Kwanii usiwasiliane na wakandarasi mbali mbali ili kulinganisha ujuzi?
Mkuu, kuna tatizo gani ukiwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki walioko nyumbani ili wakutafutie hizo dataz.Heshima mbele mkuu,
Majibu ya humu huwa yanafaida kwa wengi sio kwa muulizaji tu
kuna watu wako mbali na nyumbani(Tanzania) na hawana uwezo wa kuwaona hao makandarasi na wana plan ya kujenga maghorofa mara wafikapo nyumbani,
kama unajua weka wazi tu ili watu wakokotoe gharama
Mkuu nakutahadharisha tena nakuomba sana, ujenzi wa ghorofa (gorofa) maswala ya nondo mwachie Engineer si suala la kukisikia au kuulizia mitaani au kwa fundi mzoefu. Nasema hakuna kitu kama hicho, utakuja juta baadae!! Mahesabu ya nondo yanafanywa kwa utaalamu (calculations) kutumia fomula sio kukisia, ukubwa wa eneo/unene wa zege (floor thickness), matumizi ya jengo na pia ratio (vipimo) vya zege. "Foundation" ndio inabeba kila kilicho juu ya ghorofa, kwa hiyo huwezi kubadili juu bila kurekebisha chini au kujua chini kuna uwezo gani.
* Tuache njia za mkato, mme sahau mara hii kilichotokea Changombe/Kariakoo/Kisutu na kwengineko?
Haiwezekani kupata jibu kwa data hizo tu, inategemea na design ya jengo, aina na concrete mix, hizo nondo zitapangwa vipi etc.
Pia unasema ghorofa ya n hauwezi kufanya hesabu kihivyo, construction ya ghrorofa ya n iko effected na ghorofa zilizo juu yake na probably chini yake as well. Kwa kifupi zidhani kama unaweza kupata jibu la maana bila kuconsider design nzima.
Wapo lakini mkuu kuna taaluma zingine zinahitaji face2face consultations, sio rahisi kuomba ushauri wa daktari unapohitaji upasuaji ni lazima daktari afanye mwenyewe. Mgonjwa huwezi chukua kisu ukapasua tumbo. Kadhalika masuala ya nondo kwenye jengo la ghorofa ni mambo ya calculation si ya makisio kama vile unavyofikiria. Kwa maana ingine ni taaluma ya kulipia, ndio maana lazima Engineer uwe legally registered/licensed ili ukiboronga uwajibishwe.kwani humu hakuna engineerz?
Naomba nifahamu ghorofa standard yenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 10 inahitaji nondo za aina ngapi na kwa idadi ipi ili kukamilisha ile level ya kwanza tu bila kuhusisha zile zilizoko katika foundation na beam. Hapa nataka nifahamu idadi ya nondo kwa kila 10 or 20square meters ya 1st, 2nd....n floors.
Kinacho determine idadi na aina/ubora wa ndondo sio ukubwa wa eneo peke yake. Designer atatakiwa kujua pia aina ya mzigo inayokusudiwa kubebwa na hiyo floor (dead and live loads) na location zake. Kwa kifupi ni vigumu mno kwa engineer yoyote kuja hapa kusema ni idadi fulani ya nondo utahitaji unless afanye assumption ya hizo factors zote nyingine.
Best option ....chukua ramani zako muone QUALIFIED ENGINEER atakueleza kila utakacho taka kujua. Maelezo utakayopewa hapa sikushauri kuyapokea.Heshima Mbele mkuu Kang,
Haya hapa chini ni maelezo muhimu ya jamaa
"Naomba nifahamu ghorofa standard yenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 10 inahitaji nondo za aina ngapi na kwa idadi ipi ili kukamilisha ile level ya kwanza tu bila kuhusisha zile zilizoko katika foundation na beam. Hapa nataka nifahamu idadi ya nondo kwa kila 10 or 20square meters ya 1st, 2nd....n floors."
Naomba nifahamu ghorofa standard yenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 10 inahitaji nondo za aina ngapi na kwa idadi ipi ili kukamilisha ile level ya kwanza tu bila kuhusisha zile zilizoko katika foundation na beam. Hapa nataka nifahamu idadi ya nondo kwa kila 10 or 20square meters ya 1st, 2nd....n floors.