Huyu ndiye Prof. Sospeter Muhongo usiyemjua

Hizo ngonjera hazisaidii chochote mkuu.
Akajipange upya.
 
Ongezea hii nyingine umesahau toka kawa waziri wa nishati na madini Tanesco hasara imekuwa ikiongezeka kwa kasi ya kutisha
 
Ila pia tusisahau kuwa ni Mwizi kweli kweli alilidanganya bunge , akalibiia na Taifa mwizi kabisa kabisa hafai hata kanisani wala msikitini mwizi
 
kwenye hyo cv mbna hujaweka kipengele cha kuiba pesa za ........ingemuongezea uzito sana hyu PROPESA wetu.

Ilisemwa hapa kuwa kapata kazi ya kimataifa baada ya kufukuzwa uwaziri hapa TZ. Kumbe ile ilikuwa usanii? Mbona haitajwi kwenye hii Cv? Nakumbuka kuna wakati alihojiwa na shirika moja la utangazaji la kimataifa, naye hakugusia hiyo latest appointment!!!
 
Angekuwa Jembe asingekubali kufanya kazi na kikwete, hata kama kikwete alimuahidi kitu gani alipaswa kukataa sababu taifa Zima linajua kikwete ni muongo yeye alikubali vipi kama jembe.

ujembe wake ulipaswa umuonyeshe likelihood kubwa ya kukutana na madhira aliyokutana naye kwa kufanya kazi na kikwete,
 

Ok. Hebu mpime kwa yale mafanikio aliyoyafanya akiwa MEM, je anaweza au?

Inamaana hujaona idadi ya nguzo zilizosambaa kote nchini zikiwatafuta wanavijiji kuwaondolea ujika umasikini na maradhi?
 
Ila pia tusisahau kuwa ni Mwizi kweli kweli alilidanganya bunge , akalibiia na Taifa mwizi kabisa kabisa hafai hata kanisani wala msikitini mwizi

Aliiba kiasi gani au aliiba nini?

Isije kuwa aliwaibia wake zenu ndiyo maana mnamkasirikia na kumwita mwizi BILA KUTAJA KAIBA NINI
 
Umesahau kutaja sifa zake kuu mbili ambazo ni UWONGO na MAJIVUNO
 
Bado mnahangaika na profesa Mhongo, huyu si alishatupwa kwenye dustbin na profesa JK!!

Yeah, anaweza kuwa alitupwa kwa bahati mbaya mtoto mdogo akabeba hiyo dustbin akamwaga uchafu wake MEZANI.

Baada ya kuchambua tukakuta kuna kitu cha thamani ndani yake....:smile-big:

Sasa siku ukiambiwa ndiye CHAGUO LA CHAMA sijui utahama nchi au?

Nakushauri usitoe hukumu kwa yeyote wakati huu wa kutafuta wagombea.... kwani baadhi yao wakishinda huwa WANALIPIZA VISASI.... TAKE CARE
 
Ninaweza kutamka bila shaka kuwa, 'HATA UWE NA AKILI NA UWEZO WA NAMNA GANI, UKIPEWA KAZI YA KUWAONGOZA VICHAA SI AJABU VICHAA WOTE WAKAKUZONGA NA KUKUTUKANA KUWA HUNA AKILI WALA UWEZO WA KUWAONGOZA. NA VICHAA WANAWEZA KUUNGANA NA KUMTANGAZA KICHAA ZAIDI YA WOTE KUWA NDIYE MWENYE AKILI NA UWEZO WA KUWAONGOZA NA WAKAKUFUKUZA WEWE ULIYE MZIMA'.

Watanzania tumekuwa kama vichaa maana hatuelewi tunataka nini. Tunafurahia kuongozwa na kutawaliwa na wajinga wenye maneno ya kutupamba hata kama maneno haya hayatusaidii wala kuondoa mahali tulipo. Tunawachukia watu wenye akili na uwezo alimradi tu kama watu hao ni watii wa nafsi zao na wana ujasiri wa kutueleza ukweli ambao wakati mwingine ni ukweli wenye majonzi.

Hata tumpe uwaziri wa Nishati mtu gani, hakuna mtanzania hata mmoja wala watanzania kwa umoja wao wenye uwezo wa kutafiti mafuta au gas kwenye deep waters. Watu wanaweza wasipende ukweli huu alioutamka Muhongo lakini ni kweli kwamba hata tusipopenda haitabadilisha ukweli huo. Tunaweza kuzuia kusikia lakini hatuwezi kuzuia ukweli. Siyo kwamba mataifa mengine yote ni wajinga au siyo matajiri kama sisi kiasi kwamba mpaka leo hii ni makampuni 6 tu Dunia nzima ndiyo yanayotafiti na kuchimba mafuta/gas kwenye maji ya kina kirefu. Huo ni ukweli, na hauwezi kubadilika kwa sababu hatupendi kuusikia.


 
Huo uchafu kuupata si kazi km unaperuzi waliyoandika wengine bila kuhitaji realtime decision making.
 
....ndo maana mwizi sana kumbe limesoma hivo hili jamaa jizi sana, ...
 
Ok. Hebu mpime kwa yale mafanikio aliyoyafanya akiwa MEM, je anaweza au?

Inamaana hujaona idadi ya nguzo zilizosambaa kote nchini zikiwatafuta wanavijiji kuwaondolea ujika umasikini na maradhi?

Wow...siwezi amini kama unaweza kutoa comparison ya namna hiyo na ikakubalika. Kwanza ukumbuke kuwa kwa uzembe wake ni mabilioni mangapi yamepotea? Je unaweza kulinganiza na hizo nguzo unazosema? How many people are dying kwa kukosa madawa mahospitalini, au wanapata elimu zisizo na viwango kwa sababu ya ubadhilifu unaofanyika huko serikalini? Escrow ni mfano tu, kuna uchafu mwingi ambao haujafumuliwa kwa public ikiwemo mradi wa bomba la gesi.
 
ongeza na mwizi kwenye cv yake

Mkuu umesahau, nyodo na jeuri plus kujidai, hivi yeye anadhani ndo professa wa kwanza Tanzania?,Ila Mungu mkubwa mtu kama huyu hakupewa kipaji hata cha kusikilizwa na familia yake.
 
This kind of information needs to be known before someone gets sucked, it could help him!
 
Niseme hivi: Prof Muhongo amesheheni weledi katika taaluma. Prof Muhongo ana mafanikio makubwa sana kielemu na ni wachache sana kwenye bara hili la Africa wanafikia mafanikio yake. Hata Prof Lipumba ambaye anaitwa na mashabiki wake bingwa wa uchumi duniani (sikweli japo naheshimu mafanikio yake) ni mtoto tu ukilinganisha na miguu ya Muhongo katika taaluma na mafanikio yake. Naona uwaziri katika serikali hii iliyojaa rushwa na ubadhirifu ilikuwa ni kosa kubwa sana kwa Muhongo. Angeukataa uwaziri, kwanza si size yake lakini kibaya zaidi inamshushia hadhi na kuanika udhaifu wake katika mawasiliano.
Lakini pia niseme kwa dhati kabisa licha ya Weledi wake na mafanikio yake adhimu Prof Muhongo, ambaye alifaulu kupitia darasa nililomaliza darasa la saba miaka mingi kabla sijazaliwa ameufedhehesha taaluma na hadhi yake kwa kukubali mtindo wa kupiga dili alioukuta katika serikali ya JK Kikwete na ambayo ni desturi katika utawala wote wa CCM ulivyokuwa baada ya Mwl. Nyerere. Prophesa KAIBA pesa ya umma ambao kwa alipofikia hakuwa na haja ya kudhalilisha maadili yake kwa tamaa za kipumbavu za watu wa CCM. Angejiuzulu asijishushie heshima hata kama bosi wake JK ndiye alikuwa mkuu wa dili. Hata kama Prof hatuna ushahidi kwamba aligawiwa ngapi (kumbuka waliogawiwa Pesa Stanbic hata kamati ya PAC haikupata majina yao)ushahidi wa kimazingira na kimantiki ni kwamba wanufaikaji wakubwa wa dili hili la kishenzi ni Profesa Muhongo na bosi wake.
Profesa umejiaibisha na umeaibisha taaluma yako na wanataaluma.
Mwisho niseme Profesa amefanya kazi vizuri sana Tanescco na watu wa Tanesco amewanyosha na kuwaondolea urasimu wa kijinga waliokuwa nao. Mazuri aliyofanya hayawezi kufuta makosa makubwa waliyoitendea taifa, yeye na bosi wake Profesa wa Kichina.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…