Huyu ticha atakuwa aliwazingua Wazaramo

Huyu ticha atakuwa aliwazingua Wazaramo

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,884
Reaction score
18,824
Nasoma soma historia ya Wazaramo. Nimekutana na hiki kisa.

Basi baada ya Vita Kuu ya Pili Serikali iliongeza kujenga skuli za vijijini katika sehemu kadha za Uzaramo.

Lakini sehemu nyingine migogoro ilitokea kati ya wazazi na walimu, kwa mfano Mwalimu Barnabas Mwinyiwaziri aliyekuwa akiendesha Skuli ya Mkamba mnamo 1948, alikamatwa na kuuawa shambani kwake na watu wasiojulikana.

Baadaye wenyeji wa Mkamba walipinga na kuikataa Skuli hiyo isiwemo katika nchi yao. Basi Skuli ile ikafungwa na majengo yake yakateketezwa.

Wenyeji wa Mkamba hawakupata skuli tena mpaka miaka hii ya karibuni baada ya nchi hii kujipatia uhuru, mnamo mwaka 1962.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom