Huyu rais wetu vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu rais wetu vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, May 10, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wakuu wanaJF,
  Salaamz,
  Najua tumeshasema sana kuhusiana na utendaji kazi mbaya wa rais wetu, lakini kwa mambo anayoendelea kufanya (pamoja na kusemwa sana) naanza kuhisi ana matatizo makubwa zaidi kuliko kupenda mali, kuongozwa na marafiki mafisadi wenza, poor analytical skills, lack of concentration, na yote ambayo watu wengi tumekuwa tunayahusisha na kuchemsha kwake. Nahisi ana maradhi makubwa zaidi ya kiakili na kisaikolojia (Mtanisamehe kama lugha ni kali sana).
  Wakati serikali inahangaika kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida kama malipo ya mishahara, JK kafanya mapumziko ya siku nne wakati wa sherehe za Muungano, huko Kempiski Zanzibar ambako naamini ikulu imelipa fedha kibao. Pia yeye pamoja na waziri mkuu wamekwenda msibani Njombe kuhudhuria mazishi ya Mama yake Mh. Bi Makinda na bado Mkulu huyo kaibuka na semina elekezi ya viongozi wa juu wa serikali kwa siku nne huko Dom.
  Mtazamo wangu ni kwamba mambo haya hayana uzito wa kupoteza fedha za walipa kodi kiasi hicho hasa katika hali ya ukata tulilyonayo. Matatizo ya utendaji wa Mawaziri, Katibu wakuu na wakurugenzi mbalimbali si kwa kuwa hawajui majukumu yao bali ni kwa sababu hakuna sauti ya kuwasisitiza na kuwaonesha njia inayotakiwa. TRA kama wanashindwa kukusanya mapato vizuri ni kwa sababu hata yeye JK haijulikani anafurahia uzembe wao au haupendi.
  Anayehitaji tiba au semina ni JK peke yake na anaweza kufanyiwa huduma hiyo akiwa nyumbani au ofisini kwake na si katika mahoteli.
  Kama nchi haina fedha za kutosha jambo jema ni kuepuka matumizi yasiyokuwa ya lazima ya kifahari na si kukopa na kuongeza matumizi yasiyokuwa na maana kama semina. Sijui hata JK huwa anatumia nini kufanya maamuzi!
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kipendacho roho...dawa, ndugu. JK miaka yake 5 ya mwanzo kafanya anasa sana+kuzururazura hovyo,kipindi cha uchaguzi uliopita alipungua sana kimwili coz hakuwa anafanya anasa,na shughuli nzima ya uchaguzi alisusiwa akabaki pekeyake..watu walijua atajifunza..lakiniwapi!! ni ngumu sana kuacha anasa,ngoja tuumie tena miaka hii 5..then tutafika tu. Sasa hivi utasikia yupo uturuki.
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Pipo acheni kuandika pumba!!!

  Semina ni muhimu kwa viongozi kama team lazima muwe na wakati wa pamoja hata kwenye mpira kuna mapumziko wachezaji wanatumia ku re-group.

  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, whats wrong with kuhudhuria mazishi?
   
 4. m

  mkulimamwema Senior Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba MUNGU atuepushe na balaa za watu kama hawa wajuao kutumia mali za umma bila hofu
   
 5. b

  baba koku JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hivi kuhudhuria mazishi ya mzazi wa spika kuna nongwa gani? Baadhi yetu tuna fitna za kitoto.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kaka Maundumula -
  kuwa mkweli na wewe! Hoja si umuhimu wa semina- suala zima liko katika matumizi ya rasilimali za nchi na kwa manufaa gani zinapotumika. Kuhudhuria mazishi ni uungwana hatukatai, lakini muhimu zaidi ni kupanga matumizi kwa kadiri hali inavyoruhusu. Usije nawe ukatafsirika kama mmoja wa wale wanaotetea matumizi yasiyo ya busara! Hapo umechemka!
   
