Ibara ya 46(3) ya katiba yetu haitoi kinga kwa Rais alieondoka madarakani kutoshitakiwa kwa makosa aliyofanya kabla hawajawa Rais

Nimeamini kwanini mambo mengi yanayohitaji Ufafanuz na uamuzi wa Mahakama Bavicha huwa wanaleta Kwenye mitandao na sio kupeleka Mahakaman. Hivi katika hili la Rais kushtakiwa mbona katiba iko wazi kabisa?Kwamba bavicha vichwani ni WEUPE sana au ni kujitoa ufaham?

Linapokuja suala la siasa chafu sheria na katiba huwekwa pembeni. Sheria inayotumika ni ile iitwayo amri kutoka juu. Mtindo huu ndio unaotumika na mkulu, kuwaweka wapinzani wake ndani kwa sasa. Wakati huo ukifika hutaamini utakayoyaona. Lowassa na Sumaye walitamba sana enzi zao, leo hii huwezi kuamini upole wao. Acha jiwe atambe kwa sasa, ila atavuna anachopanda
 
Nakwambia jiwe ili akwepe kwenda jela anatakiwa abadiri katiba akae milele na akijaribu kubadiri katiba tuna mfanyia kitu ya Libya kwahiyo anatakiwa ajiandae maisha ya jela, na kazi ngumu
Alishasema kipaumbele chao ni maendeleo na sio katiba
 
Linapokuja suala la siasa chafu sheria na katiba huwekwa pembeni. Sheria inayotumika ni ile iitwayo amri kutoka juu. Mtindo huu ndio unaotumika na mkulu, kuwaweka wapinzani wake ndani kwa sasa. Wakati huo ukifika hutaamini utakayoyaona. Lowassa na Sumaye walitamba sana enzi zao, leo hii huwezi kuamini upole wao. Acha jiwe atambe kwa sasa, ila atavuna anachopanda
Mkuu mbona sikuizi umekuwa wa kulialia ovyo?Huyu aliyewekwa ndani bila sheria ni nani?Katiba gani inasema Rais akimaliza mda wake anashtakiwa?
 
Mkuu mbona sikuizi umekuwa wa kulialia ovyo?Huyu aliyewekwa ndani bila sheria ni nani?Katiba gani inasema Rais akimaliza mda wake anashtakiwa?

Narudia tena, kwenye siasa chafu sheria na katiba huwa chini ya amri toka juu. Hayo tunaona kwa macho yetu wala hatuhadithiwi. Kama unaamini katiba inaheshimiwa endelea kula kiyoyozi lakini siku yaja.
 
Katika katiba yetu ya mwaka 77,ibara ya 46(1),46(2) na 46(3),ndio zinazungumzia kinga ya Raisi kutoshitakiwa.

Ibara ya 46(1) na 46(2), zinazungumzia kinga ya kutomshitaki Raisi alie madarakani ambapo ibara ya 46(3) inazungumzia kinga ya kutomshitaki mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Raisi baada ya kuacha madaraka hayo ya uraisi.

Ukisoma ibara hiyo ya 46(3), utagundua mtu aliewahi kushika madaraka ya uraisi na baadae kuondoka madarakani, anaweza kushitakiwa kwa makosa aliyoyafanya kabla hajawa Raisi.

Ibara hii ya 46(3) inasomeka hivi:

Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Raisi kutokana na mashariti ya ibara ya 46A(10),itakuwa ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliekuwa anashika madaraka ya Raisi baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Raisi wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Raisi kwa mujibu wa katiba hii.

Kwa nilivyoelewa mimi layman wa mambo ya sheria na katiba;mpaka hapo ni kuwa, makosa aliyoyafanya huko nyuma kabla hajawa Raisi hayana kinga yoyote katika katiba yetu.

Na tutambue hiyo ibara ya 46A(10) iliyotajwa hapo inaongelea kumshitakI Raisi baada ya kuondolewa madarakani na azimio la Bunge.

Kama nimepotoka au kama kuna sheria-ambayo sasa itakuwa inapingana na katiba- inayomlinda mtu alieyahi kuwa Raisi asishitakiwe kwa makosa aliyoyatenda kabla hajawa Raisi,basi watalaamu wa mambo ya sheria na katiba mtusaidie.

Wengine hata hizo katiba hatuna weka kipande cha kifungu hicho ili tujiridhishe sababu sheria iko very technical.Upande mwingine itasema hivyo lkn ukienda in details utakuta exceptions kibao.
 
Kwa makosa yote yanayofanywa na rais plus mabaya yake yote......huwaga sikubaliani na swala kushtakiwa mala tu baada ya kuumaliza awamu au kushindwa uchaguzi mpyaaa,,,,,,,,mana pia kuna mazuri yake machache ambayo ameifanyia nchi na wamewagusa watu baadhi hata kama ni wachache.......
 
Akiwa waziri wa uje zi kulikuwa na u adhilifu wa
Tr4 tunaanzia hapo
 
Mkuu ni ww unapoteza muda kuangalia sheria zinasemaje. Kitakachofanyika ni kumkamata na kumweka ndani kwa amri kutoka juu. Akishawekwa ndani, zinaanza dana dana, mara mahakimu na mawakili wanaanza kuumana kwenye vifungu vya sheria. Hakuna dhamana kwa usalama, sababu ni kwamba kuna tetesi ya usalama wake iwapo ataachiwa. Hiyo kesi inapigwa tarehe za mbali na yanatolewa maelekezo nyuma ya pazia akutane na kazi ngumu. Ukiua kwa upanga atakufa kwa upanga. Kisha baada ya miaka mitatu akiwa ndani, hakimu anatokea anasema hiyo kesi ilifunguliwa kimakosa!
Very refreshing comment!
 
350103.jpg

Na Profesa ASSAD atakuwa shahidi
 
Kwa uelewa wangu mdogo naona upo sawa
Tafsiri na uwiano wa vipengele hivo viwili.

Article 46 (3):

Except where he ceases to hold the office of President pursuant to the provisions of Article 46A(10) it shall be prohibited to institute in court criminal or civil proceedings whatsoever against a person who was holding the office of President after he ceases to hold such office for anything he did in his capacity as President while he held the office of President in accordance with this Constitution.

Article 46A (10):

In the event the National Assembly passes a resolution that the charges against the President have been proved and that he is unworthy of continuing to hold the office of President, the Speaker shall inform the President and the Chairman of the Electoral Commission about the resolution whereupon the President shall be obliged to resign before the expiry of three days from the day the National Assembly passed the resolution.

Tafsiri/Maana kwa ufupi wa hizi Article Mbili za Katiba;

Article 46 (3): Inampa kinga Rais/Mtu aliewahi kuwa Rais kutokushtakiwa kwa kosa lolote la MADAI/JINAI kwa mambo aliofanya au ambayo alitakiwa kufanya na hakufanya wakati akiwa rais. Kinga anaenda nayo maisha yake yote. ILA kinga hii INAPOTEA kama tu ataachia kiti cha Urais kutokana na kipengele "Article 46A (10)".

Article 46A (10): Katika mazingira yoyote yale, BUNGE likipitisha AZIMIO kua mashtaka dhidi ya rais yameonekana kua HAFAI kushika/kuendelea na kiti/nyadhifa ya urais, basi SPIKA WA BUNGE anatakiwa kumpa muongozo/taarifa RAIS huyo na MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI juu ya maazimio hayo ya bunge.

Rais atawajibika kuachia ngazi/kiti ndani ya siku 3 toka azimio lipitishwe ***Kipengele hichi ndio maana rasmi ya BUNGE KUMVUA RAIS KINGA***

Uwiano wa Article hizi mbili kwa kifupi,

Rais ana kinga wakati akiwa madarakani na akimaliza muda wake wa madaraka kwa kipengele 46 (3), ila kinga yake inafutika KAMA atamwagwa na wabunge kupitia kipengele 46A (10).

*** Njia mbili za kumshitaki rais ni kwa kupitisha AZIMIO bungeni, la kubadilisha kipengele hicho au kumvua kinga yeye mwenyewe.

I humbly stand to be corrected,
 
Soma vizuri uelewa hiyo ibara ya 46(3).Kinga hapo ni kwa makosa aliyofanya wakati akiwa Raisi tu na si kwa makosa aliyoyafanya kabla hajawa Raisi.
Hiyo article ipo crystal clear mkuu kama ulivyosema. Kinga ni kwa makosa anayofanya Rais akiwa madarakani na si vinginevyo. Wakati akiwa bado hajashika madaraka hana kinga na akitoka madarakani akafanya makosa hana kinga. Kwa kifupi ni kwamba kwa mfano Rais Mstaafu JK ana kinga kwa makosa ambayo aliyafanya kati ya Mwezi Dec 2005 hadi mwezi Nivember 2015 wakati akiwa ameshika madaraka ya Urais. Kabla ya 2005 hana kinga na baada ya 2015 hana kinga kisheria/kikatiba.
 
Leo umekuwa mkweli na umesema ukweli ambao wenzako washabiki wa Jiwe kama kina MISULI wanaupinga ama kwa ubishi tu au kwakutokuja.

Ahsante sana kwa kuwa objective.
 
Back
Top Bottom