Kuwa kwenye uhusiano ni jambo lenye kheri hasa ukiwa na mtu ambae unampenda na yeye anakupenda.
Kila mtu hufarijika kwa kiasi kikubwa kuona Kuna mtu nyuma yake mwenye kumjari.
Inauna sana kuona unavaa nguo hakuna mwenye kukuambia umependeza. Inasikitisha sana kuona hakuna mtu mwenye kukupa faraja pindi unapopambana na Ugumu wa aina yoyote. Lakini ni simanzi na majonzi pia kuona huna mtu ambae ni msiri wako, mtu unaeweza kujifunua kwake na yeye akajifunua kwako.