Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,873
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake
katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
Sasa tuongelee hawa wabunge wetu wanaotukana bungeni je, hawavunji maadili ya umma?

(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano
ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;
(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais;
(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge