Huyu ndiye Mwanamke nimtakaye...

Huyu ndiye Mwanamke nimtakaye...

Mke wangu mtarajiwa (sijui uko wapi sasa), nafahamu uko sehemu salama na ukivuta muda na 'jamaa' mwingine kabla hatujaoana kwa nderemo na vifijo..., Lakini kabla sijakuweka ndani kuna yenye kutoka moyoni kwangu machache ya kukueleza LAAZIZI...

1. My dear future wife, Jiandae kuwa mother of my beloved family wala sio "mom material" .., usipaniki!!! Nitakuelewesha maana yangu mke wangu mtarajiwa...

Mke wangu mpendwa mumeo, nitakuwa 'father' wala sio 'daddy' kwa watoto wetu, usishangae nitawalea watoto wetu katika malezi ya tamaduni za kiafrika zaidi, hivyo kwa hilo ntakuwa conservative na sio liberal.

Ningependa kukuona ukiwa 'MAMA' wala sio 'MOM' ukiwalea watoto kwa tamaduni za kigeni, wewe ndie utakuwa msingi wa maisha ya familia yangu.., natambua kabisa, utapaswa kuishi katika misingi ya mumeo mimi...

2. My future dear wife, nitakuoa kutokana na uzuri wa asili uliojaaliwa na Mungu, hivyo basi usitarajie kupata wasaa wa kujipachika kope na kucha za bandia wala mawigi (nywele za marehemu)..., wewe ni nani hadi ujichafue na mikorogo..? Hakuna kutafuta uzuri nje ya uzuri wako wa asili..

3. My future dear wife, huko uliko ni vyema ukaanza kujifunza kuendesha biashara na kusimamia, mumeo siamini katika kuajiriwa Bali kujiajiri.., nimeajiriwa, nikakimbia ajira.. Sitaki kuwa mtumwa wa kiumbe mwingine.., napenda na wewe usiwe mtumwa wa mtu mwingine.. Anza kujifunza huko, boss of your own metaphor.

4. My future dear wife; Siku tutakayokula kiapo kanisani mbele ya Kasisi, nyuma wazazi wetu wakitabasamu, tutafanywa kuwa mwili mmoja, hivyo basi, nisingependa baadae kutenganishwa na password kwenye simu zetu (no passwords).., simu ina password zaidi ya lango la white house au pentagon..

5. My future dear wife; madhehebu yote mchana kweupeeeee yanakiri kwamba MUNGU ni mmoja tu, muumba Mbingu na nchi, hivyo basi nisingependa kukushuhudia ukihama madhehebu mbalimbali kutafuta ushuhuda usiotimia. Usihangaike na madhehebu, simama katika imani. Mungu wetu ni mmoja.

6. My dear future wife; kilichopo ndani ya uwezo wangu utapata., nitakupa kwa moyo wa dhati, nitakupenda kwa dhati ya Moyo wangu.., nitakupa heshima yangu yote.. sitapenda kuona mke wangu ambae hawezi kuniheshimu mimi na wazazi wangu.. Ukimpenda Mungu, utaipenda na kuheshimu familia yangu..

MY FUTURE WIFE, msalimie sana huyo mnayevuta nae muda kwa kwenda Samaki Samaki, Club84, Hyatt, Jembe ni Jembe, sijui kwenye live band huko NK mara Villa Park, Nyama Choma festival, Fiesta, sijui White Party, mara birthday na huko katika marriage festival.., na makasheshe mengine yote ya usiku mjini hapa..

Mimi nitakupeleka kanisani na kukuweka ndani ya nyumba yangu, utakuwa mke.., nitakuoa na kukupa watoto, utaniita mume na utakuwa mke wangu, mama wa watoto wangu.., nitakupenda na Mbingu na ardhi zitaimba na kusifu..

(just thinking positively.. But what do i know).., sijui sasa hivi 'wanakuviringa' wapi kipenzi changu.. Aisee!! LIFE!

Ndimi; Mumeo tarajali...
Umenena mengi ya msingi ukizingatia maisha ya sasa hivi yenye changamoto za utandawazi. Watu kuacha tamaduni za zamani na kuiga zile za kimagharibi.
Labda niongeze tu kuwa kupata mwenza sahihi awe mke au mume sio jambo rahisi kwani ndoa ni muungano unaotegemewa kudumu maisha yote (life long) baina ya watu wawili ambao wamezaliwa na wazazi tofauti na pengine kulelewa kwenye mazingira tofauti kabisa pia. Watu hao pia huweza kuwa hawajafahamiana kwa undani na uwazi kabisa.
Kwa maisha haya ya sasa wachumba huweza kuwa wamekutana vyuoni, ofisini, vituo vya basi, nyumba za ibada, ufukweni na wengi kwenye mitandao ya kijamii! Hutumia muda mfupi kufahamiana kabla ya kufunga ndoa. Watoto wengi wa kike siku hizi wanasoma ili kuepuka kuwa tegemezi kwa waume zao. Hivyo hupelekea kukimbizana na umri kwani wasichana tofauti na wavulana wanabanwa na umri haswa kwenye masuala ya kuolewa na kuanzisha familia. Kutokana na hili huwa wanalazimika mara nyingi kushurutisha wachumba wao wawaoe pasipo wavulana kuwa tayari. Wavulana wengi hujikuta wameoa pasipo kukaa kwenye uchumba muda wa kutosha kutokana na msukumo unaotoka kwa wachumba zao wa kutaka kuolewa kukabiliana na umri. Ndoa za namna hii mara nyingi huwa hazidumu kwani wawili hao hawakuwa wameshafahiama vya kutosha kujua kama wanaweza kuishi pamoja kwa kuwa na tabia zinazofanana (compartibility). Nadhani ni muhimu wachumba wakatumia muda wa kutosha kufahamiana tabia, kujua mapungufu na mazuri ya kila mmoja, kufahamu maisha ya uhalisia ya familia ya kila upande. Hili ni muhimu kwani ndoa si tu huunganisha wapendanao hawa wawili bali pia huunganisha familia walizotoka na ukizingatia tamaduni zetu, mara nyingi familia hizi huwa kubwa na changamoto pia huwa kubwa vilevile hivyo huhitaji busara na uvumilivu wa hali ya juu katika kukabiliana nazo.
Haya ni machache tu lakini la msingi na kubwa kabisa ni kuwa kupata mke au mume mwema hakutokani tu na uwezo wa kibinadamu bali ni muhimu kumshirikisha MUNGU ili aweze kukuongoza uvuke salama!
 
Ahsante kwa mchango uliosheheni madini, hekima na busara
 
Aise ukipata wa hivyo kweli umshukuru Mungu wako, ni kama hakuna siku hizi..
 
Positive people, so sweet.
Mungu akufanyie wepesi upate mwenye kukuelewa na kukupenda kwa dhati.
 
Maneno ya kufikirika hayo wanaume wa hivi walikufa vita ya pili ya dunia
 
Back
Top Bottom