Idadi ya wanachama CHADEMA yapaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya wanachama CHADEMA yapaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Technician, Jul 12, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna kila sababu ya kujiuliza sababu kubwa ya kuongezeka kwa idadi kubwa sana ya wazee kwenye vyama vya upinzani ni kubwa inakaribia kuwazidi vijana ambao inasemekana kuwa vyama vya upinzani ni kimbilio lao.Kila kukicha unasikia “””nasubiri uchaguzi 2015 nikapige kura,safari hii mpaka kieleweke””””Kila kijana unayekutana naye njiani ndio msemo wake.Ukimuuliza …….ni CHADEMA TUU …..hakuna kingine.

  Chama cha ccm hakiwezi tena kuwatetea vijana wa nchi hii,na wazee ndio wameshasahaulika kabisa hata wanapostaafu hawapati mafao yao kwa wakati,ukiachilia mbali matibabu yanayoahidiwa kila siku ya bure kwa wazee ni kama changa la macho (msemo wa waheshimiwa mjengoni)

  Asilimia kubwa ya vijana wa Tanzania wanahamia siasa za vyama vingi.hii ni ishara kuwa chama kikongwe kimeshindwa kuhimili mikikimikiki ya hawa vijana,na wanapopewa nafasi kwenye chama kikongwe wanaambulia kutukanwa kutokana na sababu nyingi ikiwamo umaskini wa watanzania na rasilimali nyingi kuchukuliwa na wawekezaji kutoka nje.

  [FONT=&quot]Utafiti huu ni wangu binafsi na hautachukuliwa kuwa ni utafiti halali wa taasisi au jumuiya yoyote.hakuna ushahidi wa moja kwa moja bali ni nadharia iliyojengeka ndani ya imani yangu kuwa kila kijana wa Ki-Tanzania mwenye akili Timamu na mwenye kuipenda [/FONT] nchi yake ,ardhi yake na mazingira yake basi anajiunga na CHADEMA.

  SOURCE:
  MIMI MWENYEWE.KOMREDI.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Tumekupata mkuu.
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilifanya mwenyewe kuulizia kila ndugu/rafiki/jamaa kama anaridhishwa na serikali asilimia 85 wamesema hawaridhishwi; je nini mbadala wao; asilimia 75 wanasema Chadema ndio kimbilio; kinachowapa imani ni nini; kati ya wanaoona chadema kimbilio lao; wanaoma nguvu ya chadema imetokana na umahiri wa wabunge wao (usomi wao) na siasa za kisasa za Dr Wilbrod Slaa; zinafanya Chadema ipae juu sana sasa
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,952
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  Kinachotakiwa ni kubadili mfumo wa Magamba!
   
 5. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Niliwahisema katika moja ya post zangu kuwa rais, uongozi, au chama kilicho madarakani kwa muda mrefu watu hukichoka. hutaka mabadiliko.

  Pili,uongozi wa muda mrefu madarakani hujisahau, huacha kutumikia umma na kuanza kujitumikia, kutumikia familia zao,rafiki zao. na hapo ndipo wananchi huuchoka uongozi huo. Mfano, Kanali Gadafi amefanya mambo mengi mazuri kwa nchi yake. Kwa kutawala muda mrefu alijimilikisha nchi yeye, familia yake na rafiki zake.

  Kwa hiyo, CCM hata wangejivua magamba yote leo hii; wananchi wamewachoka. Na dalili ya kuchokwa inadhihirishwa na wizi wao wa kura katika chaguzi karibu zote. Aidha, ripoti ya wasimamizi wa kimataifa kwa uchaguzi uliopita inasema moja ya sababu ya idadi ya wapiga kura kupungua katika uchaguzi uliopita ni wananchi kuuchoka utawala wa muda mrefu wa ccm.
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kila mahali kila mtu anataka kadi ya Chadema. That is a facts.
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Ni kweli sana kiongozi lakini upatikanaji wa kadi kwa Chadema ni wa shida sana. Sijui hapo kwako Ubungo
   
 8. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima yako mkuu Mikael P.
  Viongozi wa CHADEMA wachukue tahadhari kubwa kwa mamluki wanaokuja CHADEMA kuvuruga chama.Kutakuwa na wanachama wengi sana kufikia 2012 kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa mtaa.
   
 9. J

  Joblube JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Utafiti ulioufanya ni kama wangu kabisa assee hivi tukimwomba Mungu hawezi kumwondo JK madarakani kabla ya 2015 kama alivyomwondoa Sherk Yahaya.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nimepokea utafiti wako kwa mikono miwili!kazi nzuri,endelea kufanya tafiti zaidi ili tupate ukweli!!
   
 11. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Utafiti wako mzuri,japo sisi tuliogua mahesabu utafiti usiojumuisha namba mhh! Next time uweke vijipercentage vya waliohojiwa,na ushauri. Binafsi nakuamini sana hasa nijuapo kuwa miaka 4 ijayo serikali itakuwa imezalisha wapiga kura si tu wale wenye chuki dhidi yake bali wenye kukerwa na kunyimwa mikopo,waliopelekwa shule za kata,walimu wenye kudai haki zao za mapunjo ya mishahara,maaskari wanaolipwa mshahara wa mwezi sawa na posho ya robo wiki kwa mbunge,watoto wa maskini aliyekatazwa kuchoma mkaa akapoteza ajira watoto wakafukuzwa shule,mfanyabiashara anayeelemewa na matamko ya kutouza mahindi nje ya nchi,mafuta ya taa bei juu,umeme umekuwa hanasa. Yani kufikia 2014 watu mahututi hawatakubali kurudia makosa kwa kumchagua muuaji. Nawaasa cdm walegeze kamba ktk kuibana serikali ili kila kitu kipande,sukari itoke 2200 mpaka walikotaka cdm sh.1700 iuzwe 3000, mafuta ya taa lita itoke hapa ilipo sh.2250 ifike 5000, umeme unit moja ifike sh.500, ndipo watanzania wanaofanya mzaha kwa kuhudhuria sherehe za Tanu pale ubungo plaza wakitokea gizani mitaani kwao ndo watatia akili. Wengi waipendao ccm ni wauza samaki,urojo na cement na majenereta ila ukija viwandani,mashuleni,afya,vinyozi, vyuoni n.k wanaiona ccm kama matapeli. Mwisho waja ambapo kila raia atayakubali maamuzi ya umma na wanamapinduzi.
   
 12. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkubwa ni kweli kabisa, CCM ipo mahututi ICU,ni sawa na mtu ambae tumboni ameoza lakini anatembea kwa kudra za Mwenyezi Mungu,siku akianguka wenye kujua huwa hawashangai kabisa.Kama ni mfanya biashara mzuri basi ukitaka biashara inayotoka sana kwa sasa ni vifaa vya CHADEMA,ukitua navyo mahali ujue vinaisha haraka sana mkubwa,watu wamechoka hadi vijijini kilichbaki ni kukaza buti tu ili 2014 wakione cha moto kabla hatujaingia kwenye mtanange wenyewe.
   
 13. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kaaazi kweli kwelii...
   
 14. A

  Abel Pangamawe New Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Reserching is better inaweza kukupa walau kapicha lakini hii ya kufikiri tu si sahihi sana na vijana wengi wa tanzania ni washabiki tu tena wa muda mfupi sio committed sana kama mataifa mengine that is why tunachelewa kuleta mabadiliko. thank you for dedication time spared on it.
   
Loading...