Huyu muuaji kwanini sura yake inafichwa!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu muuaji kwanini sura yake inafichwa!?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BAK, Oct 25, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,307
  Trophy Points: 280
  KESI YA MWANGOSI: Mtuhumiwa afichwa sura

  na Gustav Chahe, Iringa|Tanzania Daima

  JESHI la Polisi mkoani Iringa, limeendeleza usiri mkubwa wa kumficha mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.
  Ikiwa ni mara ya tatu kwa mtuhumiwa huyo, Pasificus Cleophace Simon (23), kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jana, ulinzi mkali ulitawala eneo hilo, huku waandishi wakipigwa vikumbo wakizuiwa kupiga picha.

  Askari wenye sare wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakiwa na virungu, silaha za moto huku wengine wakivalia kiraia, walitanda mahakamani hapo kuhakikisha hakuna mwandishi anampiga picha mtuhumiwa huyo.

  Katika patashika hiyo, mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Eliasa Ally, alijikuta akipigwa na askari ambao walikuwa wakimzuia kupiga picha.
  Askari aliyempiga mwandishi huyo alitambulika kwa jina moja la Idirisa, na hivyo tukio hilo likazidisha uhasama baina ya jeshi hilo mkoani hapa na waandishi wa habari.

  Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani akiwa amevalia jaketi lenye kofia iliyomfunika kichwa kizima kiasi cha sura yake kutotambulika.
  Akiwa mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka ya mtuhumiwa huyo, Lilian Ngilangwa, alimweleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Dyness Lyimo, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

  Lyimo aliomba kesi hiyo ihairishwe hadi Novemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.
  Pasificus alifikishwa mahakamani hapo, akidaiwa kumuua kwa makusudi Mwangosi wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, mnamo Septemba 2, mwaka huu.
   
 2. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Hakuna kesi hapo, kinachofanywa ni kiini macho tu.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Na hata ukute hakai mahabusu ya kawaida anawekwa sehemu ingine kabisa anasubiria siku ya kesi wanamleta!kuna usanii wa hali ya juu hapo!!
   
 4. Master jay

  Master jay Senior Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 187
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kawaida mahakamani huruhusiwi kuvaa kofia yoyote zaid bharakashia, au kama una tatizo la ulemavu wa ngozi km albino. Inakuwaje hapo? Hz mahakama na lockup ni kwa ajili yetu walalahoi lkn c kwa 'wanunuzi wa kura'
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  wanamficha sura kwa sababu yule sio muuaji wa D.Mwangosi.......kwahyo akimaliza kazi yake ataachiwa mtaani so akionyeshwa sura anaweza akauliwa pindi kiini macho(Bongo movie) ikiisha pindi akionekana mtaani
   
 6. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  "Kwa sababu siyo yeye muuaji ili msimjue"
   
 7. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,864
  Likes Received: 4,246
  Trophy Points: 280
  Hata wamfiche muuaji ni muuaji tu, usanii duniani peke yake.
   
 8. M

  Malova JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  sura yake inafichwa kwasababu si polisi ni green gard aliyevishwa nguo za polisi
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ameshajulikana hata akifichwa haisaidii hata kidogo!!! Wanajisumbua!! But Mungu anamuona!!
   
 10. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  umeona eeh!
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Tukiacha mizaa! Serikali ina chofanya ni makosa na ina jaribu kuficha na kuharibu ushhidi!
  Cha kujiuliza.
  1: kwanini ana fichwa sura wakati ana julikana kama ni muhusika wa tukio lile?
  2. Je ni nani katika wanachi ana ye ijua vizuri sura ya huyo askari?
  3: Kama wananchi wanamjua huyo askari kwa sura na kuna ushahidi kwa nini wana lalamika?

  Hadi sasa ni dhahiri kabisa kuna uwezekano ushahidi unaendelea kuchakachuliwa

   
 12. Rich 4rever

  Rich 4rever Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inchi jamani kunamambo inabidi wafanye mahamuzi magumu kwa nn wanakumbatia wahalifu kiasi hiki.kwa jinc hii ni watu wa hali ya chini ndio dhahama za kimahakam halali yao aisee inatia hasira,zaid hako kamchezo ka kutufanyia kiini macho ni mbayaaaaaa!!
   
 13. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa fair kisheria huyu bwana bana ni mtuhumiwa tu na bado ni innocent mpaka hapo atakapothibitishwa na mahakama kuwa mweli alitenda kosa analotuhumiwa kutenda.

  Kimaadili ya kazi ya kiuandishi wa habari, waandishi nao wanapaswa kuzingatia swala la innocence until proven guilt by the court of law.Wasifanye kazi kiushabiki tu kwani wanakuwa wanahukumu mtu ambaye bado hajahukumiwa na mahakama ya sheria.

  Kikubwa tunachoweza kuserma ni kuwa polisi wanatumia ubabe kuficha sura ya huyu bwana kwa sababu swala hili linawahusu, ni askari polisi mwenzao.

  Zaidi ya hapo waandishi wana uwezo na hawazuiwi kupata picha ya huyu bwana na kuiandika magazetini, mradi tu wajue kuwa kwa kufanya hivyo wanaheshimu haki ya huyu bwana kwamba bado hajapatikana na hatia na wasimuweke katika mazingira ambayo atahukumiwa na jamii kabla hata ya hukumu kufanywa na mahakama.

  Kumbuka huyu bwana anaweza pia kuwachukulia hatua za kisheria waandishi wa habari kama watamdisplay katika jamii kwamba yeye ni muuaji wakati bado hata shauri lake halijasikilizwa na mahakama. Swala hili litakuwa na nguvu zaidi hasa kama mahakama baada ya kuendesha kesi yake ikampata kuwa hakuwa na hatia, kwani hapa machapisho yaliyofanywa magazetini yatakuwa yamemletea picha mbaya kwa jamii, na hiyo itakuwa ground kubwa sana kwake kuwachukulia hatua za kisheria waandishi hawa.

  KUMBUKA NI MAHAKAMA PEKEE AMBAYO INAWEZA KUTHIBITISHA MTU YEYOTE KUWA NA HATIA AMA KUTOKUWA NA HATIA....
   
Loading...