Urban Roads Authority

Barabara zilizokuwa chini ya Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa/Majiji ndizo zinazohusika

Kwani wataalamu wa ujenzi manispaa walihusika na barabara pekee??
 
Imeanzishwa Agency mpya kwa ajili ya kushughulikia barabara la Halmashauri na Vijijini inaitwa TARURA ili kuongeza ufanisi

Tuseme sawa. Japo siamini hili

Je wajenzi wote katika halmashauri ni wa barabara tu???

Vipi kuhusu ujenzi mwingine???
 
Kwani wataalamu wa ujenzi manispaa walihusika na barabara pekee??
Kulikuwa na idara ya Barabara, Majengo nadhani na Maji na umwagiliaji hivyo wale wa idara ya barabara ndio wanakwenda TARURA

Ujenzi ilipoboreshwa ilizaa TANROADS, TBA na TEMESA sasa huenda baada ya TARURA idara ya ujenzi ikaenda TBA na idara ya maji ikaenda wizara ya maji.

Huu mchanganyiko ndio iluotokea pia kati ya CDA na wizara ya ardhi kuhusu upimaji ardhi na hati za kumiliki ardhi
 
Hapo kidogo umeelezea sawia ila bado kuna mkwamo UNLESS uniambie ni idara ya barabara pekee ndio inayovunjwa na sio ujenzi.

Idara za maji zipo zinajitegemea sio wizarani. Mjini kuna mamlaka DAWASA,AUWASA DUWASA nk ila vijijini bado kuna idara nyingi za maji zinajitegemea

Hawa watu wengine wa ujenzi pengine kama unavyosema waende TBA ila itakua ni kurudisha urasimu ule ule na kupingana na ugatuaji madaraka
 
Back
Top Bottom