Idara ya Afya TAMISEMI iwe na ushirikiano na Wizara ya Afya

JembeNaNyundo

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
532
646
Miezi michache iliyopita NHIF kwa kushirikiana na Maxcom walianzisha mradi wa majaribio ya utunzaji wa kumbukumbu za hospitali (HMIS) na hospitali chache zilichaguliwa kwa majaribio. Mfumo huu watumika na hospitali mashuhuri nchi India. Mfumo huu utawezesha hospitali kuwa katika mfumo wa paperless na hivyo kuokoa pesa nyingi, na wakati huohuo hakutakuwepo ujazaji wa karatasi za bima ya afya, na hii itapunguza gharama kwa hospitali na NHIF na hata kuharakisha malipo toka NHIF.

Ingawa sera ya sasa ya serikali ni kuwafanya watanzania wote kuwa na bima za afya, hususani NHIF yalikuwa ni mategemeo ya watu wengi kwamba hospitali za Rufaa, mkoa na wilaya zitajiandaa kuupokea mfumo huu ulioletwa na NHIF kwa kuwa NHIF ni mteja mkubwa. Jambo la kushangaza, wiki moja iliyopita TAMISEMI ilikusanya Mzumbe, Morogoro waganga wakuu wa mikoa, waganga wafawidhi wa hospitali za mikoa, makatibu afya wa hospitali za mikoa na watu wengine ili kuwafundisha mfumo mpya wa utunzaji kumbukumbu ambao utakuwa ukitumika na hospitali za mikoa na wilaya. Mfumo huu murkiest ukitumiwa na hospitali ya Tumbi, na umetengenezwa kwa ushirikiano na chuo Kiki cha Mzumbe Morogoro. Mafunzo haya yalitumia siku nne.

Ingawa ni jambo jema, Lakini kumekuwa na tabia za taasisi za serikali kujiingiza gharama kubwa kwa kufanya kazi aina moja. Hospitali hizi za TAMISEMI zinaihitaji NHIF, na hivyo ni lazima watahitaji kutumia mfumo unaoletwa na NHIF ambao ni bora zaidi ya ule wa Tumbi, na unafanya kazi nyingi zaidi na pia una uwezo mkubwa wa kuintergrate vitu vingine.

Lakini pia hospitali za TAMISEMI zinatumia mifumo ya maabara ya Labnet wakati Wizara ya Afya ina mfumo mzuri wa Dyser. Sasa haya yote yanatufanya tuwe na mifumo tofauti na kujiingiza gharama nyingi.

Taasisi za serikali ziwe zafanya mawasiliano zinapotaka kufanya kazi Fulani zinazoingiliana.
 
Back
Top Bottom