Huyu shemeji

Huyu shemeji

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
8,266
Reaction score
22,055
Habari wana MMU.

Nina rafiki yangu wa karibu sana ambaye ni ME! sasa huyu jamaa ana mpenzi wake! wamedumu katika mapenzi takribani mwaka mmoja na nusu.

Nikiri penzi lao limekua na misukosuko mingi, mara zote mimi ndo niliekua nawaunganisha pale wanapotofautiana.

Kilichonileta hapa ni kwamba jamaa yangu ameachana na huyu dada kwa sababu ya tabia zake za michepuko!(tabia za jamaa) Ugomvi wa kipindi hiki ulikua mkubwa hadi nikashindwa kusuluhisha!

Sasa huyu shem(mpenzi wake jamaa) tulikua tunawasiliana mara moja moja pindi wakiwa na jamaa! Lakini tangia waachane amekua akipenda tuwasiliane sana, kiasi kwamba nisipomtafuta kidogo tu,mara nsipopokea simu yake ni matatizo.

Huu ukaribu naona unapitiliza mara vimeseji vya kunchokoza! Mara ananitumia picha zake pasipo kumuomba, na pia kuomba zangu.

kilichonifanya nije hapa leo kanitumia meseji hii
"nakupenda sana sana kuliko nafsi yangu"
Hii meseji imeniacha na maswali mengi, huu upendo ni upendo gani?

kumbuka kwamba ni mtu wa dini sana, nkajiuliza pengine anamaanisha huu upendo wa kawaida hata kwenye dini zetu tunafundishwa?
maswali ninayojiuliza; x- wake anajua tunavyochati? na kama akijua atachukuliaje? Binafsi sitaki kutengeneza uadui na rafiki yangu.

Wana jamvi nisaidieni, je nimwambie rafiki yangu au nikaushe?

Msaada wenu tafadhali
 
Kama haupo comfortable kuwa na mawasiliano nae... Katisha! After all umemfaham kupitia huyo jamaa...unless kama na wewe umeanza ku-develop kahisia fulani moyoni...
 
Ndugu si umesema hutaki matatizo? Ina maana hutaki kuwa na huyo msichana. Sasa unataka tukushauri uwe naye wakati moyo wako hautaki? Au sijakuelewa vizuri?
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Mpe pochi manyoya / kigegedo, ataacha kukusumbua!!! Hazikutoshi
 
Umepewa mtihani uzuri unafahamu njia ya kuufaulu ni ipi. Amua kufaulu au kufeli
 
Inawezekana anataka tu kumkomoa jamaa waluyeachana kwa kutembea na rafiki yake
 
nipe mm namba zake wewe achana nae mtagombana bure na mshikaji wako
 
nina mashaka kama wewe ni mwanaume au wa kiume.

mtafutie mwanaume.
 
Huna haja ya kumweleza jamaa yake, potezea hizo sms na usimtafute
 
huyo anataka kumkomoa jamaa tu na hana mapenz na wewe kuwa mwangalifu!!!"!
 
anakupenda "KULIKO NAFSI YAKE EEH?" Wacha muitwe mazombie!
 
Back
Top Bottom