Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 211
Ni siku ya ijumaa asubuhi saa 3 , nilitakiwa kwenda kituo cha polisi na risiti ya laptop ambayo polisi aliichukuwa kinguvu toka mikononi mwangu , nikamwonyesha risiti na taarifa zingine za laptop yangu , lakini nikamwomba niiwashe niangalie kama baadhi ya data zangu zipo , kweli kuangalia data zilikwepo zote , ndio hapo akarudisha laptop ya kwanza .
Kuanza kurudisha laptop hii ilibidi twende kituo cha polisi kwa nyuma ambapo amepaki gari lake na katika buti la gari ndio laptop yangu ilipokuwa imehifadhiwa , maana yake kama hiyo gari ingepata matatizo au chochote kutokea laptop yangu na vitu vyangu vingine vingekuwa vimepotea pia .
Nikamuuliza kama ile laptop yangu aliandikisha pale polisi , jibu lake lilikuwa ni rahisi sana haya ni maswala yetu , wale polisi wengine wakikuuliza usiseme kama umekuja hapa kwa kazi hiyo waambie hadithi zingine zozote usishangae sana majibu haya yanatoka kwa huyu polisi ambaye ni CID mpelelezi katika kituo hicho cha polisi .
Sasa likaja katika suala lingine la laptop inayofuatia ambayo nilinunua kwa mtu lakini hakunipa risiti , polisi anataka nielewane nae , niongee nae kiurafiki halafu nimpe pesa kidogo laki 2 hivi ndio anirudishie ile laptop au nimpe risiti , lakini nilishamwambia laptop nilinunua kwamtu na mtu mwenyewe yuko mbali hakunipa risiti .
Mpaka hapo lililo wazi ni kwamba polisi anataka nimpatie pesa kidogo ili aweze kunirudishia ile laptop pamoja na vitu vyake , kwa makubaliano ya nje ya polisi , tangia pale mwazo niliposhikwa sikuandika maelezo yoyote yale lakini ilikuwa ni haki yangu kuandika maelezo .
Nilipata vitisho kama tutakupoteza ukiendelea kuhoji haki zako , au tutakubambika kesi zingine kama ukiendelea kuhoja , unachotakiwa ni kutusikiliza sisi na unyamaze kimya la sivyo utakiona ndio hivyo kwahiyo nikanyamaza sikuwa na njia za ziada .
NJEE YA POLISI
Muda wa saa 5 hivi asubuhi nilitoka nje pale viwanja vya polisi , huyu polisi akaniomba nimpeleke mjini katika duka moja la computer akanunue kifaa Fulani sikujua ni kifaa gani , kwa kuwa mimi ni mdadisi nikaona nimsindikize tu nikaone yeye binafsi anataka kufanya nini haswa .
Ghafla ikaongia difenda ya polisi , kukawa kuna watu wamesimama polisi wawili wameshika silaha kali kali , mmoja ana uniform za polisi mwingine amevaa nguo za kiraia lakini wote ni askari .
Hiyo gari ilikuwa inafuatiwa na Toyota rav 4 , ni mama mmoja alikuwa anatokwa na machozi , wakafika pale watu wakashuka kwenda kutoa maelezo polisi , wengine wakabaki wanashangaa shangaa katika lile difenda .
Nilisikia sauti ya kijana inasema mama ninakufa , anapiga makelele sana , badi nikapita karibu kwenda kuona kule katika difenda wamepakia nini , ilikuwa maajabu kidogo ni kijana mmoja alikuwa amepigwa na damu zilikuwa zimechuruzika mwili mzima amekaa nyuma ya difenda na mapolisi wametoka kwenda kituoni bila kuangalia yule kijana atakufa au nini .
Taarifa zikasema kwamba yule kijana alikwapua simu ya mtu , na yule aliyekuwa anaendesha rav 4 ni dada yake , nilipochuguza zaidi nikakuta kumbe ni ugomvi wa kimapenzi umesababisha kijana wa watu aitwe kibaka na mmoja wa wasichana waliokuwa wanaandika maelezo eneo husika kwahiyo ndio hivyo kijana amepatikana .
Yule polisi niliyekuwa nam ngoja mimi , akaja kuangalia mwili wa yule kijana walipomweleza ni kibaka akashangilia sana , akasema safi sana , ndio wakome .
Mimi na yule polisi mguu kwa mguu mpaka nyumba moja ya wageni ambayo huyu polisi anapaki gari lake na kulala huko huko , kufika kule akaenda chumbani kwake akaleta laptop moja matata sana na ni mpya aina ya Fujitsu Seamens .
Nikaishika pale na kupakia katika gari lake la kifahari kuanza safari ya kuelekea mjini sasa katika duka moja la vifaa vya computer , gari ilikuwa inakimbizwa sana utafikiri sio polisi na alikuwa haangalii mataa yeye ni mwendo mdundo tu .
Kama unavyojua mimi sikutoa pesa pale polisi , tulivyofika kituo cha mafuta polisi akaniambia naomba uchangie mafuta kwa kuwa hujatoa chochote kule polisi mimi kwa kichwa upande nikatoa alfu 10 kwa ajili ya mafuta .
Kufika sehemu moja inayoitwa Bibi Titi akabipigiwa simu dada mmoja hivi , huyu dada akawa anataka msaada wake kwa kuwa mtuhumiwa wake alikuwa ameshamuona , polisi akamwambia ameongezee dola katika simu yake ili aweze kuwasiliana na polisi mwenzake .
Alivyoongezewa dola 20 katika simu yake yeye akampigia polisi mwenzake aliyekuwa pale kituoni akamwambia achukue taxi huyo dada aliyempigia atalipa ndio waende kumkatama mhalifu mwenyewe na ndio mambo ya askari wetu hayo .
Tukafika hapo dukani , tukashuka la laptop na kwenda katika duka lenyewe tukaomba adaptor ya umeme yenye dhamani ya dola 55 za kimarekani , na kuiwasha hiyo computer .
Computer hiyo ilivyowaka , na nilipoanza kuiangalia nikakuta hiyo laptop imesajiliwa kwa Gabriel Shirima wa Ilulu Dodoma , sasa sikuelewa hiyo laptop imefikaje pale kwa yule polisi na kwa nini anaifanya ni mali yake binafsi sikupenda kumuuliza si mali yake lakini haina usajili wake .
Na ndio tukaanza safari ya kurudi sehemu zingine na mimi nikamwomba anishushe kazini kwangu nilipokuwa naenda kuendelea na shuguli zangu zingine na ndio hivyo bwana shirima Laptop yake iko kwa polisi sijui imefikaje fikaje pale .