 7. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sasa ndugu yangu Maundumulu mbona unahasira sana au una kajishea hapo nn? Achakusema wenzako wanaandika pumba wewe umeandika nn sasa? Ndomaana tz bado tutabaki nyuma kwasababu yawatu kama wewe.

  Nakubaliana na mawazo ya jamaa kwani hizo semina helekezi mpaka ziwakusanye wote sehemu moja? Tunashindwakubana matumizi kweli? Serikali haina pesa lkn bado wanaandaa mambo ya ajabu.
  Tutapambana kuelimishana mpaka kieleweke kwan nchi yetu inalasilimali nyingi ambazo zikisimamiwa vizuri hakuna raia ambaye atakufa kwa magonjwa kama malaria/kipindupindu/ wakati wa kujifungua wakina mama na watoto.

  MUNGU IBARIKI TZ NA WATU WOTE HASA WALE WABISHI KUELEWA NA KUBADILIKA KAMA HAWA VIONGOZI WETU.
   
 8. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nilitegemea alipokuwa anatembelea wizara malimbali alikuwa anatoa maelekezo ya nini wizara husika ifanye sikutegemea kungekuwepo tena semina elekezi, mwaka 2006 semina hizi zilifanyika Ngurudoto zaidi tulichokiona baada ya hapo ni kuibuka kwa ufisadi zaidi,umaskini kuongezeka,mfumuko wa bei kuongezeka,uchumi kudodora n.k sasa tutegemee nini baada ya semina hii?
  Pili mbona katika awamu zilizopita sikumbuki kuwahi kusikia semina kama hizi kufanyika(Nikumbusheni kama zilifanyika)? na lakini viongozi walikuwa walijituma zaidi.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  alitembelea wizarani na taaisis za serikali TUKAMSIFU SANA TUU! Inamaana haikutosha watu walewale amekaanao tena dodoma halafu hakuna la maana upuuuzi tuuu eeeti UONGO MWINGI UNAKUWA UKWELI (LIKE RICHMOND)
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu ASANTE SANA BANA KWA HILI WENGINE HAWALIONI HILI!
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hana kipaumbele ndio maana unaona kwenye shughuli kama ya msiba,kiserikali angeenda yeye ama waziri mkuu basi lakini hebu niambie ni gharama kiasi gani anatumiana waziri mkuu anatumia kwa ajili ya shughuli moja ni utovu wa heshima kwa watanzania wenye njaa

  Suala la kutumia hoteli za wageni kupumzikia nadhani halifai na kwenye katiba mpya tuweke kabisa ni wapi tujenge Ikulu ndogo Mbili au katika Jiji La Mwanza,Arusha,Kigoma au Mbeya,ili ijulikane kiongozi akitaka kupumzika ni wapi anapaswa kwenda pajengwe vizuri awekewe kila vikolombwezo kama maeneo ya michezo,bustani,mashamba hata na mifugo kuliko haya mabo ya hoteli hoeli gharama zinakuwa kubwa sana na inakuwa mzigo kw taifa
  Tangu nchi kupata uhuru huyu Raisi ndio Raisi mpenda anasa zaidi kuliko kufikiri jinsi ya kusaidia wananchi yake sidhani kama anaguswa na umaskini na tabu wananzoguswa wananchi wake yeye ni mtu anajipenda kuliko kawaida ametanguliza mbele matakwa yake na ya familia yake kuliko wananchi kwa kweli inauma ,ni mroho,mchoyo,na asiyeitakia nchii hii mema yuko radhi kuitumbukiza nchi kwenye ghasia ili mradi yeye ajineemeshe
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ama kweeeli nchi inaliwa................kweli sasa naaamini kuna WANANCHI na WENYE NCHI
   
 13. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna shida Kuhudhuria msiba lakini kama rais kazi yake kuwa ni kuzuia watu wasife kijinga kuliko kuhudhuria misiba. Tunashangaa sana tunapomwona raisi akiwa katika kila msiba na sio kuwa serious na issues ya mortality na zingine amabazo zinasababisha misiba mingi kila siku ambayo hawezi kuhudhuria yote. Ila anaweza kuzuia vifo hivyo vya kijinga. Hivyo ukiwa rais mwelevu unachangua iliyo bora.

