Hii ni moja ya idea mbovu ambazo nitazipinga kwa nguvu zote, hakuna haja ya kuwa na board ya ICT, IT/CompSci/ICT/ haifanani na traditional engineering kabisa, hakuna strictly right or wrong way ya kufanya kitu ni field siyo tu inayobadilika kila siku lakini watu wanatakiwa wawe na uhuru wa kusolve matatizo kwa njia mpya za kiubunifu, ICT zaidi ya kuwa Science pia ni Art.
Board itadumaza taaluma na kuzuia new comers wasiingie kwenye field na nahisi itatumika kuzikandamiza kampuni na developers wadogo.
Beauty ya IT ni kwamba kijana mdogo ambaye hana uzoefu wowote anaweza akakaa chumbani kwake akafanya mambo ambayo yanaitetemesha kampuni yenye Mabilioni benki kama Microsoft au Apple. Jiulize kama hiyo board ingewasaidia akina Bill Gates, Michael Zuckerberg, Larry Page etc
Pia sioni haja kwa kuwa kuna standards na certifications kibao tayari, so kama mtu anayeona anahitaji project yake ifanywe kwa kufuata standard au technology fulani yuko huru kuwatafuta watu walio certified kwenye standard/tech hiyo.