Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,412
Mpo salama!
0. Wakati baadhi ya vijana kama kina Lucas wakijiingiza kwenye uchawa kwa sababu ya Woga na tabia za kujidhalilisha. Wanawake wengi sasa wanajiingiza kwenye mapigano ya haki(harakati)
Ama kweli lile andiko linasolema Mungu ameumba jambo jipya. Mwanamke atamlinda mwanaume linaenda kutimia.
1. Kikawaida wanawake wanahulka ya woga.
Na ukiona mwanamke woga unaanza kumtoka, na ujasiri unamvaa ujue mambo zamefika shingoni.
2. Nataka nikuhakikisha kuwa wanawake hawana akili kuwazidi wanaume ila linapokuja swala la hila na uovu mwanamke kamuacha mbali sana mwanaume kwa akili ya hila.
Yaani kwenye hila shetani mwenyewe anasubiri kwa mwanamke.
3. Niliwahi kueleza hapa pia, mwanamke anajua perfect time kufanya shambulio. Yaani wakati sahihi wa kutekeleza hila yake. Ndio maana wanawake wengi kwenye kuangusha maadui zao hufanikiwa kirahisi tofauti na sisi wanaume.
4. Elewa mwanamke hanaga kitu kinaitwa msamaha. Yaani ukishamuona ameingia kwenye game, ring, pambano basi ujue hakunaga kitu anatambua kama msamaha.
5. Elewa wanawake kisaikolojia anapokuchukia ili akusamehe lazima akulipe kwanza na kama ulimfanyia moja yeye atataka akulipe mara kumi yake.
Kumbuka mwanamke ni Multiplier, amplifier, ukimpa moja anaifanya kumi na moja.
Ukimpa kizuri kimoja anakifanya kinakuwa mara nyingi yake. Ukimpa kibaya anakizidisha maraduru yake
6. Wanawake hawatakiwi kuongoza sio kwa sababu hawawezi kuongoza bali ni kwa sababu ya tabia yao ya kutotaka maridhiano na maadui zao.
7. Mwanaume anaweza kuongea na mwanaume aliyemuibia Mke na wakaelewana kabisa na wakasameheana kabisa.
Lakini Mwanamke hiyo kitu haiwezekani.
8. Ongezeko la wanawake nchini kuwa vinara wa wanaharakati ni jambo ambalo linashangaza pakubwa na linaweza kutoa tafsiri mbalimbali.
9. Wanawake wao ndio huwaambia waume na watoto wao wasifanye harakati kwa kuhofia waume au watoto wao kuuawa.
10. Ukiona wanawake mmoja mmoja wanajiingiza front bila kujali wao ni wanawake. Bila kujali wana watoto au waume hii ni moja ya maajabu ya dunia.
11. Tafsiri yake kutakuwa na ongezeko zaidi la vijana na wanaume wanaharakati wasioogopa juwa front kwani watakuwa wamepewa go ahead na wanawake zao.
12. Ieleweke kuwa Wanaume wengi hupigana kufa kupona kwaajili ya Wanawake wao(wake), na watoto wao.
13. Ikiwa wanawake hulka ya uoga itaondoka na wakawapa moyo wanaume zao waende kupigania kile ambacho wanaona ni HAKI. Hakuna silaha yoyote ya kumzuia kijana.
14. Nilikuwa napitia mitandaoni na kufanya tathmini yangu kwa kulinganisha na miaka kadhaa nyuma. Kuona uchangiaji wa wanawake mtandaoni kuhusu mambo yanayohusu harakati na siasa;
15. Nikabaini kuwa kuna ongezeko kubwa la wanawake ambao woga unatoka na wana ujasiri wa kutoa maoni yao yenye mlengo wa kutaka haki kwa gharama yoyote.
16. Nataka niwaambie wanawake ndio walezi wa watoto na vijana.
17. Wanawake hawana nguvu za mwili lakini wana nguvu ya ajabu ya ushawishi kwa watoto wao.
18. Mwanamke(mama) akimuambia kijana wake apambanie HAKI kwa gharama yoyote. Nakuhakikishia huyo kijana atafanya hivyo bila kusita.
18. Unaweza kupuuza wanaume. Unaweza kuwaonea wanaume mambo yakaenda lakini huwezi kupuuza wanawake au kuwaonea alafu mambo yakaenda.
19. Ikiwa mama anaweza kumpa maneno ya sumu mtoto kwa Babaake mzazi. Na akamchukia kwelikweli. Vipi mama akampa mtoto sumu kuhusu watu wengine ikiwemo serikali.
20. Kisiasa usipoungwa mkono na wanawake ni jambo la hatari sana. Kuwakasirisha wanawake na kuwapandisha uchungu ni jambo ambalo sio salama.
21. Nataka nikuhakikisha usalama wa nchi yoyote ni wanawake.
22. Wanawake ndio hutuliza wanaume zao na watoto wao huko majumbani. Huwapa moyo na faraja na matumaini na kuwaambia watulie mambo yatabadillika.
23. Sasa ongezeko la wanawake kuingia katika harakati kiintelijensia lazima lichukuliwe kwa ukaribu, uangalizi wa kutosha na maboresho ya malalamiko katika haki yafanyike.
24. Sio kwamba Taikon natishia watu. Hapa na. Nazungumzia ukweli uliowazi ambao kwa wengine huenda inachelewa kuonekana.
25. Wanawake ndio wanaweza kujua HAKI ni nini kwa sababu wao ndio wanazaa kwa uchungu. Wao ndio wanaleta watu duniani.
26. Ukiona jamii inaupole basi moja kwa moja ujue wanawake wa jamii hiyo ndio wapole.
27. Ukiona mtu fulani ni jasiri wewe usipate shida kumtathmini yeye wewe angalia wafuatao. Mamaake, mkewe na binti zake.
28. Binti yako au mkeo au Mama akikuambia kijana wangu, mume wangu au Babaangu fight kwaajili ya haki, kwa ajili yetu. Huyo mwanaume hakuna namna atakuwa mwoga.
29. HAKI ni suluhisho la migogoro
30. Unapoleta maridhiano hapa unazungumzia HAKI Kufanyika na sio vinginevyo.
Ijumaa Kareem.
Nawatakia maandalizi ya Sabato
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam