I love these ladies; don't you (picha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I love these ladies; don't you (picha)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 31, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Askari Polisi wa Kike kutoka Tanzania Waelekea Dafur Kulinda Amani

  [​IMG]

  Kamanda Munisi akikabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa Mkuu wa msafara huo Mrakibu wa Polisi Hawa Luzy.

  [​IMG]
  --------------

  Na Mohammed Mhina na Charles Tupa wa Jeshi la Polisi.

  Kundi la kwanza la Polisi wanawake linaondoka nchini kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya kuongeza nguvu katika maswala ya kulinda amani katika eneo la Darfur nchini humo.

  Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema,Mkuu wa Utawala Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Zuhura Munisi,amewaasa askari hao kwenda kuzingatia maadili ya kiutendaji ili kuleta heshima ya taifa letu mbele ya sura ya Umoja wa Mataifa.

  Kamanda Munisi amesema kuteuliwa kwa askari wanawake kwenda kulinda amani nchini sudani kunatokana na ukweli kwamba wengi wa wahanga walioko katika maeneo yanayokumbwa na migogoro nchini sudani ni wanawake na watoto.  Kamanda Munisi amewakabidhi bendera ya Taifa askari hao kwa Mkuu wa msafara huo Mrakibu wa Polisi Hawa Luzy.

  Naye Mkuu wa Mahusiano ya Kimataifa wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Geofrey Kamwela amesema kuwa kundi hilo linakwenda kuungana na askari kutoka nchi mbalimbali duniani zinazolinda amani nchini sudani.


  Kamanda Kamwela amewataka Askari hao kwenda kudumisha nidhamu na kuzingatia maadili na tamaduni za raia wa Sudan ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Wengine waliohudhuria katika hafla ya kuwaaga askari hao ni Makamanda ACP Adolfina Chialo na Afisa Mnadhimu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi SSP Hassan Mbezi.

  My Take

  Sasa..kipaumbele ni kipi.. kupokea mipira, baskeli na viatu au kuwaaga mabinti na dada zetu wanaoenda mbali wakiitikia wito wa taifa lao? Yaani hata Waziri hayupo wa kuwapa bendera..? I'm sorry.. I couldn't resist..

  Nevertheless, I'm so proud of these daughters of our nation serving in the tradion of many so other women who have served our nation with distinction. You go girls!! Salute!
   
 2. K

  Kijunjwe Senior Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inasikitisha, inaleta picha mbaya na kuvuja morali ya askari wetu. Sina hakika kama ni dharau au lah au hakukuwa na taarifa ya kupewa majukumu hayo kwa askari wetu. Wanamichezo hupewa heshima na waziri mwenye dhamana, sasa inakuwaje hawa hata waziri mwenye dhamana hayupo? au kwa kuwa ni wanawake(Siamini). Kuna kitu hakijakaa vema hapa.

  Kazi njema dada zetu!
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Is this true!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  I dont believe if the Tanzania peoples defence force (TPDF) has failed to do their responsiblities and handover the assignment to Tanzania Police Force (FFU)
  NOW:
  1. Who is going to take care of our National presdential and members of parliament elections which will takeoff on october early this year.
  2. Who is going to take care of the Mosques at mwembechai and..........
  I am worried wether this was derived and agreed with the national interests.
   
 4. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Hawa ladies wako kikazi zaidi 2010 kama FL1.
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Mi navyoelewa hiyo ilikuwa ni party ya kiaskari zaidi,maana wakitoka hapo wanaenda kuungana na JWTZ,na hawatavaa green jungle hizo za FFU,ila watavaa za JWTZ,hapo ndo huwa wanaagwa rasmi na amiri jeshi mkuu.I luv women in green jungle as my wife is...
   
 6. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Technician,si kweli kuwa TPDF,ndo huwa wanaenda operation za kijeshi pekee,Operation zote za kijeshi zinabeba wanajeshi wa majeshi yote(wale wote unaowaona wakicheza gwaride la uhuru,ikiwemo magereza,polisi na TPDF),Tofauti ni kwamba wote wanavaa uniform za aina moja,na hiyo iko ndani ya taratibu za kijeshi,na sio kwamba TPDF,wameshindwa kazi au wako wachache.Mfano ile operation ya Comoro ilibeba FFU wengi tu.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  sasa hata Waziri au Naibu wake wasiwepo?
   
 8. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Unachokiongea ni kweli mkuu,lakini angalia hata askari waliopo hapo,mwanaume mwenye cheo kikubwa hapo ni assistance commissioner wa polisi.Vyeo vya polisi huanzia,IGP wanafuatia CP alafu DCP then SACP ndo anakuja huyu ACP ambaye yupo hapo.Unaweza kuona hiyo sherehe haikuwa na uzito mkubwa sana wa kitaifa,na sitawaelewa iwapo haitafanyika nyingine rasmi.Siwezi kumlaumu waziri sababu anapokuwa waziri kwenye issue za kijeshi,basi atakuwepo IGP au mmoja wa ma CP.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani huko Darfur wanahitajika wanajeshi peke yao? Mbona hata mapolisi wanahitajika. Hizi ni fani mbili tofauti na tusizichanganye. Polisi si mwanajeshi hata kama tunaita jeshi la polisi.

  Amandla........
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nadhani mama Zuhura ni SACP..
   
 11. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Yah,nilikuwa nasema mwanaume mwenye cheo cha juu,pia tunaweza sema ilikuwa ya wanawake zaidi kuwaaga wenzao
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  naona wengi ni maofisa tu.. kuanzia warakibu wasaidizi (naona ndio wengi hapo) na kwenda juu.
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  All the best
   
 14. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  si unajua tena mapc wanabaniwa.
   
 15. R

  Renegade JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Kila la heri dada zetu.
   
 16. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Aluta kontinuaaaaa!
  Machooo mbelee, tembeaaaaaaaa!
   
 17. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikila peke yangu, ati baba mchoyo..............................................nikiachia watoto nao wajichane peke yao, ati baba hajali kula na wanawe!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Halafu wote ni wali kwa nazi mwanawane! Nakwambieni Dafur kuzuri
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Mar 31, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Aah vaa miwani. Yupo hapo anawaaga pia! Humuoni?
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi baada ya kukabidhiwa hiyo bendera wanaweza kukabidhiwa nyingine tena? Si ndio imeishatoka? Mimi naona wakuu waliona kuwa hapa hapana maslahi.

  Amandla.........
   
Loading...