Sasa sijui mwizi huyu awekwe kundi gani!
Ni mtu mwenye huruma, au ni msomi, au mpumbavu au genius?
Embu wanaJF nisaidieni kumchambua mtu wa jinsi hii!
TRUE SCENE!...Imetokea!!
Nina jama yangu anayeishi na kufanya kazi Mbeya, ambaye kwa bahati mbaya aliibiwa simu yake katikati ya mwezi huu July 2009, akiwa kwenye Hiace!
Huyu jamaa, kabla ya hapo, alikuwa ametuma maombi ya kufanya Matriculation Exam Arusha University.
Katika hali isiyo ya kawaida, inaelekea mwizi wa simu yake siku moja aliweka chip iliyokuwa kwenye simu ya huyu ndugu yangu, na mara alipoweka alikutana na meseji iliyotumwa na Arusha University kuhusiana na tarehe ya Matriculation Exam!
Mwizi huyo aliamua kuiforward meseji hiyo kwenye namba mbalimbali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye hiyo line hiyo, na hatimaye ujumbe ukamfikia huyu ndugu yangu, ukieleza tarehe, mahali,eneo, na muda, ambapo ishu hiyo ingefanyika, ambapo ni jana(29/7/2009)!
Huyu jamaangu alisafiri kwenda Arusha na KWELI KABISA ilikuwa ndo tarehe ya Exam hiyo, na amefanya, na leo 30/7/2009 yuko kwenye basi akielekea Dar na hatimaye Mbeya!
Sasa sijui mwizi huyu awekwe kundi gani!
Ni mtu mwenye huruma, au ni msomi, au mpumbavu au genius?
Embu wanaJF nisaidieni kumchambua mtu wa jinsi hii!
Sasa sijui mwizi huyu awekwe kundi gani!
Anabaki kwenye kundi la wezi hatuna kundi lingine la kumweka,na pia kwa ushauri mwambie rafiki yako akablock line isiendelee tena kutumika.
Acha kushangaashangaa mwambie awajulishe watu wote waliokuwa na hiyo namba yake, next time huyo msomi mtasikilia kwingine mfano;Anabaki kwenye kundi la wezi hatuna kundi lingine la kumweka,na pia kwa ushauri mwambie rafiki yako akablock line isiendelee tena kutumika.
Wezi wa simu mara nyingi hufanya vitendo kama hivi vinavyoonekana vya kiubinadamu kwa vile humo kwenye simu hata hivyo kuna credit! Mara nyingi watu pia wamejua kuhusu ajali au vifo vya watu wao kutokana na ajali baada ya kupigiwa simu na wezi wa hizo simu.All in all tukumbuke kuwa wezi wa simu wengine ni watu kama wewe na mimi hawana alama kuonyesha ni wezi au watu wabaya.
Hawana utu wala nini.Wangekuwa nao basi wasingeibia wenzao simu.
huyu ni mwizi lakini kama vile kulivyo na wivu mbaya na wivu mzuri[wa maendeleo]basi na huyu mwizi ni wa kimaendeleo,