I do solemn believe in the greatness of this Nation..

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,654
Kuna hili swali ambalo kila wakati nimekuwa nikijiuliza na kukosa usingizi. Ni nini tunahitaji kama taifa? Kwanini tuko pamoja kama Taifa? Mwelekeo wetu ni upi? Je ni kutafuta mkate wetu wa kila siku tu na kupata sehemu ya kuegemeza vichwa vyetu tusinyeshewe na mvua pamoja na kupigwa na jua? Je ni nini kilituunganisha kama Taifa? Ni Wapi tunataka kufika?

Ni ukweli usiopingika sisi kama taifa ni lazima tuwe na mwelekeo. Hatujawa taifa kusudi tunywe na kula na kusherekea kuna kitu kikubwa zaidi ya hicho. Kuna nguvu kubwa zaidi ya hiyo ambayo mungu ameiweka ndani ya taifa hili ambayo ni lazima izaliwe.

Kama tukifikiria tumekuwa taifa kusudi tule, tunywe na kufurahi maisha yetu hayatokuwa na faida.
Kama mawimbi yanavyojikusanya na kuvamia nchi kavu ndivyo nchi yetu inatakiwa kuwa. Kuna nguvu iliyo ndani yetu ambayo ni lazima ichipue kama mche utokavyo kwenye mbegu. Na hii nguvu ni lazima ikue hivyo.

Kwahiyo taifa hili ni lazima liungane na tuwe na lengo moja, tutumie nguvu zetu na akili zetu kulijenga.
Nguvu na mamlaka hukusanywa kidogo kidogo kwa juhudi na maarifa ya pamoja.
Hatujawa taifa kusudi tutafute mkate tu kuna jambo kubwa zaidi ya hilo. We must build our strength.. I do believe in the greatness of this Nation. We must prepare ourselves. We must have this courage..


''Wakati mwingine katika maisha unapambana na hali ngumu. Unatumia akili na nguvu zako zote. Kwenye msitu mnene unatafuta njia, na unapofanikiwa kuona jua kutoka kwenye msitu wa kiza kinene unakumbana na bahari. Unakaa chini na kuchoka safari yako bado haujafika pengine unaweza kunyanyuka na kuangalia bahari na kusema wewe kikwazo lazima nikushinde lazima nifike ninapotaka kwenda lazima nikushinde. Jamii nyingi zilishindana na vikwazo vingi lakini with the boldness of mind and courage walishinda.
Baadae ya dunia hii haiko kwa wale wanaokata tamaa bali kwa wale wanao persevere na kushinda vikwazo kufikia malengo yao.''

Huu ni ukweli ambao taifa hili lazima liukumbatie. Ni lazima tujue ni wapi tunataka tufike na tuanze safari sasa.
Hakuna mkato kwenye safari hii ambayo inahitaji kujitolea kwa dhati ili kuona taifa hili likikusanya nguvu na kupata mwelekeo. Hii nguvu ni lazima ilale kwenye ushupavu wa watu wa taifa hili na utayari wao kuona taifa hili likichukua nafasi katika dunia. But all these things need a bold and determined leadership.

Uongozi ambao unataka kuona mapinduzi ya kweli kuanzia ya kifikra, kiroho hadi ya kimali bila vyote hivyo taifa letu halitoweza kusonga mbele. Hii nguvu lazima tuijenge kwa watu wetu kwasababu ni nguvu muhimu katika kuleta mabadiliko ya taifa hili. Hatutaweza kufanikiwa kujenga taifa hili katika udhaifu.

Hii kiu ya watu wetu kutaka kuona mabadiliko, kutaka kuona taifa hili likichukua nafasi yake katika dunia ni lazima iwe driving force ya kila mwananchi. Kwasababu naamini tuna hii nguvu. Hii nguvu iko mikononi mwetu na ni lazima tubadili mindset zetu. Umoja wa taifa hili ni muhimu ili kufanikisha hili jambo ambalo ni muhimu kwa heshima yetu kama taifa.

Kwahiyo nguvu kubwa ambayo kiongozi yeyote makini anayetaka kuona taifa hili likinyanyuka ni kwenye umoja wa watu wake kwasababu ni muhimu sisi kama taifa kuwa na mwelekeo mmoja wa wapi tunataka kufika. Ni lazima kuwepo na kujitolea huku pasipo kujitolea huku hakuna maendeleo tutayopata.


 
Umesema vema mkuu lakini umesahau unawaambia kina nani, wale wanasema piga au wale wanaoambiwa wapigwe? kwa maana hawa siyo wamoja!
 
Umesema vema mkuu lakini umesahau unawaambia kina nani, wale wanasema piga au wale wanaoambiwa wapigwe? kwa maana hawa siyo wamoja!

Tatatizo liko hapo..nakubaliana na wewe ndio maana nasema tunahitaji mabadiliko kwa viongozi wetu jinsi wanavyochukulia raia..kwasababu bila ushirikiano wa raia kwa taifa hili maendeleo ni ndoto.
 
Back
Top Bottom