I hold a degree in Education. I specialize in English and History but i can also teach Civics very well. Please contact me on 0769306968. Currently am in Geita town
Mkuu,watu wasikuzingue...binafsi nimependa kwa uthubutu wako...sio kila mtu anaweza andika japo sentensi mbili za kingereza hadharani,achana wa watu ambao kazi yao ni kukejeli binadamu wenzao,usiwajali sana maana wanashida hadi matakoni tena wengi wao hata kuelewa ulichoandika ni shida,wanajifariji kwa kuponda ponda wenye kila lifanywalo na binadamu wenzao. Achana nao mkuu wewe endelea kumuomba Mungu atakusaidia.
Binafsi naona kuna ugumu wakupata kazi kwa nyakati hizi ila nakushauri angalia namna yakujihusisha na kilimo na ufugaji mkuu...tena achana na kuzunguka na bahasha mjini,nenda kijijini au maeneo ambayo hayajachangamka....lima vitu vidogo vidogo nyakati ambazo sio za msimu mfano unaweza lima matikiti,maharage na n.k
Pambana,ishi kwa shida...acha wenzako wakae huko mjini wewe pambana na shamba,then anza kununua ardhi kidogo kidogo tu huko huko kijijini ( hakikisha unanunua ardhi isiyo na migogoro)anza kupanda miti kama mikaratusi na mingine mingine inayovumilia ukame( hali ya hewa inabadilika sana)...pia anzisha biashara itakayokuwa inakupa ela kidogo kidogo huku ukiendelea na kununua ardhi na kupanda miti mwaka mpaka mwaka bila kusahau kilimo cha maharage na vitu kama hivyo.....
Ndugu nakuambia baada ya miaka 13 utakuwa na hecta zaidi ya 10 ambazo ukiziuza utajenga shule yako na zaidi....
Maisha yapo kijijini ndugu yangu hasa kwa watu tusio na mtaji mkubwa au kuliotoka familia duni....
ZINGATIA:-ukienda kijijini usijifanye wa town,shiriki nao kwenye kila jambo jema,ongea kiswahili na ukiweza jifunze hadi salamu kwa kiluga chao
Pia achana na wasichana/ wanawake wa huko....chagua msichana mwenye malengo especially asiye mzawa wa huko(mfano unaweza date au kuoa mfanyakazi kama mwalimu,nesi n.k)
Usijihusishe na POMBE za kienyeji,zitakupotezea malengo sana,
Jiepushe na migogoro maana watu wa vijijini wana roho ngumu sana,mtu hakawii kukukata kichwa au kiganja kisa unamsalimia salimia mke wake mara kwa mara au kwasababu za kijinga jinga tu.
Zaidi jifunze kupuuzia.
Mungu akubariki sana mkuu......karibu kijijini.