Huyu mwanamke simuelewi, naomba ushauri

Huyu mwanamke simuelewi, naomba ushauri

Kuna mambo munatakiwa mukae chini na muyajadili na kuyaongea kwa marefu, then kila mmoja ataamua ipi ni njia sahihi,.
Mkuu sasa hivi tuko kwenye bonge la mgogoro, kwa sababu zingine nimemueweke tinted leo siku ya 3 anatuma msg na kupiga simu. Kaomba msamaha lakini bado anakataa kukiri jambo fulani. Nimesema ntaleta mrejesho.
 
Mkuu sasa hivi tuko kwenye bonge la mgogoro, kwa sababu zingine nimemueweke tinted leo siku ya 3 anatuma msg na kupiga simu. Kaomba msamaha lakini bado anakataa kukiri jambo fulani. Nimesema ntaleta mrejesho.
Basi na muyazungumze mkuu, kila mmoja awe wazi kwa mwingine, coz suspicious yko kwake yaweza kuwa wrong na ukapoteza mke wa maisha yako. Vivyo hvyo yaweza kuwa kweli na ukapoteza mda wako. Naamin sana ktk mazungumzo,.
 
Basi na muyazungumze mkuu, kila mmoja awe wazi kwa mwingine, coz suspicious yko kwake yaweza kuwa wrong na ukapoteza mke wa maisha yako. Vivyo hvyo yaweza kuwa kweli na ukapoteza mda wako. Naamin sana ktk mazungumzo,.
Hili nalihofia sana. Dogo amekuwa mpole ghafla ni kweli nimekuwa suspicious na ukweli siujui....hata kama ikiwa kweli haina issue coz jamaa nnayemhisi ameshaowa na hayupo hapa Tz kwa sasa. Kuna kitu tatizo naye haweki wazi.
 
Habari za Jumamosi wakuu.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Nina rafiki wa kike ambaye nishamweleza kinaga ubaga nia yangu ya kumuoa. Yeye ni mwanafunzi wa chuo na Mungu akipenda atahitimu mwakani miezi ya mwanzoni.

Kuna kitu kinanitatiza sana kuhusu yeye na mpaka sasa sielewi. Ni hivi, licha ya kwamba namhitaji kwa ajili ya ndoa na akashauri nimsubiri amalize masomo; mwezangu amekuwa msiri mno. Hapendi uhusiano wetu ufahamike kwa watu wake wa karibu. Mfano, nilikuwa na mawasiliano na dada yake lakini akanikataza kwa kuniomba nisiendelee kuwasiliana naye. Yaani niwe nampotezea, sababu dada yake ni mapepe kidogo. Binafsi sikuona sababu ya msingi ya kunifanya nimpotezee kabisa kabisa. Siku hizi sioni hata akinisalimu kama ilivyokuwa kawaida yake nahisi naye amemkataza kuwasiliana nami.....ingawa alikataa kuwa hajamuambia dadake afanye hivyo ila ni mimi tu ndio ameniomba nisitishe mawasiliano ya mara kwa mara.

Kingine ni katika mazungumzo yake hasa ya message baina yetu. Anaweza kusema "mimi atakayeniowa asifanye hivi au vile" wakati anajua kabisa mi huwa sifanyi hivyo. Mfano leo kasema "mwanaume akija kunichumbia akifanya......aende tu akaowe pengine, sio lazima anioe". Hapendi kuzungumzia our future. Ni kama yuko nami ila bado room iko wazi kama akija mwingine anaweza kuconsider, kutokana na hayo maneno yake yanayonirudia rudia. Alishawahi kumuonesha mama yake picha zangu na kumpa habari zangu. To the top of her CRAZINESS alimuonesha na pic ya jamaa mmoja yuko nje ya nchi ila anataka kurudi bongo akaomba atafutiwe mchumba msomi. Anti yake (binti) ndio alimpa habari hizi na akamuonesha picture (ya jamaa) naye akamuonesha mama yake. Mama yake wanted to know more about me kuliko mchizi wa nje. Story hii kaniambia yeye mwenyewe. I didn't buy the story though. Akiwa kwao mkoani huwa nampigia simu natafuta sababu (mfano akiwa anaumwa) niongee na mama yake ila huwa anakwepesha jambo hili.