  Pili laiti angekuwa busy kama kiongozi mwenzie hapo chini angalia work plan yake kwa siku asinge opata muda wa kwenda kufanya shop kwenye misiba


  All in a day's work

  By TOM NEWTON DUNN

  A DAY is a long time in politics, or so the saying goes - and that's certainly true for David Cameron.

  The Prime Minister was out of bed for 17 and a half hours yesterday. Here we give an insight into what kept him busy.

  5.30am: Wake up.

  5.45am: Start work on red boxes at No11 flat's kitchen table.

  7.30am: Breakfast with the kids.

  8.30am: Regular morning meeting with his closest No10 advisers on the day's main events.

  9am: Nation Security Council committee on Libya.

  9.45am: Interview with The Sun.

  10.30am: Meeting with military chiefs about Afghanistan.

  12pm: Meeting with Chancellor George Osborne.

  12.45pm: Lunch in No11 flat with eight-month-old daughter Florence.

  1pm: Meeting with the Deputy PM.

  2pm: Meeting with CEOs from top businesses.

  3pm: Strategy meeting on future policies.

  4pm: Second regular meeting of the day with his closest No10 advisers to review events.

  5pm: Meeting with three Cabinet ministers on trade and investment.

  6pm: Drinks reception with TV broadcasters.

  7pm: Bath children and put them to bed.

  8pm: Babysitting while wife Samantha is out.

  10.30pm: Watch Newsnight on BBC2.
  11pm: Bed.  Read more: David Cameron’s first year as Prime Minister | The Sun |News
   
 14. K

  Kamura JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JK akikaa kimya mnachonga ooh, Rais mpole jana kawatolea uvivu mawaziri na makatibu wakuu mnasema anatumia hela vibaya. Tz isigeuzwe jamhuri ya walalamishi, tukosoe na kutoa mbadala wa kutatua tatizo si kubwabwaja.
   
 15. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Nani kakwambia Serikali haina fedha? Ni mtumishi gani ajalipwa mshahara mpaka leo hii?

  Ukijibu haya nitachangia hoja yako,vinginevyo ni umbea ama uzushi wa mtaani usio na tija zaidi ya siasa za majitaka.Mambo ya ajabu haya Mpishi (Mkulo) haaminiwi ila mlaji (Zitto) anaaminiwa!!!!!!!!!!!!!!!.Hii kweli tanzania ya siasa mpaka msibani as if you will not die.
   
 16. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Hakuna anaebwabwaja hapa sote tuwe tunaangalia kotekote,Jk alipokuwa akizitembelea wizara mbalimbali hivi majuzi na kuongea na mawaziri husika haikutosha?mpaka akaandae semina elekezi"huo si ufujaji wa pesa za walipa kodi masikini(wananchi)?Nani anaebwabwaja Kama sio wewe!!.
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Jamani mwacheni naye apumzike japo kidogo kwni nchi ngumu sana kuiendesha.

  Pumzika Bro Kikwete usije fia kazini
   
 18. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hana matatizo unayodhania,he is a Freemason,fullstop.These guys are a different species in the way they think.
   
 19. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mimi ni mtumishi wa serikali, nilipata msharhara wa mwezi wa nne tarehe 7 may balada ya tarehe 28-30/April. Hii ni dalili kuwa serikali ilikuwa imeishiwa na kukopa. Kama unataka data zingine sema tukupe na siyo kukurupuka kama watu wa chama cha magamba.
   
 20. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ni mjinga tu (kama wewe) anayeamini kwamba hao mawaziri na makatibu wakuu watafanya walichoambiwa?? nyerere,mwinyi na mkapa walifanya 'semina elekezi' ngapi kwa cabinet zao? washamjua huyu mkulu ni kiazi tu so walienda kuhalalisha Per Diem zao tu!! Business As Usual!! Kama Gamba mmetoa lakini mbona bado mabwege tu?? aaaggghhhh!!!
   
Loading...