Hydrogen gas

Hydrogen gas

mjarrab

Senior Member
Joined
Nov 13, 2015
Posts
108
Reaction score
55
Habari wakuu!

Naomba msaada wa kitaalamu kuhusu gesi ya hydrogen,inafaa kwa matumizi ya kupikia, nimegundua njia rahisi ya upatikanaji wake,naomba kwa enaejua anijuze.

Naomba asitumie maneno ya kitaalamu sana kwani mimi elimu yangu ni ya kawaida sana, maelezo yawe ya kiswahili na mepesi kueleweka.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Habari wakuu!naomba msaada wa kitaalamu kuhusu gesi ya hydrogen,inafaa kwa matumizi ya kupikia,nimegundua njia rahisi ya upatikanaji wake,naomba kwa enaejua anijuze,naomba asitumie maneno ya kitaalamu sana kwani mimi elimu yangu ni ya kawaida sana,maelezo yawe ya kiswahili na mepesi kueleweka,natanguliza shukrani zangu kwenu

Wewe ni muongo na uko hapa kwa ajili ya kukejeli watu, watu kama nyie mko wengi sana hapa Bongo, huwa mkijifunza kitu mnataka na kupima wengine kama nawo wanajua kama ninyi sasa sijui unapata faida gani, kama wewe una ujuzi kuhusu gesi ya hydrogen njoo na uwapatie wengine ujuzi wako na siyo kuja kwa njia ya kujifanya haujui ili uweze kukebehi watu hilo halitakusadia wewe wala wengine wote wasio na uelewa, dhumuni kuu la Elimu na kuelimishana na siyo kupimana!

Mtu asiye na uelewa na mwenye Elimu ndogo hawezi kuuliza swali kama hilo kwanza umejuaje hata kama Hydrogen inapatika kwa urahisi kama wewe hauna uelewa?

Acha kupotezeana muda jikite zaidi kwenye kujenga jamii na siyo kuikebehi, tumia Elimu yako kwa manufaa ya wote!
 
bahati mbaya sana!ndugu kama huwezi kutoa msaada ni bora uikae kimya!kuliko kuongea vitu visivyo na msingi,kugundua jambo si lazima uwe mtaalamu,kama unamsaada wa hilo toa!usikejeli waatu!
 
Mhh kwa staili hii tutafika kweli:shock:
 
kwa anaye jua tafadhali!inaweza kuwa msaada na ukombozi kwa walala hoi!
 
Kama hunautaalamu wa mambo ya gas ulijuaje kuwa hiyo ni gas ya hydrogen,acha kutuzingua!
 
sasa ndugu kama swala la kujua hydrogen hakumaanishi kwamba mimi ni mtaalamu,nacho omba kutoka kwenu ni kutaka kujua kwamba gesi hiyo inafaa kwa kupikia au la?sasa haya mambo ya kujua au kuto kujua ya nini?gesi ndiyo nimesha igundua naomba kujua uasalama wake inaafaa au haifai kwa matumizi!ni hilo tu wakuu,msiwe na jazba tuelimishane
 
tuelezee njia rahisi uliyoitumia kupata Hydrogen.Hiyo gas inaweza kuendesha mitambo.Na kukatia vitu
 
Habari wakuu!

Naomba msaada wa kitaalamu kuhusu gesi ya hydrogen,inafaa kwa matumizi ya kupikia, nimegundua njia rahisi ya upatikanaji wake,naomba kwa enaejua anijuze.

Naomba asitumie maneno ya kitaalamu sana kwani mimi elimu yangu ni ya kawaida sana, maelezo yawe ya kiswahili na mepesi kueleweka.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Ndugu hiyo gas ni hatari wala usijaribu
kuangaika nayo inaweza kukuletea madhari,
labda kama una kiwanda cha kutengeneza milipuko
inaweza kukufaa.
 
nashukuru mkuu,kwa maelezo yako kwamba gesi hiyo inaweza kuendesha mitambo na kukatia vitu,ila hujanieleza kama inafaa kwa mtumizi ya kupikia!kuhusu kutoa elimu hii tufanye subira,kwani inaweza kuharibu biashara za watu,ila naomba kupata elimu zaidi kuhusiana na gesi hii
 
Ndugu hiyo gas ni hatari wala usijaribu
kuangaika nayo inaweza kukuletea madhari,
labda kama una kiwanda cha kutengeneza milipuko
inaweza kukufaa.

