Huyu mwanamke namuacha rasmi

Huyu mwanamke namuacha rasmi

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] si ndo hapo chacha, mnakomaa na demu mmoja utazani mama yako. Achana naye tafuta mwingine. Maneno ya wakubwa yanamadhara sana. Mzazi anapokuamhia ktu kaa chini fikiria mara mbili kabla ya kulipotezea wazo lake lakini wazee wetu wanakua wameshajionea mengi. So ushauri wangu ni kwamba PIGA CHINI
Yeah! Nikweli wazazi wanakuwa wamepitia mambo mengi magumu ambayo sisi watoto hatujayafikia
 
Dah, mkuu naona kama wewe ndiye mwenye matatizo hapa.

1. Unaonesha bado hujakubaliana na maelezo yake juu ya kilichotokea kuhusu mtoto. Hivyo, ingawa humuambii, lakini moyoni mwako unajua huna amani wala imani kubwa ju yake.

2. Ngono ni kitu kimoja powerful sana. Kilimuangusha hadi mfalme Daudi. Ukifanya ngono na mtu kuna maamuzi mengine baadaye ukija kuyawaza huamini kama uliyafanya. Dunia ya sasa imefanya ngono kuonekana kuwa kitu cha kawaida (kuingizia na kutoa) lakini kiuhalisia ni very powerful. Kama utaweza, mkae walau mwezi (ningependekeza ile formula maarufu ya siku 90) bila kufanya ngono. Muishi kawaida na kushirikiana mambo mengine. Kama baada ya siku hizo 90 utajisikia bado unampenda na kumhitaji basi tutahamia point ya 3.

2 (b). Kama ukigundua upo naye kwa kuwa ni mzuri wa sura na umbo na kwamba yupo tayari kwa ngono kila unapomhitaji then naamini unajua cha kufanya. Hiyo pia itasaidia kujua kinachokupa hesitation huenda ni ile 'nimemzoea' tu na si upendo kama ambavyo unajiaminisha.

3. Ukigundua kuwa unampenda kweli na mnaweza kuishi pamoja na kupanga na kufanya mengine bila kuwa na kiunganishi cha ngono, basi fanya jambo la busara ambalo naamini ungependa dada zako wafanyiwe. Nenda kamchumbie mfunge ndoa. Muoneshe unamthamini. Kisingizio cha kusema mtoto wa kwanza hukumpata ndani ya ndoa hakitosi kuhalalisha yeye kushika mimba yako sasa. Wanasema kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa. Kila siku tunaimba hapa kuwashauri single mothers kutorudia hayo (hapa nakumbuka maushauri tunayompaga dada mmoja anajiita Anna pita ). Kama kweli unampenda, umepata amani ya yote yaliotokea na hutokuja kuyatumia baadaye kumuumiza (ni muhimu sana upate amani ya moyo juu ya haya) basi fanya hima mfunge ndoa. pamoja na kwamba dini zinatutaka hivyo lakini kisheria itamlinda yeye na watoto.

4. Hili jambo nimelifikiria leo wakati nawaza ya kwangu. Ndoa ni jambo la ajabu sana. Yani unaondoka kwa watu uliounganishwa nao kwa damu (mama yako) na kwenda kuishi na mgeni (mkeo) na tena anakuwa na priority kuliko mama yako wa damu. Ni fumbo ambalo nimewaza nikakosa jibu. Lakini point yangu ni, unapofanya uamuzi huo (kama ni wa imani basi omba sana) jua ni uamuzi unaotakiwa 99% uwe ni mawazo yako peke yako. Ukichanganya ushauri wa watu juu ya nani uwe naye hamtofika mbali. Simaanishi upuuze ushauri wa mama yako lakini jitahidi sana kufanya maamuzi yako. Hata ukimuacha huyu.

5. Hii nimarudio lakini nadhani ni ya muhimu kuisema tena. Maelezo yako yanaonesha bado una 'reservations' juu ya binti. Bado una kusitasita juu yake, maelezo yake na huna amani 100%. Jitahidi sana kabla hamjapeana mimba uwe umesuluhisha hili moyoni mwako. Umewaficha ndugu na wazazi juu ya mtu unayetuambia unampenda. Mimi hapa naona red flag kubwa mno...ni vile nikiandika zaidi utachoka kusoma.



MWISHO nisaidie kumpa hongera huyo binti kwa kuweza kujilinda asishike mimba ya pili kabla ya ndoa. Kwake ndoa ni muhimu ila inaonesha kwako haina uthamani wowote (sikuhukumu though). Ila mpe hongera zangu na ukiweza muambie akuepuke mpaka pale ambapo definition zenu za maisha (hasa ndoa kwa hapa) zitakapofanana.
Mkuu nakupa hongera sana kwa kuandika maneno ya busara kwa hisia sana but kitu ambacho nataka kuongezea kwako ni juu ya upande wa pili kuhusu hawa wadada ambao umesema kuwa baadhi ya wavulana wanawaforce kupata mimba kabla ya ndoa naweza sema wakati mwingine wanaume wako sahihi unajua kivipi, unaweza ukawa ktk mahusiana na binti ambaye amesha toa mimba/kula vidonge vya kuzuia mimba kwa mda mrefu na huenda hata kizazi chake kikafa je hauoni kama ukija kumuoa inaweza kuwa tatizo ktk familia kiasi cha kuwasingizia wachawi kuwa huenda amelogwa kumbe alijiloga mwenyewe. Je nikipi kilicho sahihi
 
Mkuu nakupa hongera sana kwa kuandika maneno ya busara kwa hisia sana but kitu ambacho nataka kuongezea kwako ni juu ya upande wa pili kuhusu hawa wadada ambao umesema kuwa baadhi ya wavulana wanawaforce kupata mimba kabla ya ndoa naweza sema wakati mwingine wanaume wako sahihi unajua kivipi, unaweza ukawa ktk mahusiana na binti ambaye amesha toa mimba/kula vidonge vya kuzuia mimba kwa mda mrefu na huenda hata kizazi chake kikafa je hauoni kama ukija kumuoa inaweza kuwa tatizo ktk familia kiasi cha kuwasingizia wachawi kuwa huenda amelogwa kumbe alijiloga mwenyewe. Je nikipi kilicho sahihi


- Umeshawahi kufikiria unafunga ndoa kisha unakuja kugundulika mbegu zako hazina nguvu za kutosha kurutubisha yai?

