IBADA YA KULIOMBEA TAIFA
Kuna njia nyingi za kuonyesha hatupendezwi na yanayoendelea nchini na kuombea muafaka wa kitaifa kwa kushiriki ibada maalum tunaweza kutenga saa, siku kadhaa kuliombea Taifa. Hizi ibada, maombi dua maalum zinaweza kwenda pamoja na mfungo kila mtu kwa imani yake lakini zote ziwe coordinated.
NINI TUNAOMBEA.
1. Tunaombea wote waliopotea au kupotezwa wapatikane.
2. Familia za wote waliouwawa kama za familia za Soka, Mbise, Kibao kupata faragha.
3. Wote waliovunja viungo na kupewa vilema vya kudumu.
4. Wote walioteswa na wanaondelea kuteswa hata leo wakipitia maumivu na mateso makali kwenye mashimo ya polisi, nyumba za siri na misituni walipotupwa.
5. Wote walio ndani ya magereza kwa kupigania haki kama wanaoishi na kulala karibu na shimo la choo na kuteswa Tundu Lissu, Frida, Kiduku, Ofsa Ngiri na wengine.
6. Familia za wote wanaopitia maumivu ya kuondekewa na wapendwa wao.
7. Wote wanaoendelea kupigania haki na kusimama na ukweli pamoja na vitisho wanavyopokea. Vitisho kama kufungwa biashara zao, waliofukuzwa kazi, biashara zao kuharibiwa kwa kutetea haki, kusimama na ukweli.
8.Kuliombea Taifa letu kwa Mungu tupate haki, uwajibikaji na viongozi wazalendo wenye maono, uthubutu, wasio wezi, wakweli wenye upendo na nia ya dhati kulitumikia taifa hili na watu wake.
9. Kuliombea taifa kutupa haki, umoja, mshikamano na upendo.
Katika maombi hayo tunaweza kutaja majina ya wahanga wote moja baada ya lingine.
Hii ibada inaweza kuwa dakika,saa, siku kadhaa au mkesha wa siku moja au ibada itayoendelea hadi tutakapopata suluhu, muafaka wa kitaifa.
Tunaweza kukusanya sadaka inayoweza kupelekwa kwa wahanga wa watekaji, familia zao na wale wote wanaopigania haki, uwajibikaji na Tanzania bora kwa watu wake wote.
Wakati wa hizi ibada, siku hizo tunaweza kuonyesha mshikamano wetu kwa kuvaa nguo nyeusi au nguo nyeupe kama ishara ya umoja na mshikamano.
Ni muhimu hizi ibada zote zirekodiwe na kuwekwa mitandaoni kote kama Tiktok, youtube, Instagram, X, Telegram.
Sababu za kuweka kwenye mitandao ni
1.Wale wasioweza kwenda kwenye nyumba za ibada kupata nafasi yakushiriki.
2. Kuhamisha umoja, mshikamano na upendo.
3. Kuwapa wahanga faragha, kuwatia moyo walio katika wimbi la majonzi, maombelezo pamoja na kuwatia moyo.
Kwa wale waokwenda kwenye ibada wenye uwezo wanaweza kuleta chakula, maji, juice ili wale wasio na uwezo wapate chakula, lakini pia ni vizuri kula pamoja kama familia ya moja ya Watanzania.
2.KUKAA NYUMBANI.
Kupanga siku miji, mbili, tatu, wiki Watanzania wote kukaa nyumbani kwa pamoja siku tutakozichagua.
Tunaweza kuonyesha kutopendezwa na mambo yanayoendelea kwa umoja wetu kukaa nyumbani na kutoenda kazini, kutofungua biashara au kwenda shambani kwa siku kadhaa pamoja mfungo wa kula chakula na kutafakari mustakabali wa Taifa letu.
Kama hata robo ya Watanzania wasipojitokeza kuendesha daladala, bajaji, bodaboda, wanafunzi, walimu, polisi, wanajeshi, sekta zote binafsi na za umma hata tukifanya kwa siku tatu, saba serikali itapata ujumbe na kutafuta muafaka.
Hizi njia mbili ni ngumu kuingiliwa na polisi au kikosi cha utekaji. Pia tutakuwa hatuvunji sheria yoyote ya nchi. Unaweza kutoa sababu yoyote, udhuru au dharura ya kutokwenda kazini.
Hiyo itatuma message kwamba hatufurahishwi na yanayoendelea tunahitaji muafaka wakitaifa wote kwa umoja wetu ikiwa ni pamoja na kuwatoa watu magereza, nyumba za siri za mateso, katiba mpya, uchaguzi mpya ulio huru, wazi na wa haki.
Tutaweza kuwa na hashtag kama
# Muafaka wa Kitaifa.
#Haki, uwajibikaji umoja na upendo TZ wote.
#Tiktok challenge iwe wimbo Imeniuma sana by Zabron Singers.
Maoni ya wadau wote yanakaribishwa.
Kuhusu mambo na vitu vya kuviombea.
Njia za kushirikisha na kuwafikia watu wengi zaidi.
Hashtag nzuri.
Maoni yoyote chanya.
Kwenye tiktok challenge unaweza kubadilisha maneno yawe kuliombea taifa haki, uwajibikaji, upendo kwa Watanzania wote.