Huyu Ndio CID

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ni siku ya ijumaa asubuhi saa 3 , nilitakiwa kwenda kituo cha polisi na risiti ya laptop ambayo polisi aliichukuwa kinguvu toka mikononi mwangu , nikamwonyesha risiti na taarifa zingine za laptop yangu , lakini nikamwomba niiwashe niangalie kama baadhi ya data zangu zipo , kweli kuangalia data zilikwepo zote , ndio hapo akarudisha laptop ya kwanza .

Kuanza kurudisha laptop hii ilibidi twende kituo cha polisi kwa nyuma ambapo amepaki gari lake na katika buti la gari ndio laptop yangu ilipokuwa imehifadhiwa , maana yake kama hiyo gari ingepata matatizo au chochote kutokea laptop yangu na vitu vyangu vingine vingekuwa vimepotea pia .

Nikamuuliza kama ile laptop yangu aliandikisha pale polisi , jibu lake lilikuwa ni rahisi sana “ haya ni maswala yetu , wale polisi wengine wakikuuliza usiseme kama umekuja hapa kwa kazi hiyo waambie hadithi zingine zozote “ usishangae sana majibu haya yanatoka kwa huyu polisi ambaye ni CID mpelelezi katika kituo hicho cha polisi .

Sasa likaja katika suala lingine la laptop inayofuatia ambayo nilinunua kwa mtu lakini hakunipa risiti , polisi anataka nielewane nae , niongee nae kiurafiki halafu nimpe pesa kidogo laki 2 hivi ndio anirudishie ile laptop au nimpe risiti , lakini nilishamwambia laptop nilinunua kwamtu na mtu mwenyewe yuko mbali hakunipa risiti .

Mpaka hapo lililo wazi ni kwamba polisi anataka nimpatie pesa kidogo ili aweze kunirudishia ile laptop pamoja na vitu vyake , kwa makubaliano ya nje ya polisi , tangia pale mwazo niliposhikwa sikuandika maelezo yoyote yale lakini ilikuwa ni haki yangu kuandika maelezo .

Nilipata vitisho kama tutakupoteza ukiendelea kuhoji haki zako , au tutakubambika kesi zingine kama ukiendelea kuhoja , unachotakiwa ni kutusikiliza sisi na unyamaze kimya la sivyo utakiona ndio hivyo kwahiyo nikanyamaza sikuwa na njia za ziada .

NJEE YA POLISI

Muda wa saa 5 hivi asubuhi nilitoka nje pale viwanja vya polisi , huyu polisi akaniomba nimpeleke mjini katika duka moja la computer akanunue kifaa Fulani sikujua ni kifaa gani , kwa kuwa mimi ni mdadisi nikaona nimsindikize tu nikaone yeye binafsi anataka kufanya nini haswa .

Ghafla ikaongia difenda ya polisi , kukawa kuna watu wamesimama polisi wawili wameshika silaha kali kali , mmoja ana uniform za polisi mwingine amevaa nguo za kiraia lakini wote ni askari .

Hiyo gari ilikuwa inafuatiwa na Toyota rav 4 , ni mama mmoja alikuwa anatokwa na machozi , wakafika pale watu wakashuka kwenda kutoa maelezo polisi , wengine wakabaki wanashangaa shangaa katika lile difenda .

Nilisikia sauti ya kijana inasema mama ninakufa , anapiga makelele sana , badi nikapita karibu kwenda kuona kule katika difenda wamepakia nini , ilikuwa maajabu kidogo ni kijana mmoja alikuwa amepigwa na damu zilikuwa zimechuruzika mwili mzima amekaa nyuma ya difenda na mapolisi wametoka kwenda kituoni bila kuangalia yule kijana atakufa au nini .

Taarifa zikasema kwamba yule kijana alikwapua simu ya mtu , na yule aliyekuwa anaendesha rav 4 ni dada yake , nilipochuguza zaidi nikakuta kumbe ni ugomvi wa kimapenzi umesababisha kijana wa watu aitwe kibaka na mmoja wa wasichana waliokuwa wanaandika maelezo eneo husika kwahiyo ndio hivyo kijana amepatikana .

Yule polisi niliyekuwa nam ngoja mimi , akaja kuangalia mwili wa yule kijana walipomweleza ni kibaka akashangilia sana , akasema safi sana , ndio wakome .

Mimi na yule polisi mguu kwa mguu mpaka nyumba moja ya wageni ambayo huyu polisi anapaki gari lake na kulala huko huko , kufika kule akaenda chumbani kwake akaleta laptop moja matata sana na ni mpya aina ya Fujitsu Seamens .

Nikaishika pale na kupakia katika gari lake la kifahari kuanza safari ya kuelekea mjini sasa katika duka moja la vifaa vya computer , gari ilikuwa inakimbizwa sana utafikiri sio polisi na alikuwa haangalii mataa yeye ni mwendo mdundo tu .

