ICC imeishia wapi?

Sasa umeanza kunielewa!! Nashukuru unatumia akili yako positively
Sijawahi kuwa na mawazo ya kuwategemea ICC au mtu mwingine yeyote toka nje ya Tanzania kuja kufumbua matatizo tuliyonayo hapa.
Usijifanye kuwa huna akili kabisa hata za kuelewa kilichoandikwa.
 
Naona kimya as if nothing had happened in TANGANYIKA
Yaani ICC waje wamshtaki Rais na wasidizi wake (JWTZ & TANPOL), waliozima machafuko ya uharibifu wa mali, wizi, uchomaji moto mali kwa ufanisi wa hali ya juu ndani ya masaa 12??? Hakuna ICC ya hivyo
 
Story za vijiweni wakati wa kunywa kahawa, hakuna kesi itakayomkabili SSH na serikali anayoiongoza.

Serikali ilizima shambulizi la mapinduzi yaliyopangwa kwa njia ya kuleta machafuko.

Hakuna shambulizi haramu linaloweza kuzimwa kwa wahusika kupewa mashada ya maua.
 
Samia mhalifu atashukuru sana wakija; kwa sababu hiyo ndiyo matumaini pekee yatakayompa fursa ya kununua muda.
Mkuu kuna vituo vya mwendokasi vilichomwa tarehe 29 October havijaanza kazi mpaka leo, kuanzia pale Morocco kuelekea Kivukoni hakuna usafiri huo kwa sababu vijana walichoma moto na wakaiba maduka ya watu.

Ulitaka wachukuliwe kiungwana wakati wao walishatanguliza vitendo vya kihuni?.
 
Hawa tunaoongea nao humu wengi ni mawakala wa taasisi za kizungu, walitaka baada ya ushenzi ule mitaani serikali iwaruhusu waende mpaka ikulu wakachukue nchi kirahisi tu!!.

Hawawezi tena kurudia kufanya ule ujinga.
 
Nani alipanga mapinduzi?
Ni huyu lisu anayetuhumiwa uhaini? Au TEC kupitia kitima ambao wanaogopwa kupewa kesi ya uhaini?
 
Ili kiongozi aweze kupelekwa ICC kwanza kinachoangaliwa ni nani aliyeanzisha hizo vurugu, iwepo intention ya kufanyika kwa hayo mauaji kwa asilimia 100.

Kule Rwanda wameshtakiwa wale wauaji wa kihutu kwa sababu ushahidi wa mipango ya awali kabla ya jinai kutekelezwa upo dhahiri kabisa.

Kule Ujerumani walishtakiwa wale wasaidizi wa Hitler kwa sababu ulipatikana ushahidi wa genocide kuandaliwa mapema, mpaka upo ushahidi wa kujengwa kwa yale majiko maalum ya kuwachomea wayahudi.

Tanzania hakuna ushahidi wa serikali ya SSH kupanga kuua vijana kabla ya October 29, serikali ilizima uasi wa mapinduzi haramu hivyo huwezi kumshtaki Rais anayeilinda nchi aliyoapa kuilinda, suala lake ni tofauti kabisa na namna ICC inavyowakamata washtakiwa wa mauaji kwenye mataifa mengi duniani.

Zisingetokea zile vurugu za kuchoma maduka na biashara za watu hakuna mtu hata mmoja ambaye angepigwa risasi.
 
Nani alipanga mapinduzi?
Ni huyu lisu anayetuhumiwa uhaini? Au TEC kupitia kitima ambao wanaogopwa kupewa kesi ya uhaini?
Wanajijua wenyewe, kuna uhusika wa majirani zetu wa kaskazini walioshirikiana na watanzania walioamua kutusaliti.

Lissu kabla hajakamatwa aliapa kukinukisha dhidi ya CCM. Heche akasema uchaguzi hautakuwepo kabisa.

Ka kifupi walitaka turudi nyuma miaka 50 iliyopita, wenye akili wakaona hawa wachache hawawezi kuturudisha nyuma kipuuzi tu wakaamua kuwarudisha wao nyuma kwanza.
 
Amiri Jeshi huwa na sababu za msingi za kuamuru matumizi ya risasi, hakurupuki tu.

Jiulize kwanini mtandao wa mawasiliano ulizimwa katika siku zile tatu za vurugu, hasara yake ni bilioni 500 serikali ilipata kwa kuzima mawasiliano yale.

Yale yalikuwa mapinduzi ambayo kwa nje walitaka dunia idhanie ni maandamano ya kudai haki, walitaka waige ule ujinga wa Sri Lanka, eti waingie mpaka ikulu halafu waanze kuchezacheza kwenye vitanda vya viongozi wakuu kabisa.

Wamejifunza kitu muhimu sana kuhusiana na namna Tanzania ilivyo na mfumo wa kiulinzi.
 
Wewe ni nguruwe tu unayewaza masalia pekee toka kwa Samia; kiasi kwamba hutaki kujuwa huyo huyo mfigaji wako ndiye mhusika wa matokeo yote hayo unayoyataja wewe.
Hakuna namna nyingine, ni lazima mhalifu Samia awajibike kwa maovu yote anayoyafanya.
 
Wewe ni nguruwe tu unayewaza masalia pekee toka kwa Samia; kiasi kwamba hutaki kujuwa huyo huyo mfigaji wako ndiye mhusika wa matokeo yote hayo unayoyataja wewe.
Hakuna namna nyingine, ni lazima mhalifu Samia awajibike kwa maovu yote anayoyafanya.
ICC siyo ya baba yako wala haitoki kijijini kwenu Nangurukuru
 
ICC siyo ya baba yako wala haitoki kijijini kwenu Nangurukuru
Tanzania haina uhitaji wa ICC. Ungekuwa na akili unglilia sana hiyo ICC ije kumwokoa mwovu Samia kuliko yatakayompata katika mikono ya waTanzania wenyewe.
 
Tanzania haina uhitaji wa ICC. Ungekuwa na akili unglilia sana hiyo ICC ije kumwokoa mwovu Samia kuliko yatakayompata katika mikono ya waTanzania wenyewe.
Dua la kuku hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…