kisugujira
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 774
- 200
Kisugujira,
Nimejaribu ku -relate Heading na What is in nimeshindwa totally, sijui umemaanisha nini
Kweli haina haja tena ya mihadhara, watu wakafundishwe ktk nyumba zao za ibada
daah, maamuzi magumu hadi lipigwe guruneti kumlenga balozi?Mlikuwa hamjui vurugu ikikomaa; hakuna posho! Hakuna vikao wala washa...?"Nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa ni kisima cha amani na mfano wa kuigwa. Lakini sasa hivi kuna ufa umetokea nchini hakuna amani. Wakristo na waislamu wameishi kwa kuheshimiana na kwa upendo kwa muda mrefu. Hivi karibuni kumekuwepo na chokochoko za kidini. Makanisa yanachomwa moto, mapadri, wachungaji na waumini wanauawa. Chama Cha Wananchi CUF kiliitwa ni chama cha kiislamu! Sasa hivi CHADEMA kinasemwa ni chama cha kikristo! Haya yote yanasemwa na serikali na wabunge wa CCM bungeni yakilenga kujenga hofu na kuleta chuki kwa wabunge wa upinzani na wananchi.'' Maneno hayo yalisemwa na Mh.Zito Kabwe wakati wa mjadala wa wizara ya mambo ya ndani baada ya tukio la kusikitisha na kutisha lililotokea Arusha. Aliomba liundwe azimio litakalokemea na kupinga kauli za chuki (hate speeches) toka kwa wabunge wa CCM kwenda kwa wabunge wa vyama vya upinzani bungeni. Pia alipendekeza mihadhara ya kidini yenye kuleta na kuchochea chuki ipigwe marufuku nchini, huku akisisitiza upendo na umoja kwa kusema, "Sisi sote ni ndugu. Linapokuja swala linalohusu maslahi ya Taifa,tofauti za vyama, dini na ukabila yatupasa kuvitupilia mbali."Leo hii azimio hilo na mambo mengine yenye manufaa kwa Taifa yamepigiwa kura na kuungwa mkono na wabunge wote bungeni Dodoma, huku Mh. Dr Augustino Lyatonga Mrema, akitoa siku saba za kukomesha mihadhara yote ya kidini hapa nchini.
hivi kuna tofauti yoyote kati ya mihadhara na mikutano ya injili?? lugha inanisumbua
hivi kuna tofauti yoyote kati ya mihadhara na mikutano ya injili?? lugha inanisumbua
Kisugujira,
Nimejaribu ku -relate Heading na What is in nimeshindwa totally, sijui umemaanisha nini
Mtoa mada acha unafiki, mbona vipande hivi hapa umeviacha, ZZK kaugusa "mfumo" tunaolalamikia waislamu....
Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni "very irresponsible" tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.