Kama unavyojua mimi sikutoa pesa pale polisi , tulivyofika kituo cha mafuta polisi akaniambia “ naomba uchangie mafuta kwa kuwa hujatoa chochote kule polisi “ mimi kwa kichwa upande nikatoa alfu 10 kwa ajili ya mafuta .

Kufika sehemu moja inayoitwa Bibi Titi akabipigiwa simu dada mmoja hivi , huyu dada akawa anataka msaada wake kwa kuwa mtuhumiwa wake alikuwa ameshamuona , polisi akamwambia ameongezee dola katika simu yake ili aweze kuwasiliana na polisi mwenzake .

Alivyoongezewa dola 20 katika simu yake yeye akampigia polisi mwenzake aliyekuwa pale kituoni akamwambia achukue taxi huyo dada aliyempigia atalipa ndio waende kumkatama mhalifu mwenyewe na ndio mambo ya askari wetu hayo .

Tukafika hapo dukani , tukashuka la laptop na kwenda katika duka lenyewe tukaomba adaptor ya umeme yenye dhamani ya dola 55 za kimarekani , na kuiwasha hiyo computer .

Computer hiyo ilivyowaka , na nilipoanza kuiangalia nikakuta hiyo laptop imesajiliwa kwa Gabriel Shirima wa Ilulu Dodoma , sasa sikuelewa hiyo laptop imefikaje pale kwa yule polisi na kwa nini anaifanya ni mali yake binafsi sikupenda kumuuliza si mali yake lakini haina usajili wake .

Na ndio tukaanza safari ya kurudi sehemu zingine na mimi nikamwomba anishushe kazini kwangu nilipokuwa naenda kuendelea na shuguli zangu zingine na ndio hivyo bwana shirima Laptop yake iko kwa polisi sijui imefikaje fikaje pale .
 
Sasa hii ni muendelezo wa ile ya kwanza titled " hili ndio jeshi letu" au hii mupya kabisa.........nipo interested sana na hizi stories zako, nilikuwa disappointed uliposusa kwenye ile nyingine!!!.
Sasa ulifuatilia kujua hatima ya "kibaka mpakaziwaji" mwizi wa simu?..je huoni kuwa ni busara kuweka jina la kituo husika cha polisi hapa ili watu wawe makini?.
Je wewe ulipata laptop yako? Unampango wowote wa kumtafuta bwana Shirima ili upate upande mwingine wa story.....!!?
 
Sasa hii ni muendelezo wa ile ya kwanza titled " hili ndio jeshi letu" au hii mupya kabisa.........nipo interested sana na hizi stories zako, nilikuwa disappointed uliposusa kwenye ile nyingine!!!.
Sasa ulifuatilia kujua hatima ya "kibaka mpakaziwaji" mwizi wa simu?..je huoni kuwa ni busara kuweka jina la kituo husika cha polisi hapa ili watu wawe makini?.
Je wewe ulipata laptop yako? Unampango wowote wa kumtafuta bwana Shirima ili upate upande mwingine wa story.....!!?

NDIO HUU NI MWENDELEZO KWA SABABU WALISEMA NI UDAKU NA IKAONDOLEWA BASI NIMEANZA KUANDIKA KWA VIPENGELE KWA VICHWA VYA HABARI TOFAUTI TOFSAUTI .

YULE KIBAKA NITAENDELEZA HADITHI YAKE WAKATI UJAO KATIKA MAKALA INAYOFUATIA , JINA LA KITUO NAFICHA KWA SASA KWA SABABU JUMAPILI HII KUNA TUKIO LINGINE LINAENDELEA NATAKA KULIANDIKA JUMATATU KWA SABABU NITAKUTANA NA POLISI HUSIKA KWA MAZUNGUMZO

LAPTOP MOJA NIMEPATA NYINGINE SIJAPATA SASA HII YA PILI NDIO ANATAKIWA ANIPE JUMAPILI NAPENDA KUITA WAANDISHI WA HABARI ILI WAONE MOTION ZAKE NA MANENO YAKE KILA HATUA

BWANA SHIRIMA SIJAFANIKIWA KUMPATA
 
Hongera sana mkuu kwa juhudu zako.....watu kama mimi tulio mbali na nyumbani tuna tegemea sana watu kama wewe kutupa hizo uptodates za maisha huko home.
Wale waliosema udaku shauri lao, lakini kumbuka kwamba huu ni uwanja mkubwa sana....kwahiyo audiance ipo tu no matter what!!!
Nimeona nyingine tena ya "miezi 4 baadae".....intriguing!!!. Lakini kaka, mie naona kama yule dada,polisi na jamaa aliyekuwa anauza laptop siku ile pale cafe kama timu moja vile...what do you think!!?.
Anyway,mie nitaendelea kutega sikio.....again hongera kwa juhudi zako za kuweka hawa "mabaradhuli" hadharani, watakao sema udaku just ignore them na usisuse........
 
Ndio wale ni kitu kimoja kwa sababu moja ya email niliyoisoma sasa hivi nimeangalia IP address inafanana zote mbili na polisi sasa hivi ametoa siri nyingi kwa hao watu na wengine wengi kuhusu taarifa hizo lakini nashangaa kwanini polisi anatoa taarifa kwa wahalifu wakati kesi bado inaendelea
 
kwanza pole pili nakushauri uende pcb na wakupe pesa za moto na uwashikishe hao polisi wasio na haya mbele ya watu wa pcb bila wao kugundua.... wakomeshe uwezavyo na iwe mwanzo na mwisho wao...
 
Jana jioni rafiki yangu mmoja alipata na tatizo kidogo , yeye alipaki gari lake sehemu Fulani kule mikocheni , kisha askari wa jiji wakaja kubeba lile gari lake wakapeleka kituo cha oysterbay .

Alipofika pale akaambiwa gari lake liko kituo cha polisi akaamua kwenda mpaka kituo cha polisi alivyofika pale akaambiwa anatakiwa alipe alfu 30 kama faini ya kupaki gari ovyo na zingine alfu 20 kwa ajili ya gari lililokuja kubeba gari lake .

Huyu jamaa yangu akagoma kutoa hiyo hela kwa sababu alisema yeye hajafanya kosa lolote na eneo ambalo yeye alipaki gari lake haikuwa na kibao chochote kinachosema hakuna kupagi gari sehemu husika au hakukuwa na alama zozote za barabarani .

Nikapigiwa simu mimi nikatakiwa kwenda pale kituoni na nikafika kwa wakati muafaka hapo katika mapokezi ya polisi , kuulizia nikaambiwa mwenzako amefanya hivi na vile naomba ulipe kiasi Fulani che pesa lakini kabla sijaanza kutoa pesa , polisi mmoja akaniuliza kwani kuna nini nisiwe na presha

Nikamwambia achukue hizo hela halafu warudishe kadi za gari na vitu vingine muhimu katika gari , baadaye kidogo polisi mwingine akaniambia wanataka kuangalia hilo gari kama limelipiwa kodi zote na kuangalia vitu vingine kama vizima au la .

Ghafla nikaona mtu mmoja analetwa na polisi anapigwa mateke , alipifika mapokezi akakatwa ngwara mpaka chini kichwa chake kikajigonga katika ukuta akaishiwa nguvu kabisa wakamwambia avue mkanda wake , alipokuwa anavua mkanda wake polisi mwingine akaja zake huko na bakora akamchapa .

Baadaye yule kijana akapelekwa mahabusu bila maelezo yoyote pale mapokezi ya polisi na alipokonywa vitu vyake vyote kule ndani aliingia na kibukta chake tu bila maelezo yoyote zaidi

Muda kidogo tukaenda na polisi nje wakakague gari letu , tulipofika kule tukakuta matairi yameshatolewa upepo na moja likawa limebadilishwa limewekwa tairi kipara , tukawaomba wajaze upepo tu tuondoke na gari hatungependa kuendelea kukaa pale zaidi .

Sasa nikaanza kuongea na polisi kama rafiki yangu wa kawaida tu , nikamuuliza kuhusu yule jamaa aliyeletwa pale ana makosa gani mbona wamempiga vile na kumuweka mahabusu bila maelezo yoyote yale si makosa ?

Hili ndio jibu lake

“ BWANA WALE NI PCB WANAJIFANYA WANAPESA ZA MOTO WAMEKAMATA WENZETU NA LEO TUMEMKAMATA YEYE , MUACHE TUMUONYE , NI JAMAA WA RUSHWA WALE “

Jibu hili lilitosha kunionyesha ndani ya chombo hichi cha usalama kilivyo , kumbe polisi nao wanawatafuta PCB na PCB wanawatafuta Polisi , CID wanawatafuta askari wa kawaida na kadhalika mambo kama hayo

Kwahiyo hata wewe siku moja ukiamua kumshitaki polisi au kumweka sehemu mbaya au kumuharibia ujue kwamba yule polisi ana ndugu zake na jamaa zake wengine na wakati mwingine wakati unaenda kumtia matatizo huyo polisi wenzake walikwepo wanakushika sura

Sasa siku moja , wanaweza kukutafuta tu , kama alivyotafutwa Huyu jamaa wa PCB inasemekana amepewa kesi ya ajabu ajabu , ambayo hana dhamana kwa sasa hivi

UNAONA SASA ?

