Huyu ndiye mwanaume sasa

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,471
2,000
Mwanaume unatakiwa kujitambua na kujiheshimu bila kusahau kuutunza ujana wako kwa maneno yenye hekima na busara, kama wewe ni kijana na haujaoa na una miaka 25 kwenda juu basi jua wewe ni baba pasipo mtoto jiandae kuwa baba bora na mume bora kwa matendo na mawazo bila kusahau kuitunza haiba yako ya kiume kwa mavazi safi na bora.

__MWANAUME
anayejiheshimu huwa hanyoi kiduku hata siku moja, kijana bora mwenye kujitambua huwa sio mtumwa wa pombe hata siku moja, kuwa na idadi kubwa ya wanawake sio ujanja bali ni utumwa wa fikra sababu unatakiwa uitawale pombe na wanawake.
Sasa ni wakati sahihi wa kuacha ujinga na kujiandaa kuwa mume bora na baba bora.

_MWANAUME
anayejitambua havai nguo za kubana mapaja, havai mlegezo wala havai nguo za kubana makalio, mtoto wa kiume' jaribu kuwa muungwana sababu neno mwanaume limebeba ubora wa utashi wa fikra na tabia

_WANAWAKE
wanapenda wanaume wenye upeo mkubwa na wanao jiamini sababu mwanaume ni kiongozi na kichwa katika familia sasa unawezaje kuwa kichwa cha familia na kiduku huku ukiwa na mlegezo??
Wewe ambaye upo chuo ujanja si kupiga selfie na wanawake au kushinda kwenye instagram part kila weekend' badilika sasa na acha ujinga tumia chuo kama kiwanda cha maarifa na sio sehemu ya fashion show na mashindano ya kununua smart phone, kuwa mwanaume bora ili ukikutana na wanaume wenzio uzungumze kama mwanachuo aliyekomaa na sio kulamba lamba midomo.

Ongeza idadi ya kusoma vitabu na sio kuwa mashindano ya kuwa na idadi nyingi ya likes za picture za swagger na wingi wa majina yasio na tija' kumbuka kendrick lamar alitengeneza brand ya jina lake na wewe tengeneza brand name yako na sio kuiga ujinga usio na tija.

YOU CANNOT CHANGE YESTERDAY, BUT YOU CAN CHANGE TODAY AND TOMORROW;
JIFUNZE KUHESHIMIWA NA WAZEE WA HEKIMA NA KUJIONA KIOO KWA WENGI KWA KARIA YAKO
 

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,343
2,000
_MWANAUME
anayejiheshimu huwa hanyoi kiduku hata siku moja, kijana bora mwenye kujitambua huwa sio mtumwa wa pombe hata siku moja, kuwa na idadi kubwa ya wanawake sio ujanja bali ni utumwa wa fikra sababu unatakiwa uitawale pombe na wanawake.
Eti unaitawala vipi Pombe?...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom