Kwa shida nnazopata am sure ntakizibua nibebe ela....
Hapo nilipo weka Alama nyekundu achana na marafiki wa mwisho wa mwezi
kama nyumbani kwenye familia yenu una wazazi wawili i mean Baba na Mama ndio wa kuwapa msaada lakini ndugu na marafiki wengine simamisha kwanz akwa muda jiangalie wewe
mwenyewe huo mshara wako wa mwezi unakutosha kukidhi mahitaji yako? Huna nuksi wala nini una matatizo ya kupenda kutowa misaada ovyo ovyo bila ya mpango na una tabia ya
kupenda kuwakopeha watu kisha hao unaowakopesha hawakulpi hela zako jichunge na
marafiki wa mwisho wa mwezi utafanikiwa. Ingawa hujatueleza una miaka mingapi? Una mpenzi au mchumba? ukifuata ushauri wangu utaweza kufankiwa asante.
Huyu ni kama yule Kassim wa mataumizi walimuimba Ochestra Mlimani Park Sikinde ngoma ya Ukae miaka 1980 asipotumia akili zake atakuwa kila siku hana pesa kazi kwake.
Mkuu ni vizuri kuwa unajua kiini cha tatizo kama ulivyoainisha hapo juu. Unachotakiwa kufanya weka kiwango maalum cha kuwapa wazazi kwa mwezi na wao wajue hivyo pia punguza hizo ahadi za kuwapa watu pesa. Kumbuka wanaomba zakwako lkn zao wanafanyia mambo ya maana na yenye kuonekana siku ukija kugundua utaumia. Sisemi usiwasaidie toa msaada pale inapolazimu tu. Kama ulivyoshauriwa na wadau wengine fungua account humo jiwekee kiwango cha kuweka kila mwezi yaani upunguze mshahara wako kwa kama laki 2 au kama unapokea 1mil basi upunguze mshahara kwa laki 4. Weka bank hizo lk 4 na zinazobaki panga matumizi yako kwa mwezi. Yaani iwe kana kwamba mshahara wako umeshuka kwa kiasi hicho na lazima uishi kwa mshahara.
Ukifanya hivi itakusaidia sana kujiwekea akiba na pengine waweza fanya mambo makubwa. Yaani hicho kiwango utachokipunguza kwenye mshahara fanya kukisahau kabisa na ujitune kana kwamba wewe ni wa kima flani cha mshahra. Kitu kingine kinachomaliza pesa ni michango ya harusi, kipaimara, komnio n.k usitoe au punguza kiwango cha kuchangia kwani si lazima kila mwezi uende kwenye sherehe. Pombe na starehe zingine zinazofanana na hizoo kama unafanya basi punguza .
Mkuu ukifanya hayo na mengine waweza ona mafanikio .
Nimekumbuka chuo i had this gal aliwah kuniambia kwa namna nnavyojiaxhia na maisha km cntampata gal mwenye akil kuni-control i wil die poor....now i see coz she knew me for almost 2 yrs means she knows alot.....
Alikuja akigoma mara nying mm kuwasaidia watu...she said like bado haujawa na uwezo wa kutoa msaada..i thout ana roho mbaya bt now i c wat she meant
Kwanza, hii inategemea na umri wako, muda uliokuwa kazini na mengine.
Wakati naanza kazi nilikuwa na tatizo kama lako, mbaya zaidi mie kazini nilikuwa napata kila kitu, kuanzia chakula hadi vocha ya simu, na bia juu free.
Lakini nilikuwa najikuta hadi nimeomba advance ya mshahara kwa shida zisizo zangu kwa kama miezi 7 ya mwanzo. Kuna siku dada mmoja alisema mno tabia ya advance, yale maneno yaliniingia, nikaapa kutochukua.
Sasa ikabaki mwisho wa mwezi, uwiii nakutana na mambo meengi, hela yote kwishney. Nikahamia sehemu tofauti, majukumu yangu binafsi yakaanza kuongezeka maana sehemu nilohamia hakukuwa na huduma kama za awali, basi nikaanza kujipanga taratibu na kuanza kuwa mchoyo a bit.
Baada ya muda nikaona nafanya kazi, lakini nipo nipo tu. Nikaanza kujipangia malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Labda unapanga, baada ya miaka miwili nataka niwe na hiki, unapanga kulingana na kipato chako. Una unajaribu kujistretch to your limits, ili hata usipofika ulipopanga uwe umefika mahali fulani.
Kama wewe naweza kupangia hiki, kabla mwaka haujaisha, walau uwe na kiwanja, hata kama itakubidi kulipa taratibu. Najua kwa logistic za Dar baadhi huanza na magari, hii itategemea sana kipato chako, usije ukanunua halafu pesa ya kulihudumia daily likakwamisha mambo yako mengine.
Kama bado unaishi kwenu, jipe azimio la kuhama na kupanga chumba chako, nunua vitu vya ndani unavyohitaji, kidogo kidogo unaanza kujifunza nidhamu ya pesa.
Kutunza pesa ni kitu unajifunza, hakiji tu, unajifunza taratibu. Ina maana gani wewe kufanya kazi halafu maisha yako yako vile vile kila siku? Elimu yako itakuwa haijakukomboa. Kama umeshagundua hili, jua uko kwenye direction sahihi kabisa.
Daaahh magombe junior angekua na mke au dada au hata rafiki kama wewe... wenda huu uzi usingekuwepo hapa!!!
Heshima kwako Kongosho !!! Wazo zuri...
Mkuu magombe junior , mara yako ya mwisho kutoa 'zaka' au fungu la kumi ni Lini? Fanya hivo nawe utaona matokeo yake, maana hiyo ndiyo silaha kuu!
If we keep other things constant, huyo ndo mwanamke wa kuoa!!! Kama uko nae karib changamkia fursa!!
Tatizo huna malengo anza kuweka malengo kufikiria kipi unataka kufanya ktk mshahara na make sure hiyo hela haiguswi usiendekeze nafsi utakufa maskini
Malengo yapo ispokua namna ya kuyatimiza ndo inakua shida kidgo...ila kwa ushaur ambao nishaupata umu nategemea a great improvement!!
Hayo ndio maneno mkuu!! Na sisi kama wana jf tunaiman sana wewe ni msom na ni mtu mzima fanya ya maana mkuu!!!
Na kama mdau alivosema hapo juu... jiyahidi kupitia kule jikwaa la biashara na ujasiriamali, uzi wako binafsi umenisaidia naiman na wewe pia umepata kitu!!
Mimi ..wewe...na yule sote tusikate tamaa, tuweke akiba na tuwe na malengo chanya kwa maisha na vizazi vyetu vijavyo!!
Ila pole sana... kila la kheri na ufanikiwe katika kipindi hiki cha mpito!!!