Kama alivyosema mwenzetu mmoja hapo juu, ukiangalia kwa chini ya hicho kibox cha kulogin utaona wameandika 'I cant access my account'. Bofya hapo, itakuja page inayokutaka ku tick your problem. Isikuchanganye, we piga Next. Kuna maswali mawili utatakiwa kujibu ktk pages zinazofuata. Ukiyajibu kwa usahihi itafika pahali unatakiwa ku change pasword. Nakushauri uweke pasword ndefu kidogo at least 8-10 digits. Nimeona pasword fupi imekuwa ikisumbua sana kwenye account za yahoo.
Note: Unaweza ukafika mwisho ukisubmit ikaleta error. Bofya try again. Na pia inaweza ikakurudisha mwanzo kabisa ulipoanzia, sio issue, ingiza cupture itakayoonekana kwenya kibox hapo chini then sign ni. Lkn inaweza kukataa tena, inabidi uendelee kujaribu tena na tena itafunguka tu.
Ikifanikiwa kufunguka kama unatumia computer/simu mwenyewe nakushauri usi sign out.