Niwape kidogo kuhusu yeye. Mwanzo nilipimtongoza alikataa.....akisema tuwe marafiki tu wa kawaida. Kama mwanaume atampata tu atakapomaliza masomo na hajajua wazazi wake watampangia nani wa kumuowa. Nikakomaa kiume kweli kweli ndio akanielewa. Akawa mtu wangu wa karibu sana akanipa VITU vingi sana mpaka siri za familia yao na kuniamini sana. Kati kati hapo akayumba.....mapenzi yaliyumba mno. Akisingizia ni ubusy na masomo. Niliona huyu binti ni pasua kichwa. Nikapanga kumwacha aendelee na maisha yake, nikaanza kumpotezea pole pole nami nikijifanya niko busy na kazi zangu.

Alipoona reaction yangu hiyo...akajirudi na kuomba tuwe kama zamani. Na hapa naomba niwe wazi, siku moja tulikuwa tunapata chakula mahali fulani akaona kuna simu imeingia ikampa mashaka na niliyekuwa naongea naye. Hakuniuliza pale pale. Tulipoagana ndio akafunguka kuwa anahisi nina mtu, na roho inamuuma. Sikumficha....nilimuambia yule dada huwa ananisumbua na ni mtu mwenye wadhifa tu. Akahoji kwanini ananisumbua....nikamwambia yeye hudai nimekuwa mtu wa mawazo sana...so anataka kunijulia hali na kunifariji. Baada ya kisanga hiki ndipo akaona threat na kujirudi kwa kuomba msamaha kuwa ni kweli amekuwa mbali nami kiasi napata stress.

Ni mtu anayependa sana dini na ana misimamo, hili nalipenda bila shaka. Anapenda sana privacy na hana marafiki wengi. Sio muasherati hili nina uhakika nalo. Niseme ukweli, NAMPENDA SANA huyu binti na anajua hilo. Nimekuwa nikimsaidia hili na lile na sometimes naogopa kutumia pesa yangu nyingi kwake sababu sijamuamini bado. Simsomeshi, bali namsaidia kiasi ambacho am willing to loose. Naogopa kuja kulia baadaye. Na najiona kama nabet kwake juu ya hatma yetu.

Binafsi namuona bado hajafanya maamuzi rasmi ya kujicommit kwangu au bado hajakuwa kiakili....japo mi siamini to the latter. Nimepanga kumuambia kuwa nimefikiria tuachane nione reaction yake. Akinipa go ahead....I'll leave her for good. Niko tayari kwa lolote. I don't need to beg to be loved.

Unanishauri nini? Samahani kwa uzi mrefu.

mwanamke anaye kupenda na mwenye nia na wewe ana mambo ya TBS sana
 
Mkuu sasa hivi tuko kwenye bonge la mgogoro, kwa sababu zingine nimemueweke tinted leo siku ya 3 anatuma msg na kupiga simu. Kaomba msamaha lakini bado anakataa kukiri jambo fulani. Nimesema ntaleta mrejesho.
Jambo gani kakataa kulikiri?
 
Jambo gani kakataa kulikiri?
Kuna story alinisimulia about her friend naye yuko involved. Within the story kuna vitu nimehoji haweki wazi....na kasema hayuko tayari kuzungumzia tena about that story na hatajibu chochote. Kuna kitu kiko hidden na hataki kukiri hicho ninachokitilia shaka.
 
Kuna story alinisimulia about her friend naye yuko involved. Within the story kuna vitu nimehoji haweki wazi....na kasema hayuko tayari kuzungumzia tena about that story na hatajibu chochote. Kuna kitu kiko hidden na hataki kukiri hicho ninachokitilia shaka.
Kitu gani? Mkuu ungefunguka hapa ili usaidike kizuri zaidi tuko wadada humu tungekusaidia! Wee unzafcha ficha shauri yako!
 
Anayekupenda anakuwa HANA mambobya TBS au ana mambo ya TBS?

mwana mke mwenye mambo ya TBS utashindwana naye na si mke wa kuweka ndani ni sawa kukalibisha ugonjwa wa moyo
 
Wewe usimumuwazie sana mwishowe ukapatwa na vidonda vya tumbo.. mpotezee kiaina tu ila akipata muda anakuja unakula unatulia
 
Kaweka msimamo. Nimemtishia asinitumie text zake asipoweka bayana jambo lake kakomaa poa.
 
Nimepanga kumkaushia for 3 more days. Let's wait.
 
ukiona msichana hataki uwe na ukaribu na familia yake mfano dada au ndugu wengine huyo hataki commitment na wewe. tena huyo ukiweza unamwacha kimya kimya kama vile upo ila ndo unaondoka mdogo mdogo.
 
You are wasting your time, mkuu...

Inauma lakini hamna namna, jiongeze tu.
 
Back
Top Bottom