Huyu Trafic hatufai!!

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Wana Jf naleta hii kutoka Arusha, kuna Askari wa barabarani (trafic) mitaa ya mianzini anasimamisha kila hiece (daladala) na na kijana mmoja anamchukulia 1000 kwa kila gari, akisha simamisha wala yeye hafati gari ila kijana mmoja anafahamika kama "Sheikh" ndiye anayefuata gari na kuchukua hela, nikamuuliza dereva mbona unatoa hela na trafic hajakufuata akasema yeye haji ila kijana wake ndo anakuja. sasa ukipiga hesabu ya kila daladala anakula 1000 na usipotoa anakuwekea kinyongo huyu kweli anatufaa???
 
Wenye daladala wamuwekee mtego huyo kijana wake, akikamatwa huyo kijana wake, akisha lambwa makofi na askari (wenye uadiliifu), yeye mwenyewe atataja hizo pesa anamkusanyia nani.

Rushwa, napendekeza Tanzania iweke sheria ya kuuwa tu, kwa anaetowa na anaepokea rushwa. Kama China. Hivi wabunge mnaoingia humu JF, kwa nini hamlipeleki hili kulitungia sheria bungeni? Rushwa = Kifo.
 
Yaani wanamwogopa jamaa (trafic ) mbaya kabisa, yaani mtu anakusimamisha then anaendelea na kazi zake halafu hakuna anayethubutu kutokutoa hela....
 
mwacheni, nani anyeishi kwa mshahara wake asimane hapa tumwone.
 
Back
Top Bottom