- Umeshawahi kufikiria kuwa mnaweza kuwa wazima kabisa halafu mkeo kila akishika mimba baada ya miezi michache inatoka?

- Umeshawahi kufikiria mkeo baada ya kujifungua mtoto wa kwanza akashindwa kushika ujauzito tena?

- Umewahi kufikiria umempa binti ujauzito na mwezi mmoja baada ya ndoa mimba inatoka?

- Umesahwahi kufikiria yule aliyelala na bibi harusi, siku moja kabla ya harusi, na wala si bwana harusi?

- Umeshawahi kufikiria?

Sasa kabla sijakujibu naomba niseme hivi pia;
- ninapenda watoto, ninatamani Mungu anibariki na watoto watokao viunoni mwangu, damu yangu.


Ikitokea hayo niliyoyaandika hapo juu nitaumia sana...na hapo ndipo wazee wanapokuambia hayo ni majaribu ya ndoa. Sina majibu kwayo kama ambavyo sitarajii wewe kunijibu.

Point yangu ni, dada zetu wengi tumewaacha single parent kwa visingizio hivi hivi. Ushauri mzuri, kama wataka kufahamu kama ana kizazi ama la, nendeni hospitali mkapime kabla ya ndoa. Kuna vipimo vya kila aina vya kufanya ambavyo havihitaji kutiana mimba kabla ya ndoa. Tena mtapima hadi damu na kila kitu mtakacho.

Point ya pili ni, huenda vijana wengi siku hizi hatujafunzwa kwa nini watu wanafunga ndoa. Kumbuka misingi ya ndoa haikuletwa na dini, ilikuwepo enzi za mababu zetu. Kidini, ni kukamilisha mipango ya Mungu, kupata baraka na kutohesabiwa dhambi ya uzinzi.

Kiserikali ni mkataba halali utakaosaidia hao unaowapenda (mkeo/mumeo na wanao) hasa endapo hutokuwa tena duniani.

NDOA ni muhimu sana...ni muhimu zaidi kupata watoto ndani ya ndoa. Tuachane na visingizio vya zamani enzi ambazo teknolojia haikuwepo. Tumesoma..tuoneshe tofauti hiyo.

Kila la kheri mkuu..kama kweli unampenda, unamthamini, utamdhihirishia kwa kuanza na ahadi ya ndoa. Mvishe shela kalba ya 'tiniti'.

Sote tunapenda watoto na hakuna anayetaka kuoa mwanamke asiyeweza kuzaa, kama hiyo ni priority kubwa kwako basi zungumzeni hilo mkafanye vipimo, usimpe shida binti wa watu. Kuna a lot more uncertainties kwenye maisha na ndoa ambazo kumtia mimba kabla ya ndoa hakutakupa jibu...PLEASE mkuu. Natumai nimeweza kukujibu vyema. Tuwapende na kuwathamini dada zetu ila nadhani zaidi tujifunze nini hasa maana na lengo na kufunga NDOA; kidini na kisheria/serikali.


Heri ya pasaka kwenu nyote.
 
Mentor upo sahihi kabisa hakuna asiyependa kuwa na watoto, shida inakuja kumwangukia mwanamke, sawa anaweza katoa mimba sawa lakini huyo mme akawa hana uwezo wakumpa mimba, nachojiuliza kila siku mkemia anaongea %kubwa watoto wanaozaliwa si wababa walio olewa na mama zao sasa mpaka wanapewa mimba na wengine wenyewe wanakuwa wapi? Mungu ndiye mueza wa yote anampa huyu yule anamnyima na ukipata asichekwe asiye kuwa nacho, lakini binadamu wakaidi sana
 
Uko darasa la sita au la saba mkuu? Ushasema unamuacha rasmi that means ushaamua afu tena unaomba ushauri!!? Muulize mwalimu mkuu wako hapo skonga
 
Mpaka hapo wewe ndio msumbufu.. Tena umshenzi usiye na huruma... Hebu muweke dada yako ktk hiyo nafasi ya huyo bint... Wewe unataa uhakikishe nini sasa? Mana bora angekuwa hajazaa ungesema labda u confirm kwamba anauwezo wakukuzalia ndio umuoe.. Jengine eti wataka mtoto kwa kulipizia usumbufu aliokupatia awali... Kijana huna huruma hata chembe... Na nampongeza bint ametambua dhumuni na ulaghai wako..



Kuhusu kiburi au jeuri za bint.. Sikuzote fuata ushauri wa wazazi mana wanaona mbali..
 
Wanaume sijui mnatakaga nini. Tayari ushajua anauwezo wa kuzaa. Afu unataka mpaka apate mimba.
Embu kuweni na huruma basi.
 
Wanawake wote ni jeuri, aisee cha maanankwenye ndoa ni upendo, kama anakupenda na wewe unampenda muoe aisee. Usije ukarogwa ukaoa mwqnamke usiyempendaz maana mwisho wa siku mamako haishi nanhuyo dada, its you and her
 
Back
Top Bottom