Nashukuru kwa tahadhari hiyo!umesema niachane nayo kabisa,kwa hiyo inamaana haifai kabisa kwa matumizi ya kawaida?
 
nashukuru mkuu,kwa maelezo yako kwamba gesi hiyo inaweza kuendesha mitambo na kukatia vitu,ila hujanieleza kama inafaa kwa mtumizi ya kupikia!kuhusu kutoa elimu hii tufanye subira,kwani inaweza kuharibu biashara za watu,ila naomba kupata elimu zaidi kuhusiana na gesi hii

Haifai kwa kupikia mkuu...jibu hilo lakutosha??...ni gesi hatari ina ptoperty za kulipuka
 
Haifai kwa kupikia mkuu...jibu hilo lakutosha??...ni gesi hatari ina ptoperty za kulipuka

nashukuru kwa tahadhari hiyo mkuu!na kwa wale waliokuwa wakitaka maelezo ya jinsi ya upatikanaji wake waniwie radhi kutokana na hatari ya gesi hiyo sitoweza kuitoa tena!asante sana mkuu.
 
Naomba jibu la swali hili, kama umesema wewe sio expert, je umejuaje kua hiyo ni hydrogen?
Kama unajua ni hydrogen basi lazima utakua unajua na properties zake pia, umekuja hapa kutupima akili.

Haya tukirudi kwenye mada, natoa jibu kusaidia wengine wanaotaka kujifunza ila sio wewe coz unatupima akili.
Hydrogen ina-burn na inaweza kutumika kwenye kupika, lakini kuna sababu za msingi za kwa nini usiitumie kwenye upishi.

Kwanza ni usalama wake, hydrogen haina harufu kwa hiyo in case ime-leak chumba kizima hutojua, utawasha flame nyumba italipuka.

Pili, ukiwa unapika kwa kutumia gas mara zote unahitaji kuona flame ili ufanye regulation ya amount of heat unayotaka, hydrogen ikiwa inaungua inatoa white flame, so hutoweza kuona vizuri we utashangaa tu heat inaongezeka, hutojua kama umeweka moto mwingi au la, unaweza zidisha kumbe flame imejaa sufuria zima kwa hiyo its a waste.

Hizo sababu zinatosha kabisa kukufanya usijaribu kuichezea kabisa.
 
nashukuru mkuu!
 
Nilizani wana JF hawataki kukutendea haki uzi wako wala kukupa idea ya wanayo fahamu kuhusu hiyo gas....Kumbe wewe mwenyewe una ubinafsi unaulizwa umewezaje kujua kama hiyo ni H hutaki kutoa somo....Sijui unahisi ukitoa somo tuta tajirika sio???

Watu kama nyie ni wakuupuzwa maana hamna msaada kwenye jamii...Unataka kuexplore idea za watu lakini wewe hutaki kutoa idea zako....Shame on You
 
الصلواة والسلام عليك يارسول الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ُ ( سیار زٌھب )
 
Nilizani wana JF hawataki kukutendea haki uzi wako wala kukupa idea ya wanayo fahamu kuhusu hiyo gas....Kumbe wewe mwenyewe una ubinafsi unaulizwa umewezaje kujua kama hiyo ni H hutaki kutoa somo....Sijui unahisi ukitoa somo tuta tajirika sio???

Watu kama nyie ni wakuupuzwa maana hamna msaada kwenye jamii...Unataka kuexplore idea za watu lakini wewe hutaki kutoa idea zako....Shame on You

nashukuru nimetendewa haki na wana jf,kama ulivyo ona wataalam wmeonyesha hatari ya gas hiyo!kwa hiyo lazima kuchukua tahadhari,kwa hiyo siwezi kutoa elimu hiyo iwe sababu ya watu kudhurika!wala si ubinafsi!na sikutaka kuitumia bila kupata ushauri wa wataalam,na kama ulivyoona wataalam wameonya juu ya matumizi yake!kwa hilo niwiye radhi ndugu!
 
Watu wengine bana waajabu kweli, kwani huwezi kutoa elimu kisha ukatoa tahadhari! Ndo maana wwenzetu wameendelea ukiingia internet utakutana na kila kitu watakachofanya ni kukupa tahadhari tuu..
 
Back
Top Bottom