Nikichangia hoja hii nasema irudi kama zamani au kama zamani sana. Zamani sana ni katika mfumo wa mwanzo kabisa wa Tanganyika yaani Majimbo. Hii haimaanishi ni kuunga mkono UKAWA au chama chochote. Ni jambo ambalo lilikuwepo huko nyuma. Hata hivyo ikishindikana, mikoa ibaki ile ile 20 huku Bara na 5 Znz. Mipaka inaweza kufanyiwe re-demarcation/relocation ili kubalance ukubwa wa mikoa. Kwa mfano, mkoa wa Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mtwara ni midogo sana, lakini ina watu wengi kwa maana Population Density(People per km) ni kubwa! Dar inaweza kumegewa maeneo ya Mkuranga, Kisarawe na Bagamoyo, wakati Mtwara inaweza kumegewa Tunduru na eneo la Lindi Vijijini. Kilimanjaro inaweza kumegewa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tanga na Manyara!