KAZI IPO
 
kaka huku dodoma zimeibiwa laptop kama 20 mahali fulani kwa hiyo inawezekana hiyo ikawa moja wapo.
ngoja nifuatilie nione kama hilo jina litakuwa ni moja kati ya watu walioathirika na wizi huo katika taasisi moja nyeti
 
Kama nilivyosema siku zilizopita huyu polisi ana mambo tena makubwa sana halafu inaonyesha anacheo kakubwa kidogo pale ndani polisi wenzake wakimwona wanamwongopa wanatikisika akisema kitu kidogo wanamfuata na kumsikiliza kwa umakini mkubwa sana .

Siku ya jumatano ya wiki hii asubuhi wakati natoka tabata kuelekea mwenge akanipigia akaniambia kwamba kuna mtu ameibiwa laptop aina ya mackintosh kwahiyo huyo mtu ataenda pale officini kwake muda mfupi ujao halafu atanipigia simu

Nilivyokata hiyo simu akapiga tena akaniomba niongee maneno haya wakati yule mtu akifika office kwake “ akifika hapa nitakupigia simu kwa loud speaker , jifanye wewe ndio ulinitafutia laptop halafu muulize mbona hamtulipi hela nzuri tukiwafanyia kazi zetu ? muombe kama laki 2 hivi za kuanzia kazi hiyo na mwambie inaweza isipatikane au ipatikane halafu kazi nyingine zote niachie mimi “ huyu ndio CID mwenyewe ananiambia niongee maneno hayo ili yeye aweze kujipatia chochote kutoka kwa yule jamaa .

Bahati nzuri wakati ananipigia nilikuwa nimeshafika sehemu Fulani na kuwaambia wale jamaa wawe mashahidi wa kitu ambacho polisi anataka kifanyike alivyopiga nikaongea kama anavyotaka yeye , ili afurahie na ili asinisumbue mimi siku hiyo kwa kuwa nilikuwa na shuguli zingine zaidi .

Nashangaa kwa nini serikali au jeshi la polisi linakabidhi kazi za kutafuta au kuhakiki vitu vya mawasiliano kama simu , computer , radio na kadhalika kwa watu ambao hawajui vifaa hivi vinavyofanya kazi hata mtandao wake ulivyo na taarifa zake zingine ?

Mfano huyu polisi anamiliki laptop ambayo sio yake ni ya mtu mmoja anayeitwa Gabriel Shirima wa iLulu Dodoma ni fujitsu seamens , sasa zile data za mtu anayeitwa Gabriel ziko mule ndani bado , programu zake na mali zake zingine , polisi hajui afanyie nini hajawahi kushika computer au hata kukaa nayo karibu

Lakini ndio huyo huyo watu wanaenda kumpa kesi zao awatafutie mali zao zilizopotea kama computer na simu , sasa yeye atafanyaje kazi hizi kama hawezi kutafuta ushahidi ambao unaweza kumtia mtu matatani kama anazo au amekamatwa nazo ?

Mfano polisi anapomkamata mtu na vitu kama laptop huwa anaulizia risiti na nyaraka zingine apewe ili ahakiki , je huyu mtu akienda kuforge hizi risiti na nyaraka zingine halafu arudi kuletea polisi ? polisi atakuwa na ushahidi gani kwamba ndio vyenyewe au sio venyewe ?

Hapo mjini nimeona watu wanauza na kutengeneza risiti za maduka makubwa kama GAME , SHOPRITE na sehemu zingine na wanawauzia wafanyakazi ambao sio waaminifu wa maduka hayo au sehemu huzi , je plisi wanaweza kufuatilia kujua kwamba zile mali hazijawahi kuuzwa na maduka hayo au sehemu hizo ?

Mfano laptop zinakuwa na serial number , model number , operating systerm za version mbali mbali , na vitu vingine ambazo ni tofauti na laptop zingine je polisi wetu wanauwezo wa kuangalia yote haya ? najua hawana wanahitaji msaada tena mkubwa sana na wasilazimishe vitu sayansi iko pale pale inachotakiwa ni wao kwenda kusoma na kuelewa zaidi vitu hivyo vilivyo na vinepoelekea .
 
Nimeshakwenda Na Polisi Wameshamkamata Leo Mchana Na Yuko Mikononi Mwao Ingawa Ndugu Zake Wananiomba Tumalizane
 
Hamna kumwacha, ila wewe badili namba yako ya simu ili wasikusumbue zaidi. Waeleza jamaa wa PCB yaliyompata mwenzao........sheria itachukua mkondo wake hapo!!!.
 
safi sana shy na wanaosema udaku to hell wit them najua hayo mambo yanatokea kila siku na ndio hali halisi ya idara yetu ya polisi iliyojaa rushwa na ubadhirifu...kuna kila sababu ya kuendelea kutoa hizi story,keep it up bro!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom