Kwa rasilimali hizi lukuki tulizojaaliwa nazo za watu, ardhi nzuri/kubwa na maliasili za madini na nyingine kama gesi; tunahitaji Rais wa awamu ijayo afutilie kwa mbali 'misifa ya ujanjaujanja' wanayojimwagia Wakenya kwamba ndio kiboko wa uchumi (economic giant) wa Afrika Mashariki. Na kazi hiyo aifanye ndani ya miaka mitano ya kwanza ya utawala wake. Kisha, ile mitano tutakayomuongezea iwe ni ya kukimbizana na Malaysia, Thailand, Afrika Kusini, Nigeria na India; huku tukimkodolea mimacho na kumnyemelea China kwa mbali!!