PostGE2025 Huyu ndiyo Msigwa, msemaji mkuu wa serikali ya CCM

PostGE2025 Huyu ndiyo Msigwa, msemaji mkuu wa serikali ya CCM

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,691
Reaction score
2,303
KI VIPI MSEMAJI WA SERIKALI GERSON MSIGWA NI FIELD JOURNALIST? AU FIELD MARSHALL JOURNALIST?

1764316118271.png
  • Kwa testimonies zake baada kumaliza sekondari alifanya biashara kuuza mahindi na duka Songea
  • Alianza mtangazaji trainee RTD Songea chini ya waandamizi watangazaji Chisunga Stephen na Seleman Muhogora
  • Alipatiwa mafunzo in-service training RTD Pugu road, TSJ, UDsm School of Journalism na mwaka jana alipata part-time MBA degree Strategic Planning St John's University Dodoma. Je, alisoma Results Based Management (RBM)?
  • Aliripoti ziara za Tunduru za Rais Mkapa, Mh Kinana katibu mkuu CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na waziri maliasili utalii Prof Jumanne Magembe
  • Alipewa kazi na Rais Magufuli kutangaza barabara za kimkakati kuunganisha mikoa kutoka Mtwara mpaka Mutukula Bukoba kutangzwa TBC tv redio
  • Rais Magufuli alimteua mkurugenzi ikulu habari mawasiliano
  • Ana digrii 2 atuanbie dissertations zake professionally na academically zilihusu nini?
Hizi ndizo sifa za kuwaambia wengine yuko bora Field Journalist pia Field Marshall Journalist?

Huku siyo kunajisi taaluma na maadili?
Angekuwa kama Dr Ayub Riyoba na Dr Engelbert Mkoko walianza kama reporters angevimba kichwa na kuzidi vijembe?
Hajui vyeo serikalini ni kupanda na kushuka?

1971 General Idd Amin alimpindua Rais wa Uganda Milton Obote akiwa Singapore kwenye mkutano The Commonwealth, akarudi Tanzania na Mwl Nyerere kama mkimbizi.

Mwaka 1977 nikaanza masomo Makerere University Kampala.Ni mwaka CCM ilizaliwa. Pia mwaka alizaliwa Gerson Msigwa.

Ni mwaka General Iddi Amin alijipa cheo Field Marshall Dr Idd Amin baada ya kulazimisha PhD Makerere University akiwa Chancellor

Kauli za Gerson Msigwa kutangaza mkutanoni Dar es Salaam kuwa yeye ni Field Journalist pia Field Marshal Journalist ni uwongo. Atupe ushuhuda wa data

Sikuzipenda kauli kujikweza. Hakuitendea haki tasnia habari wala wana habari. Huku ni kunajisi taaluma kujipa sifa hazipo duniani. Kama msemaji na katibu mkuu hakupaswa kupayuka. Ni kukiuka maadili ya tasnia na uongozi wa umma alikula viapo

General Idd Amin baada ya kujipa cheo Field Marshal aliapa kutwaa miji ya Kenya na Tanzania kuwa sehemu ya Uganda. 1977 akaanza kuupiga mabomu mji wa Mwanza kwa ndege za kijeshi na kisiwa cha Sanane, karibu Butimba TTC, sasa ni national park.

Huu ukawa mwanzo wa kuivamia Tanzania mkoa wa Kagera, zamani ziwa magharibi

Nilikuwa Makerere mwaka wa pili. Agosti 1978 mabomu yalipiga daraja mto Kagera na kiwanda cha sukari Minziro Misenyi. Oktoba 1978 Rais Nyerere alitangaza vita dhidi General Amin na majeshi yake.

Kulikuwa na wanafunzi Makerere (35) fani mbalimbali na chuo cha urubani Nakasongola Soroti (12)

Rais Amin akisema adui wa Ugabda ni Mwl Nyerere (labda kwa kuwapa hifadhi Waganda (mfano Obote, wahadhiri, wanafunzi kama Yoweri Museveni).

Alisema Watanzania waliopo Uganda wawe watulivu.

1977 East African Community ya kwanza ilivunjika. Kenya ilichukua mali nyingi 80% kama fedha (kulikuwa na sarafu moja), ndege East African Airways, treni, East African Railways nk

Tanzania ilifaidika bandari headquarters makao makuu ya jumuiya sasa AICC. Uganda ilifaidika na posta na simu headquarters na East African Development Bank

Makerere nilikuwa waziri serikali wanafunzi bweni Livingstone hall maarufu the Gentlemen wa habari, maktaba na burudani. Tulikuwa na ukumbi wa mikutano na TV ya serikali UBC, ikifunguliwa kuanzia jioni, mchana lunch time tukiweka radio set dining hall, weekend kulikuwa wall weekly na local radio programs kutumia redio cassette. Tukitangaza habari za bweni, chuo na kimataifa BBC VOA RSA na Deutche Welle. Ulikuwa ubunifu wangu programs hizi. Nikiitwa Kondo the minister liberator. Nchini Uganda neno kondo ni jizi jambazi, sikuogopa ila walishangaa

Kulikuwa na bajeti Makerere serikali za mabweni yote 8 (wasichana 2 magorofa) Kulikuwepo na serikali kuu Makerere Students Guild. Pia nikichangia pesa zangu, kupata hela uhasibu ikichelewa

Pia nilikuwa katibu wa Tanzania Makerere Students Association TAZAMA

General Amin akitamka kuna mashushu wa Rais Nyerere. Kila sekta aliweka security agents kutoka State Research Bureau SRB Kulikuwa na maagents wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi nk Ilikuwa rahisi kutekwa na kuuawa makao makuu SRB Nakasero hill karibu na Uganda Television

General Amin aliipendelea dini ya Kiislam. Ijumaa ilikuwa mapumziko. Nlipenda kujichanganya kuswali Ijumaa msikiti wa chuo ulijengwa na Sultan wa Zanzibar 1940s kuendelezwa na Agha Khan 1950s. Rais Amin akija kuswali Makerere. Pia wanafunzi Waislam tukialikwa kufuturu Ikulu ndogo Kololo hill

Mji Kampala umejengwa kwenye vilima 7: Makerere, Kololo, Nakasero, Rubaga, Mengo, Namirembe na Old Kampala hill.

Kusoma Makerere au Uganda wakati ule ilikuwa hali ngumu uhai na kiuchumi. Mipaka Uganda na Kenya ilifungwa usafiri rasmi. Kwenda Entebbe na Nairobi tukipanda ndege ATC zilibaki mpaka Seycheles Ethiopia, Rwanda au Burundi

Uchumi wa Uganda ulikuwa umedorora. Ukiwa na pesa ya Kenya unabadili traveller cheques dola kupata KSh Nairobi na kwa magendo mpakani Busia na Malaba 1 Ksh kwa Ug.Sh 500 - 1,000

Kufuatana na testimonies zake Gerson Msigwa baada ya masomo ya sekondari 1994-1999 Songea boys na Mtwango kata, alifanya biashara kuuza mahindi duka kujiajiri

Alikuwa na damu ya Kikinga. Wakinga ni Wachaga mikoa nyanda za juu sawa Wamakonde mikoa ya kusini

Alijiunga Radio Tanzania RTD Songea kama trainee enzi za kina Chisunga Stephen na Seleman Muhogora watangazaji waandamizi RIP. Baada ya in-service training RTD Pugu road akaanza utangazaji Songea

2004 tulienda Songea mafunzo ya NGOs mikoa ya kusini kuhusu MKUKUTA II Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania mpango wa Rais Mkapa.

Tuliwaalika waandishi wengi tukimtumia Adam Mwaibabile RIP mwakilishi ITV.. Gerson Msigwa alisema RTD Itawakilisha na Ms Nyoni, alimuoa baadae. Ni kipindi hiki Radio Maria ilianzishwa Songea na kanisa katoliki

Mara ya pili na mara kadhaa 2006- 2012 nilikutana naye Gerson Msigwa wilayani Tunduru (kwetu) kituo cha maendeleo maarufu KIUMA kijijini Milonde Ndenyende (nyumbani) - angalia picha. RC Ruvuma alikuwa Said Mwambungu RIP.

KIUMA ni kama shirika la elimu Kibaha. Tofauti kuna Ikulu ndogo na uwanja wa ndege. Alikuja wakati wa ziara za Rais Mkapa, Mh Kinana katibu mkuu CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na waziri maliasili utalii Jumanne Magembe. Akija na mwandishi Tunduru DC redio tv Juma Nyumayo

Kwangu hii ni moja ya field journalism tasks akiwa mkoani Ruvuma. Wakati wa Rais Magufuli alipewa jukumu kutangaza barabara za lami zinazounganisha mikoa kutoka Mtwara kusini hadi Mutukula mpaka na Uganda. Hii ni field journalism tasks yake ya pili. Baadae Rais Magufuli akampa promotion kuwa mkurugenzi ikulu habari mawasiliano.

Hizi kazi 2 ndizo za kujisifia kuwa yeye ni Field Journalist? Pia Field Marshall Journalist? Zipi zingine?

Nafahamu
ana diploma uandishi habari kutoka Tanzania School of Journalism TSJ, digrii uandishi habari UDsm School of Journalism and Mass Communication na mwaka jana kapata MBA degree Strategic Planning kutoka St John's University Dodoma part-time degree program

Gerson Msigwa atuambie dissertation BA journalism ilihusu nini professionally? MBA degree dissertation ilihusu nini academically?

Je akipata PhD degree kama Dr Ayub Riyoba alianza kama Daily News reporter na Dr Engelbert Mkoko alianza kama reporter Star TV na ITV, atawadhalilisha vibaya waandishi wenzake na kuwanyanyapaa "stigmatise" kwa kujiona bora kuliko wengine?

Hajui cheo serikalini ni kupanda na kushuka?
 
Huyu mpumbavu ndio amechangia kwa zaidi 90% kuua media za ndani hasa kwenye awamu hii ya Ibilisi samuya, hakuna professional journalist pale kama anavyojinasibu
 
Tunahitaji location wapi anaishi na familia yake, hilo ni muhimu sana ili haki ikatendeke na ionekane kutendeka 9dec .
 
Mkuu hadi tushasahau aisee kama alisema hivi au ndo ulikuwa unachimba vitu
 
Back
Top Bottom