I am 42 yeas old and finished


Basi Utakuwa na Matatizo ya Akili kwa maana huwezi kujieleza kwa Kiswahili na pia hicho Kiingereza unachokimbilia pia hukiwezi, kwa maana umeandika kiingereza kibovu sana!

 
Tafuta ushauri wa kisaikolojia. Hayo unayopitia wapo wengi wenye matatizo zaidi.
As long as umegundua you need a change, you should change namna unavyofikiri.
Forget the past, angalia unachotaka kuachieve, then tafuta ushauri kwa unaowaamini.
Better late than never!
 
A proffesional male ndio kazi gani? Ya kutia mimba?

Learn from Le Mutuz na Babu wa Loliondo, sio mwisho wa dunia
 
tulia jipange,,badilisha lifestyle,,marafiki wabaya, tegemezi tupa kule,,be yourself,,,omba mungu,,,,,tabia za kupiga watu ofa achana nazo,,,wanawake wengi acha,,wanarudisha sana nyuma,,maanake wanakula vyako vyao wanawekeza,,,,take care
 
wajameni thithi wingine tumithoma mwisho darasa la tatu hivyo tumieni kiswahili nasi tuelewe!
 
Yaani best umenigusa na comment yako hii
nahisi itamfundisha huyu mtoa mada
 
eti this world is not fair....ulijisahau na kamaisha flani kalikokupitia...wewe ndo hukuwa fair na dunia...

Lipa ulichokipanda duniani mkuu.. mbinguni kuhesabiwa tu sikuhizi.
 
NI USHAURI TU BESTITO WAWEZA KUUCHUKUA NA KUTENDEA KAZI KAMA UTAPENDA

Bestito yawezekana unapita katika magumu na unaona hakuna njia tena na unakata tamaa.
Umefika mahali na unasema siwezi kupata kazi tena, hii kazi siwezi tena, hawa watoto wamenishinda, siwezi kujenga, hii biashara imekufa, siwezi kuwa na biashara tena, n.k…….


Ninataka nikuambie ya kwamba IPO NJIA. Inaweza isiwe rahisi na inaweza iwe ndefu. Hata kama panaonekanika kama hakuna njia, kwa Mungu kuna njia wakati wote. Na kama Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, Utakuwa na ubunifu wote ulimwenguni upo ndani yake, na kwa kuwa yupo ndani yako, ubunifu utaupata. Mungu ana uwezo wa kukupa fikra ambazo hujawahi kuwa nazo na kukuonyesha njia ya kufanya vitu ulivyofikiri hutakaa uweze kufanya.


Badala ya kukumbatia magumu, inatubidi kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na tujue ya kwamba yeye yupo kwa ajili yetu na nguvu yake ipo kazini kwa ajili yetu. Tufike mahali tuone ya kwamba iwepo njia au isiwepo Yesu ndiye njia yangu na nitaipata njia ya kutokea tuu.


Mungu ametuahidi katika Isaya 43:19 akisema "tazama, nitatenda tendo jipya; sasa litachipuka, je! Hamtalijua sasa? NITAFANYA NJIA HATA JANGWANI, na MITO YA MAJI NYIKANI". Katika injili ya yohana 14:16 Bwana Yesu alisema "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima". Yeye ndiye njia, atakusaidia kuiona njia pale inapoonekana kama hakuna njia. Pia katika Wakorinto wa kwanza 10:13 tunafundishwa ya kwamba "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya mwanadamu; ila Mungu ni mwaaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili". Hivyo rafiki usikate tamaa wala kuvunjika moyo kuona miaka imesonga sana wala huoni ulichofanya Mwamini Mungu kuwa anaweza naye atafanya njia na vilevile jipe tumaini kuwa ipo siku utatoka hapo ulipo na vilevile fanya juhudi na bidii katika kila jambo ufanyalo MSHIRIKISHE MUNGU usipende kufanya pekee na kumuweka Mungu mbali fanya kila kitu kwa uwezo wa Mungu na USIWE MVIVU AU MLEGEVU au mwenye KUCHAGUA AINA YA KAZI au MWENYE KUCHAGUA kitu BALI fanya lolote la halali mbele yako kwa utukufu wa MUNGU.

CC: muuza ubuyu , Ntuzu
Passion Lady
 
Last edited by a moderator:
eti this world is not fair....ulijisahau na kamaisha flani kalikokupitia...wewe ndo hukuwa fair na dunia...

Lipa ulichokipanda duniani mkuu.. mbinguni kuhesabiwa tu sikuhizi.

Watu mna makavu!!? badala ya kumfariji mnazidi kumshusha kaburini.Anahitaji faraja.Lets give him a second chance...
 
Watu mna makavu!!? badala ya kumfariji mnazidi kumshusha kaburini.Anahitaji faraja.Lets give him a second chance...

ni kuambiana tu ukweli..kumfanyia unafki si vizuri...
second chance na 40's? arudi kwao tu akapumzike...
na ukute kachanganyikiwa sababu hata kwao alihasi...sahizi anajiona kabaki pekeyake hana kwa kukimbilia...
 

all is not lost mkuu,

Keep your head up, explore options, start humble utafanikiwa, njia ileile uliyoingilia mara ya kwanza inaweza kukusaidia

Hakuna kifo kibaya kama cha kukata tamaa, ni kibaya kuliko kufariki dunia...

You were born to toil and this is the way to go... As long as you define your priorities well, kwa sasa sidhani kama mke na watoto itakua ndio priority yako, i think you should focus on sustaining you life before anything else

Hakuna kisichowezekana chini ya jua
 
you are what??? Finished doing what ???? You sound like you have a programmed calender!!! This absolutely wrong! You dont just give up! Never say never! You dont surrender ......! Men ich kweli nenda mvomero ukalime watermelon, ufuta nk
 
Nakuvutia taswira naona ulikua mtu fulani matawi sana ndio nyie mlikua mnavaa soksi na kandambili. Ila hujachelewa Mungu hashindwi na jambo, mrudie Mungu wako fanya toba atakusamehe na atafanya njia umri wako unaruhusu .

umenichekesha kweli, nina rafiki zangu wabeba mabox hao wakishukaga bongo ndio pozi zao sandals kwa sox kama maparoko wa kikatoliki kutoka ulaya.
 
ni kuambiana tu ukweli..kumfanyia unafki si vizuri...
second chance na 40's? arudi kwao tu akapumzike...
na ukute kachanganyikiwa sababu hata kwao alihasi...sahizi anajiona kabaki pekeyake hana kwa kukimbilia...

Mhhh.Yanaweza kukukuta hata wewe.Never judge anyone.Huyo ni kweli kachanganyikiwa kwa jinsi alivyoandika but mpaka kaandika hiyo thread anaonesha anahitaji msaada.Ni jukumu letu kumtia moyo.Kila mtu ana eneo lake katika maisha alilochemsha lakini duniani tunainuana kwa kupeana faraja.Umtendee mwenzio lile upendalo utendewe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…