Idadi ya makanisa kudhibitiwa Burundi

Idadi ya makanisa kudhibitiwa Burundi

Status
Not open for further replies.

mansoorsaid

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Posts
1,498
Reaction score
286
140710113016_burundi_kanisa_512x288_bbc_nocredit.jpg


Bunge la waakilishi nchini Burundi,limepitisha mswada unaodhamiria kupunguza ongezeko la makanisa nchini humo.

Utafiti wa serikali uliofanywa mwaka jana, ulipata madhehebu 557 ya waumini wa kikristo wanaofanya ibada zao nchini humo.

Sheria hiyo mpya itahitaji makanisa kuwa tu na waumini 500 pamoja na jengo nzuri linalotumiwa kama kanisa.

Makanisa ya kiivanjelisti, yalianza kuongezeka kabla na baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika 2005 ambapo karibu watu 300,000 waliuawa.

Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, Prime Ndikumagenge, anasema kuwa mswada huo uliungwa mkono na wabunge wote katika bunge la waakilishi na huenda usipingwe utakapowasilishwa kwa baraza la Senate.

Ikiwa hautafanyiwa mabadiliko yoyote, mswada huo utahitajika kutiwa saini na Rais ishara ya kuudhinisha na kuufanya sheria mpya katika siku 30, la sivyo urejeshwe kwa bunge la waakilishi kurekebishwa.

Pindi itakapotiwa saini, makanisa yatapewa mwaka mmoja kufuata sheria hiyo na masharti mapya.

Kwa kanisa la kigeni kusajiliwa , lazima wamiliki kuonyesha kuwa iliwahi kuwa na waumini 1,000.

'Kashfa makanisani'

140710113130_burundi_kanisa_512x288_bbc_nocredit.jpg


Ni jambo la kawaida kuona waumini wakiwa wamepiga kambi kando ya barabara katika mahema wakifanya ibada siku za Jumapili.

Mtu yeyote anaweza kujitangaza kama muhubiri na kumekuwa na kashfa kadhaa zikihusisha kanisa ndogo ndogo.

Baadhi ya wahubiri wametuhumiwa kwa kuwanyanyasa waumini.

Kuna kisa kimoja ambapo muhubiri aliwaambia wanawake wasio na uwezo wa kushika mimba kulala naye ili awazalishe.

Idadi kubwa ya watu nchini Burundi ni wakristo, wakati wengine wanafuata itikadi za kitamaduni.

Wakati wa mjadala kuhusu swala hilo bungeni, mbunge mmoja kwa jina Jean Minani, aliwatakia waumini wenye imani ambazo sio za kidini kuruhusia kuabudu watakavyo.

Lakini waziri wa mambo ya ndani alipuuza imani hizo na kuzitaja kama za kijadi na zisizokubalika.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza - ambaye zamani alikuwa muasi, alichaguliwa kama Rais mwaka 2005 na ni mlokole huku mkewe akiwa muhubiri katika kanisa la kiivanjelisti.


Chanzo: BBC swahili
 
Na asubuhi nimesikia kila Mwanamke wa Kirundi ana wastani wa watoto saba, hongera zao kwa kujaza nchi.!
 
unamanisha madhehebu.? Au dini.! Sina uhakika kama mkoa mmoja unaweza kuwa na dini zaidi ya 400, labda madhehebu, hata dunia nzima haina dini zaidi ya 400, acha uwongo, kama vipi taja dini hata 4 zilizopo mbeya.!
 
inaweza kuwa idadi ya makanisa, sio madhehebu wala dini.!
 
Ninavyofahamu mm kuna dini ya kikristu na kiisilam mkuu anamaanisha madhehebu
 
mkuu id yako ni kama unatokea sehemu za Burundi je ni kweli.?

Hata akibisha nitamtetea kuna kabila la Waha majina yao yamefanana na watu wa Burundi. Wahaya na Uganda. Wanyakyusa wa kyela na Malawi.
Kubwa kuliko ni wa Maasai wa Arusha na Kenya.
 
Dini inaleta ustaarabu

Hakuna kitu kama hicho tena kwa sehemu kubwa inchangia kuharibu ustaarabu na kuondoa amani!!haswa haya madhehebu wanayojiita walokole mengine ni hatari mno!!wanajifanya wanajua kumbe wanaungua jua
 
Hakuna kitu kama hicho tena kwa sehemu kubwa inchangia kuharibu ustaarabu na kuondoa amani!!haswa haya madhehebu wanayojiita walokole mengine ni hatari mno!!wanajifanya wanajua kumbe wanaungua jua

Acha waabudu wanachoamini na ulokole wao watajua wenyewe ndo mana kukawa na freedom of worship na hamna dini bora kuliko nyingine inategemea na muumini mwenyewe
 
ni jina langu, Mtanzania... Mwenye asili ya Burundi na Rwanda.. babu yake na babu alitokea huko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom