Idadi sahihi ya siku za mapumziko ya sikukuu ya Idd kitaifa ni 2 au 5?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
habari wapendwa!

kutokana na kwamba baadhi ya skukuu kubwa husherekewa kwa pamoja kitaifa na kimataifa!

  1. Naomba kufahamishwa hapa Tanzania kama Taifa idadi sahihi ya siku za mapumziko ya skukuu ya idd ni 2 au 5?

Maana nasikiaga tetesi Zanzibar wao huwa wanakula idd siku 5 je tunatofautiana nao namna ya kusherekea kitaifa?
2. siku za kitaifa zina mipaka kati ya bara na visiwani?

Pia naomba kufahamisha ikiwa bara tuna Sheikh Mkuu ambaye ndiye msemaji Mkuu wa waisilam Tanzania;

3. Swali: Shekhe Mkuu huyu anahusika hadi Zanzibar au ukuu wake haufiki visiwani?
4. Bakwata inawahusu wazanzibari au kule napo ipo Bakwaza?

5. Je; Zanzibar nayo ina sheikh Mkuu wake?

Ikiwa Rais wa Zanzibar kipindi cha mfungo alisikika akipiga marufuku watu kula hadharani;
6. je; Rais Alizungumza kwa niaba ya serikali au kwa niaba ya imani ya dini ya kiislam kama sheikh? Aliyekaidi angeshitakiwa na jamhuri au kadhi?

Naombeni majibu wadau

CC; kipozeo
 
Shekhe huyu nadhani hayupo kwenye maswala ya muungano huyu wetu sisi huku bara
 
Nadhani mengine tuya ache yalivyo na tukubali kwamba ALLAH ndiye ajuaye zaidi.
 
mmmh hii ya kula idd siku 5 naisikia leo
Sherehe za Idd zinakua siku 4 Zanzibar sio 5 lakini sherehe tu kwa maana ya Viwanja vya kufurahishia watoto vinakua wazi kwa hizo siku nne. Ila kazi zinakuwepo kama kawa kama kalenda ya serekali inavyosema
 
kwanini Zanzibar siku NNE na bara siku mbili?
 
katika uislam idd kubwa (eid al hajj/ al adha) hua ni mwezi 10 ikiambatana na masiku matatu ya kuanika nyama (ayyam tashriq) ambayo ni mwezi 11 hadi 13 ko ukijumlisha hapo unapata siku 4 ambazo ni haramu muislam kufunga swaumu ndani ya siku hizo hivyo ni mwendo wa kula na kunywa
 
duh
 
Peleka hili swala lako kwa waziri anaehusika na Muungano ili likajadiliwe kama unahisi nalo ni miongoni mwa kero za Muungano..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
Mungu Ibariki Gairo
 
Back
Top Bottom