Huyu ndugu ananikera kwa tabia hizi

kishamawe

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
267
360
Moja kwa moja kwenya mada tajwa, nina ndugu yangu kiumri ananizidi, ni kaka yangu ki ukoo, mtoto wa baba mkubwa, baba zetu wana changia baba (babu yetu) mmoja mama tofauti.

Anaishi nje kidogo ya mji ninapoishi mimi (mjini). Sasa imekuwa ni kawaida yake kufika kwangu, leo mara ya 3 anafika saa 3 usiku bila taarifa yoyote na anaondoka saa 12 asubuhi. Huyu ndugu kiukweli amekuwa ni kero kwangu, kwa vile amekuwa akifika hapa kwangu bila taarifa na vile vile hasemi shida inayomleta, siyo kwamba sipendi wageni kwangu.
 
Moja Kwa Moja kwenya mada tajwa , nina ndugu yangu kiumri ananizidi ni kàka yangu ki ukoo mtoto WA baba mkubwa , baba zetu Wana changia baba ( Babu yetu) mmoja mama tofauti. Anaishi nje kidogo ya mji ninapoishi mie ( mjini).Sasa imekuwa no kawaida yake kufika kwangu Leo mara ya 3 anafika saa 3 usiku bila taarifa yoyote na anaondoka saa 12 asubuhi , huyu ndugu kiukweli amekuwa ni kero kwangu Kwa vile amekuwa akifika hapa kwangu bila taarifa na vike vile hasemi shida inayomleta, sio kwamba sipendi wageni kwangu.

Akirudi tena mwambie hivi “bro hii tabia ya kuja Usiku bila taarifa inanikera”.

Kila jema

Aquila non capit muscas
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mwambie tu asije tena,atakasirika lakini zigo unakuwa umetua
 
Moja Kwa Moja kwenya mada tajwa , nina ndugu yangu kiumri ananizidi ni kàka yangu ki ukoo mtoto WA baba mkubwa, baba zetu Wana changia baba ( Babu yetu) mmoja mama tofauti.

Anaishi nje kidogo ya mji ninapoishi mie ( mjini). Sasa imekuwa ni kawaida yake kufika kwangu Leo mara ya 3 anafika saa 3 usiku bila taarifa yoyote na anaondoka saa 12 asubuhi, huyu ndugu kiukweli amekuwa ni kero kwangu Kwa vile amekuwa akifika hapa kwangu bila taarifa na vike vile hasemi shida inayomleta, sio kwamba sipendi wageni kwangu.
Kama unaona aibu kumwambia,akija msimfungulie.
 
Na mimi nasema mkubwa aendelee kuheshimiwa na utulize mshono huo pindi mwenye nyumba anapoingia kwenye himaya yake bila taarifa.. wewe si unaogopa kutoa maamuz ndan ya utawala wako..
 
Tatizo ni kwamba kwako kuna sehemu ya kulala. Ukitaka ndugu wasije kwako basi usiwe na sehemu ya ziada ya kupokea mtu
 
Fukuza asikuletee mazoea ya kipuuzi. Mi nlifukuza mama mkwe kwa tabia hii ya kuja kwangu bila taarifa ili hali anajua binti yake sikai nae sehemu moja. Lazim watu waheshimu nyumba za watu na si kuingia tu ovyo ovyo ka choo cha stendi

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Huyo hana adabu hata kidogo. Anatakiwa kujifunza kuwa unapokwenda kwa mtu ni vema kutoa taarifa mapema ili akuandalie mapokezi.

Ni uswahili na ushamba wa hali ya juu kwa miaka hii mtu kukurupuka tu na kutokea bila taarifa kwenye makazi ya mtu.
 
Wewe ni masikini tafuta pesa!
Ndugu yako anaweza kufika kwako muda wowote na hakuna sababu yoyote ya kukupa taarifa yoyote!
Jiulize inakuaje anapita nyumba zoooote huko na kuja kuingia kwako! Unadhani nyumba zingine hazioni?!
Kinachokusumbua wewe ni umasikini uliopelekea kujenga uchoyo na roho mbaya!
Kuna watu wanatamani kuwa na ndugu wa kuwathamini na kuwatembelea.
 
Unajua thamani ya undugu wewe, mwache alale hapo kwako tani yake,uoni kuwa anajivunia kuwa na ndugu mjini???
 
Back
Top Bottom