Icc yasema "mauaji ya gaddafi ni uhalifu"

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Kifo cha aliyekuwa kiongozi
wa Libya Muammar Gaddafi
"kimesababisha mashaka" ya
kugeuka uhalifu katika vita,
amesema kiongozi wa
mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu kesi za
jinai. Luis Moreno-Ocampo
amesema ICC imeanza
kulishuku Baraza la mseto la
Libya (NTC). Kanali Gaddafi aliuawa tarehe
20 Oktoba alipokamatwa na
waasi kijijini alikozaliwa
Sirte. Viongozi wa Baraza la mseto
mwanzoni walidai kuwa
aliuawa wakati wa
mapigano, lakini baada ya
shinikizo kutoka Mataifa ya
magharibi wakasema watafanya uchunguzi. Bw Moreno-Ocampo
amewaambia waandishi wa
habari kuwa "nadhani mauaji
ya Kanali Gaddafi yanazua
maswali na hofu ya uhalifu
wa kivita. "Naona kuwa hili ni suala
nyeti. Na tunaelezea hisia zetu
kwa wakuu wa nchi hiyo na
wao wameanza kuandaa
mpango wa jinsi ya
kupeleleza uhalifu huu." Wapiganaji waasi walimkuta
Kanali Gaddafi amefichama
ndani ya mtaro wa maji
machafu kufuatia mapigano
ya muda mrefu
yaliyofanyika katika mji alikotoka Kanali Gaddafi wa
Sirte. Picha za video zilizotangazwa
wakati wa kukamatwa
kwake zilimuonyesha
kaueruhiwa ingawa alikuwa
hai bado, huku
amezungukwa na wapiganaji waasi waliojaa ghadhabu. Aliburuzwa kupitia halaiki ya
watu akipigwa na
kuangushwa chini mara
kadhaa, kabla ya kupotea
huku nyuma yake ikisikika
milio ya risasi na mdundo. Mwanae Mutassim,
aliyekamatwa naye akiwa
hai, aliuawa mikononi mwa
waasi hao. Mahakama ya ICC imemtaja
mtoto mwingine wa Kanali
Gaddafi, Saif al-Islam, kwa
tuhuma za uhalifu katika vita
kwa hivi sasa akiwa
mikononi mwa Mamlaka ya Libya. Bw Moreno-Ocampo
amekubali kuwa kesi dhidi
ya Saif al-Islam isikilizwe
nchini Libya, na sio The Hague.
 
Eti leo Icc ndo wanaona kuwa kuna makosa, WANAFKI WAKUBWA HAWA, BORA WAKAE KIMYA.
 
Back
Top Bottom